Waraka kwa wabunge wote-- sasa ni wakati wa kung'ata siyo kubweka

greenstar

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
390
53
Waraka kwa wabunge wote-- sasa ni wakati wa kung'ata siyo kubweka
Salute kwa Wabunge wote !
Naomba niwakumbushe wabunge la JMT kuwa sasa ni wakati wa kung'ata na siyo kubweka kama mbwa koko,kwani baadhi ya mawaziri ni viziwi kwa kelele mnazopiga hapo mjengoni,wanamtandao wa kufanya umafia kwa watu wanaopiga kelele sana....Rai yangu kwenu,vaeni ngao za kivita katika kulitetea TAIFA letu lenye UTAJIRI wa kutosha lakini wanafaidi mafisadi tu,huku mtanzania akilia na ugumu wa maisha.

Achani kujidanganya na KAMATI TEULE kufanya uchunguzi maana kwa kufanya hivyo ni kuwasaliti wenzenu ili wafanyiwe mambo ya kimafia na kuwajengea CHUKI katika kazi zao au kurubuniwa wakati wanafanya hizo kazi.Tumieni mbinu za NYUKI na SIAFU katika kushambulia adui FISADI. Wote ni mashahidi juu ya watu makini walivyoweza kuhujumiwa kwa njia za kimafia (umafia hapa ni UCHAWI,AJALI,SUMU na Kumuondoa katika system za SIASA nk.).Haya mambo yapo wazi watu kufa vifo vya gafla,kuugua gafla au kupewa vyeo visivyo vya lazima ili asithubutu kupiga kelele.

Nawapongeza kwa kuwasha moto bungeni ambao natumaini hautazimika milele kama kweli mnapenda kutuwakilisha wanyonge wa nchi hii. Kama SERIKALI imeshindwa kuwajibuka basi ni zamu ya BUNGE kuwajibika,msiogope BUNGE kuvunjwa kwani SERIKALI ya mpito atateuliwa na nyinyi mtapewa DHAM<ANA ya kutekeleza yale ambayo serikali imeshindwa kufanya.Ni lazima wezi wote wafilisiwe mara moja. Tumieni hata kushawi JESHI la nchi ambalo bado ni waadilifu kwa kiasi fulani kutokana na misingi iliyowekwa na Mwl.Nyerere.

Naimani kubwa na WATANZANIA wote kuwa wapo pamoja na nyinyi katika mapambano haya ambayo yataleta mageuzi yenye TIJA kwa nchi nzima.Kumbukeni masuala nyeti kama RICHMOND,EPA,KAGODA na MEREMETA bado hayajafanyiwa kazi,badala yake zile kamati ndiyo zinaadhibiwa kwa kusema ukweli bungeni bila hata kuwatetea,hii ni hatari kwa UMOJA wenu.IPO siku wabunge wataogopa kuunda kamati kwa kuhofia vifo au hujuma ya aina yoyote.

Asanteni kwa kusoma na kupokea waraka huu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA !!
Edit Post Reply Reply With Quote
 
Back
Top Bottom