Waraka maalum wa kujivua Uanachama ndani ya CCM

Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,626
2,000
Kama kweli CCM huwa wana iba unayo yasema wewe ndio wana yatekeleza sishangai kwa nini nchi iko hivi. Na tusha umia jumla jumla

Kama kweli wewe ni mwalimu, ni hatari kwa wanafunzi wako kwani hauko sawa.
 

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
2,000
Kama wewe mwalimu nawaonea huruma hao wanafunzi kama wewe ndo mwalimu uko hivi je hao wanafunzi unaweza kuwa coma moto wote?
 

Punnisher

JF-Expert Member
Jul 28, 2014
798
1,000
WARAKA MAALUM WA KUJIVUA UANACHAMA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI- CCM.

Leo 29 January 2017, Mimi Deogratius Kisandu niliyejiunga CCM tarehe 27 September 2014 na kupokelewa na Mh. kinana Katibu Mkuu wa CCM na Mh. Nape mwenezi wa CCM wilayani Lushoto,Tanga katika kata ya Mlola. Leo ninatangazia umma wa Tanzania kuwa nimeipa talaka CCM. Kuanzia Leo Mimi sio Mwana chama wa CCM tena.

KWANINI NIMEIPA TALAKA CCM.

Kuna mambo mengi sana maovu na ya kinyama yaliyofanywa juu yangu na CCM na viongozi wake kwa miaka mingi sasa. Kwakuwa wao kama chama wameshapanga tangu zamani kuwa nikitaka kuondoka CCM watajifanya kama walikuwa hawajui maovu na unyama uliokuwa unaendelea. Hivyo Mimi sio mtoto mdogo najitambua na ninajua nafanya nini.

CCM kila mtu anatumia nafasi yake kudhalilisha walio chini. Huwezi amini Balozi anauwezo wa kumdhalilisha Mtanzania mwenzie kisa anategemea nguvu ya DC au RC au agizo la Waziri Fulani.

Kesi nyingi za Watanzania ni za kubambikwa ambao ndio mchezo mchafu unaochezwa na CCM, hata hivyo wameahidi kuniteka kama nitaondoka CCM, Mimi nasema Niko tayari. Japo viongozi WA juu wa CCM wao wamepanga nifunguliwe kesi yoyote ili kunizima kisiasa tena wakitaka kuniondolea sifa ya kugombea Urais 2020.

Nachelea kusema vijana wengi kutoka upinzani watabambikwa sana kesi ili wapoteze sifa ya kugombea 2020, na kuna ma DC na Ma RC wanataka majimbo 2020 hivyo wanatumia fursa hiyo ya udhalilishaji wa kubambika kesi ili wenzao wapoteze sifa 2020 na wao wapate kugombea majimbo hayo.

Katiba ya CCM inasema DC na RC ni wajumbe katika vikao vya CCM wilaya na MKOA. Hivyo sishangai mateso niliyopata kuagizwa na wajumbe hao. Wapo Mawaziri walio wahi kuagiza nibambikwe kesi lakini watu wema wakakataa.

CCM wanatumia maandiko yangu ya mitandaoni kuongoza Nchi, CCM wanatumia Vitabu vyangu kuongoza nchi(Utani wa serikali na Wananchi, kijarida cha Ukombozi wa Pili wa Taifa Letu) halafu wanakana kwamba sio Mimi, tena mwezi Jana kunamtu kawavujishia kitabu changu kipya cha Mwanamalundi, na wameiba mawazo yangu na kuanza kuyatumia, huku wakijipanga kunipinga.

Kadi yangu ya CCM niliyopewa Lushoto ni No. AF 5864962. Na kwa utaratibu wa CCM nilienda kwenye tawi la Shunu, Kahama ,Shinyanga ili kunitambulisha na kupewa kadi No. AI 8229534 na kwenye daftari ni mwanachama wa 905.

CCM ni chama kisichokuwa na mawasiliano kila kiongozi anaweza Fanya jambo bila kutoa taarifa kwa mwenzake. Kwa mtindo huo ni rahisi sana hata kufanya mauaji maana hakuna kutarifiana. CCM watu wenye nguvu kama Deo Kisandu wanawekwa Vizuizini na kuwekewa vikwazo vya kimaisha ili Wafe au wadhalilike na wao kunona.

CCM inahitaji wana chama ambao ni Wababaishaji na waongo waongo ndio ambao wanafaa kwa mamlaka yao.

Mimi Leo nimekuwa kama CHOKORAA na ni baba wa watoto, basi wao CCM ndio furaha kwao. Upuuzi huu waliufanya mpaka kwa marehemu Mzee wangu. Sasa imefika tamati.

CCM wanaagiza watu waniwekee makamera na vinasa sauti darasani nikiwa na fundisha halafu baada ya siku mbili unasikia DC au RC au Waziri kaibuka na ajenda zangu. Wamekuwa pia wakinitegeshea makamera sehemu Nazo panga vyumba vya kuishi ili wapate mawazo yangu watumie kuongoza nchi.

CCM wanapanga kunidhulumu hata mashamba, CCM wanatembelea NYOTA YANGU ili wang'ae. Mungu hadhihakiwi, tutashuhudia mengi ya kuboronga ndani ya CCM. Kuniua hamuwezi, labda mkakati ule wakunihamisha kituo kwenda kijijini.

CCM nawatakia safari njema ya utawala wenu, jitazameni sana,,,,siasa za kufanyiana unyama zimefika mwisho.

Hata hivyo bakini na CCM yenu, na sisi tutasajili chama kipya cha Arena for Correcting Africa-Tanzania (ACA) na usajili lazima mtupatie maana ni haki yetu Kikatiba. Nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi.

Wana CCM muda mrefu wamekuwa wakisema Deo Kisandu tusimfukuze Bali tusubiri aondoke mwenyewe halafu tugawane vyeo. Haya sasa nimeondoka gawaneni vyeo, tumeni na Polisi waje wanikamate kwa utovu wa nidhamu.

Kwaherini Majembe ya CCM. Ninyi ni majembe sana nawakubali sana. Lakini mimi sio jembe, Mimi ni Mpini wa jembe.

Wakolosai 4:5-6 itawasaidieni. Najua mmepanga kuniwekea Vikwazo zaidi baada ya kunidhalilisha. Nasema nitakuwa tayari kuvunja sheria kama mtanikandamiza kwasababu zenu za kimaslahi yenu.Na Kadi yenu hiyo chukueni. Hata mkivujisha video ya kujiunga CCM mliyokuwa mmeificha haitasaidia. Endeleeni kunizushia ujambazi na ugaidi mazara yake mtayaona kwenye familia zenu soon. MUNGU ANAONA.

Ndimi:
Deogratius Nalimi Kisandu
Niliyekuwa Mwana Chama wa CCM wa Mpito.
29 Januari 2017.

MWANZA, Tanzania.
mbona sijaelewa.....kivip yani.......
 

Gaspare Mbile

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
1,508
2,000
Hongera kwa kujitoa hizo pingu,lakini usije kuwa mpango ili ukisajiri ako ka chama kako kawavuruge wapinzani kugawanyisha kura zao,usije kuwa kama Mrema kwa ufupi.
 

Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,656
2,000
Hivi kuna tofauti gani ya ugonjwa na maradhi ? Maana sasa huu sio ugonjwa tena ni maradhi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom