Waraka maalum kwa Klabu ya Yanga: Hii hapa nafasi mpya ya kujikomboa kifedha

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Kwa miaka kadhaa iliyopita, Watanzania wengi wamekuwa wakizungumza kuhusu muelekeo wa vilabu vya soka hapa nchini. Na kwa sasa, mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa vilabu hivyo, limekuwa jambo linalojadiliwa zaidi.

Klabu ya Simba ndiyo imekuwa ya kwanza kuonyesha njia ambapo mfanyabiashara Mohammed Dewji ambaye ni bilionea mwenye umri mdogo zaidi Afrika alinunua hisa aslimia 49 za klabu hiyo. Wanachama wa klabu hiyo ndio wanaomiliki asilimia kubwa ya hisa za klabu hiyo ambazo ni asilimia.

Licha ya changamoto za kifedha zinazoikabili Klabu ya Yanga, huenda nao wakafuata njia hiyo hiyo kama Simba.

Suala kwamba, wanachama ndio wamiliki wa asilimia kubwa ya klabu, ni jambo ambalo Watanzania wengi wanaliunga mkono. Hii inamaana kwamba, mwekezaji anaweza kuweka fedha zake kwenye klabu, lakini bado wanachama wakawa ndio wenye maamuzi ya mwisho. Hili linawafanya mashabiki na wanachama wale wa chini kabisa kuweza kushiriki kwenye mipango ya kufanya maamuzi.

Suala hili si jipya kwani tayari limeweza kufanya kazi katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga. Wameonyesha kuwa unaweza ukafanya uwezekezaji wa kimaendeleo kwenye klabu bila kuiuza kwa mwekezaji.

Baadhi ya vilabu hapa nchini vina lengo la kufika mbali katika bara la Afrika, hivyo uwekezaji mkubwa wa fedha ni muhimu. Lakini pia unatakiwa kuwa na matumizi mazuri ya fedha. Uwekezaji wenye tija, uhamisho wa wachezaji na nguvu ya mashabiki, vyote vinapaswa kuonekana.

Ili taifa liweze kuwa na ligi ya maana na inayoendelea kukua, mashabiki wote wanapaswa kufahamu vilabu wanavyoshabikia vinatokea wapi.

Dewji ambaye ni mwekezaji katika klabu ya Simba, karibuni aliandika kuwa, jambo lolote zuri ama baya katika maisha litakufunza kitu. Namna unavyojifunza katika maisha yako ya nyuma, ina mchango mkubwa kwa kuamua maisha yako ya sasa. Simba imepitia katika vikwazo mbalimbali, lakini Yanga ndio mfano bora wakukuonyesha namna unavyotakiwa kujifunza kutoka katika mazuri na mabaya.

Yanga ilikuwa na kipindi kizuri na cha furaha wakati wa uongozi wa Yusuf Manji ambaye alikuwa mwenyekiti wa klabu hiyo. Licha ya kuwa Manji alipeleka furaha sana mtaa wa Jangwani, lakini pia kipindi kibaya kwa klabu hiyo ni yeye amekileta.

Baada ya kuachia Uenyekiti wa klabu hiyo pasipopokuwa na sababu yeyote ile, tena kwa ghafla, Yanga imekuwa ikikabiliwa na tatizo la madeni huku ikiwa haijui pakutokea. Mwaka 2016, madeni hayo yalikaribia kufika TZS 11.6 bilioni.

Mpango wa awali wa Yanga ilikuwa ni kukodishwa kwa kampuni ya Manji ya Yanga Yetu Ltd ambapo ilielezwa kwamba, asilimia 25 ya faida ambayo ingepatikana ingerejeshwa kwenye klabu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira. Lakini kwa mwaka 2016, klabu hiyo ilipata hasara ya TZS 1.5 bilioni. Maana yake hasara hiyo ni ya Klabu, sio ya mwekezaji.

Njama za kutaka kuiendesha klabu kwa mfumo wa kibiashara ziliwaondoa wanachama katika meza ya mazungumzo na kuwafanya wao kuwa watazamaji tu wakati hali ya klabu ikizidi kuwa mbaya.

Cha kusikitisha ni kwamba, baadhi ya watu ndani ya klabu ya Yanga wanadhani kuwa Manji akirudi katika nafasi ya uongozi kutarudisha kipindi cha neema. Watu hawa wako mbali sana na ukweli kwani Manji wa leo, si wajana. Yeye mwenyewe anapambana na hali yake sasa hivi, na haonekani tena kuwa msafi au ambaye atastahili kubeba masahibu ya kifedha ya klabu ambayo yeye amechangia kuyatengeneza.

Sote tunakumbuka kuwa mambo yake mengi yaliwekwa hadharani mwaka 2017. Serikali imetaifisha mashamba yake, ameshtakiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi na pia amefikishwa mwahamani akituhumiwa kutumia dawa za kulevya. Manji aliahidi kutoa eneo lake lililopo Kigamboni (huu sijui ulikuwa mkenge maana hakukuwa na maandishi) kwa ajili ujenzi wa uwanja wa mazoezi, lakini eneo hilo ninapoandika Makala haya limechukuliwa na serikali kwa shughuli nyingine.

Kampuni ya Manji ya Yanga Yetu Ltd imeshindwa mara nyingi kufanya mambo ambayo iliahidi kwa Klabu, hivyo jambo la msingi kwa Yanga ingekuwa kutupilia mbali makubaliano ya kuikodisha klabu hiyo. Bado Yanga wana nafsi adimu ya kuunda kamati nyingine ambayo itakuwa na jukumu ya kuchagua mfumo wa wa umiliki wa klabu hiyo.

Kama Yanga wataamua kufuata mfumo wa kibiashara kama kwa watani wao Simba, basi ni vyema wakamuondoa kwenye mawazo yao Yusuf Manji kwa sababi ambazo nimeeleza hapo juu. Na kwa hali ilivyo ya kupambana na hali zetu ilivyo sasa hivi nchini kumpa Manji nafasi Yanga ni sawa na kulipa jimbo upinzani. Yanga na Simba zina siasa zake.



Manji, kama matajiri wengine mashabiki wa Yanga, Mengi n.k, anaweza akafurahia mafanikio ya klabu akiwa kama shabiki. Kama Klabu, Yanga inatakiwa kusoma alama za nyakati kwani sasa hivi, hata katika ulimwengu wa biashara, nafasi ya Manji inazidi kusinyaa kila iitwapo leo. Tukumbuka kuwa amekuwa akifanya biashara nyingi na serikali, mfano TANESCO, jambo ambalo katika miaka hii sidhani kama litatokea.

Tuendelea kuwa na matumaini kuwa mashabiki na wanachama wa Yanga wataendelea kudai mwekezezaji mwenye tija ambaye ni msafi bila kuwa na makando kando, asiye mjanja mjanga kuhonga wajumbe, mtu bora na anayeweka mambo wazi ili klabu iweze kusimama na kuwapa mashabiki burudani, vingenevyo itakuwa kile kisa cha mwekezaji aliyepewa mradi mzima kujenga Mlimani City kuwa alikuja Tanzania na mtaji wa shilingi laki moja na nusu tu.



Chambilecho!



Wanzagi Talewa

Mara, Tanzania
 
Sasa mbona hujaelezea yanga inatakiwa ifanye nn au njia gani kujikomboa ulichofanya kumpaka matope manji tu mm nadhani ww ndo wale wale tu
 
mbona umemshambulia manji badala ya kusema kama wanayanga tupite wapi? ukweli wa hali ya manji anajua manji mwenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom