Uchaguzi 2020 Waraka kwa Wagombea: Kama wewe ni Mgombea na uliwekeza nguvu nyingi kwa Vijana tegemea leo kuangukia pua kwenye kura

Mr Tyang

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
1,728
6,803
Kwenu Wana badi;

Ikiwa Ni mapema kabisa mwa siku maalumu ya Leo 28/10/2020 ambapo Hatma ya Amani ya taifa inaenda kujulikana Baadaye ningependa kuwakumbusha haya machache Wagombea wote wa Uchaguzi huu kabla ya tukio ili kwa pamoja tulinde amani ya nchi yetu.

1. Kwa Wagombea wote waliowekeza na kuweka matumaini kwa Kura za Vijana;
Kwa hekima kabisa napenda kuwakumbusha enyi wanasiasa wote kuwa, kama Kuna yeyote Kati yenu alitegemea kura za vijana Basi kesho ajiandae kisaikolojia kuangukia pua katika sanduku la Kura.

Kwanini nasema hivyo;?

Kwasababu; Kama tunavyojua vijana huwa Wana amusha amusha Sana katika kampeni Ila ukweli nikuwa Hawa Hawa vijana huwa wanajikuta Wana Mambo mengi ya mhimu na yasiyo ya mhimu wakati wa kwenda kupiga kura.

Yafuatayo Ni Mambo ambayo tegemea kuyaona kwa vijana uliofikiri Watakupatia Ushindi kwenye sanduku la kura;

1. Kama kijana Ni badoboda tambua tu kesho ataendelea na mishemishe zake za kutafuta riziki maana kesho ndo inaweza kuwa siku nzuri kwake kupiga pesa kutokana na watu wengi kwenda na kutoka kupiga kura katika vituo vyao, hivyo kura yake kuikosa kutokana na kuwa busy kutafuta pesa ni Jambo la kawaida.

2. Vijana wengi huwa hawapendi kuvumilia foreni, hivyo Kama kijana akienda kituoni kwa lengo la kupiga Kura na akakuta foreni kubwa Basi tegemea kuikosa kura yake maana ataondoka huku akifoka na kupuuza zoezi linaloendelea.

3. Vijana wengi hawajaoa hivyo ikitokea amepata appointment kutoka kwa Mpenzi wake hapo suala la kupiga kura kwake Tena halitakuwa na Maana kuliko la kuenjoy na Mpenzi wake.(Ikumbukwe leo Ni Siku ya Mapumziko). Kwa hiyo hata wale vijana ambao huishi kwa kubanwa na wazazi wao kesho Wanaweza wakapata nafasi ya pekee na wakaitumia kufanya Mambo Yao ya starehe badala ya kupiga kura.

4.Vijana wengi wana tabia ya kuchukulia Mambo easy as if Kama hawahusiki moja kwa moja, hivyo Basi tegemea kusikia maneno Kama "kura yangu moja haina shida acha nipotezee tu kupiga kura"(n.k). Pasipo kujali kuwa Kura yake moja ndo Ushindi wa ampendae.

5. Vijana wengi hawana ajira na Wana hasira Sana na wanasiasa kwa maana, hao hao wanaisiasa ndo huwapigia makelele kila siku Kuwa "Vijana jiajirini" wakati wao wapo kutafuta ajira kwa Wananchi. Hivyo vijana wengi hujikuta wamepuuza zoezi zima la kupiga Kura kama kisasi Cha Hawa watu wanaombiaga wajiajiri angali wao wanatufta ajira kila baada ya miaka5

Mwisho; Yapo mengi kuwahusu Vijana Ila machache hayo yanatosha tu kuwapa mwanga wanasiasa wote wanaotegemea kura za vijana wa kitanzania. Usipoyajua haya Matokeo yake ndo kusema umeibiwa kura Mara uchaguzi haukuwa wa haki kumbe wewe ndo ulikosea kuchagua kundi la kukupa ushindi.

Mwanasiasa yeyote au chama Cha siasa hapa nchini ambacho huwekeza kwa wanawake na wanaume na Wazee Mara nyingi huibuka washindi kwa maana Kura za haya makundi siyo rahisi kupotea kuliko za Vijana.

#Nawatakia uchaguzi mwema wa haki, huru na Amani nyote.
#Tujitokeze kupiga Kura Sote.
#Tuchaguwe Viongozi Wazuri, waadilifu na wapenda maendeleo.
#Tuilinde amani ya nchi yetu wakati na baada ya uchaguzi.
 
Uzi wako umeuleta kuonyesha kuwa "kitu fulani utakifanya ama mutafanya mkisingizia vijana kuwa hawakupiga kura!Sasa tupe Sera inayovutia Wazee itakayofanya wao wapige kura!!
 
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CCM. Yule mwenye ticket yake ya 18/12 akae kwa kutulia kabisa. Asidhani atawaamsha vijana wafanye fujo kisha akimbilie Ubelgiji.
 
Mkuu, unazungumzia vijana ama kundi lipi la vijana? Vijana hawa waliojaa hamasa kubwa sana kote nchini wenye kiu kubwa ya kufanya mabadiliko yenye tija kwao, ama unawazungumzia UVCCM na green guards ambao wamezoea vitu vya dezo?
 
Yupo mmoja alijikita sana kwenye matusi, uongo na kuhamasisha vijana kuingia barabarani kufanya fujo badala ya kueneza sera za chama chake, imekula kwake. Anashindwa vibaya, na vijana mitaani hawaendi: kwani nani hajipendi?!
 
Upuuzi tu. Unajua wazee halisi (sio wale wa NEC) wako asilimia ngapi Tanzania? Unadhani katika hao watu milioni 29 wanaodaiwa wamejiandikisha vijana watakuwa asilimia ngapi?
 
wapiga kura wa mwaka huu ni wale waliokuwa vijana mwaka 1995,2000,2005,2010.

subini tuwapapase.
 
Wewe jifungie hapo ndani kwa shemeji yako vizuri unyweshwe juice taratiiiiiibu sababu haya mambo yamekuzidi kimo
 
Wewe unawazungumzia vijana wa mwaka gani? Nipo kituoni hapa na vijana wamejaa kibao pamoja na hao wa bodaboda vyombo vyap wamepaki hapa pembeni.
 
Wewe ndio msemaji wa vijana? Hizo sababu wao ndio waliokuambia?

Au ni hisia zako za kuwakatisha tamaa wagombea wa upande fulani ili waogope kupinga matokeo pale watakapoona hawajatendewa haki kwa kisingizio kwamba kundi fulani halikumpigia kura?
 
Mungu Baba ninatubu kwa dhambi zangu na taifa letu Tz, tuonee huruma, tujalie hekima na busara tukafanye wajibu wetu kupiga,kuhesabu,kutangaza matokeo kura itakayo leta HAKI na ustawi wa taifa letu.Amina
 
Back
Top Bottom