Waraka kwa wabunge wote-- sasa ni wakati wa kung'ata siyo kubweka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka kwa wabunge wote-- sasa ni wakati wa kung'ata siyo kubweka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by greenstar, Apr 20, 2012.

 1. g

  greenstar JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Salute kwa Wabunge wote !

  Naomba niwakumbushe wabunge la JMT kuwa sasa ni wakati wa kung'ata na siyo kubweka kama mbwa koko,kwani baadhi ya mawaziri ni viziwi kwa kelele mnazopiga hapo mjengoni,wanamtandao wa kufanya umafia kwa watu wanaopiga kelele sana....Rai yangu kwenu,vaeni ngao za kivita katika kulitetea TAIFA letu lenye UTAJIRI wa kutosha lakini wanafaidi mafisadi tu, huku mtanzania akilia na ugumu wa maisha.

  Achani kujidanganya na KAMATI TEULE kufanya uchunguzi maana kwa kufanya hivyo ni kuwasaliti wenzenu ili wafanyiwe mambo ya kimafia na kuwajengea CHUKI katika kazi zao au kurubuniwa wakati wanafanya hizo kazi.Tumieni mbinu za NYUKI na SIAFU katika kushambulia adui FISADI. Wote ni mashahidi juu ya watu makini walivyoweza kuhujumiwa kwa njia za kimafia (umafia hapa ni UCHAWI,AJALI,SUMU na Kumuondoa katika system za SIASA nk.).Haya mambo yapo wazi watu kufa vifo vya gafla,kuugua gafla au kupewa vyeo visivyo vya lazima ili asithubutu kupiga kelele.

  Nawapongeza kwa kuwasha moto bungeni ambao natumaini hautazimika milele kama kweli mnapenda kutuwakilisha wanyonge wa nchi hii. Kama SERIKALI imeshindwa kuwajibuka basi ni zamu ya BUNGE kuwajibika,msiogope BUNGE kuvunjwa kwani SERIKALI ya mpito atateuliwa na nyinyi mtapewa DHAM<ANA ya kutekeleza yale ambayo serikali imeshindwa kufanya.Ni lazima wezi wote wafilisiwe mara moja. Tumieni hata kushawi JESHI la nchi ambalo bado ni waadilifu kwa kiasi fulani kutokana na misingi iliyowekwa na Mwl.Nyerere.

  Naimani kubwa na WATANZANIA wote kuwa wapo pamoja na nyinyi katika mapambano haya ambayo yataleta mageuzi yenye TIJA kwa nchi nzima.Kumbukeni masuala nyeti kama RICHMOND,EPA,KAGODA na MEREMETA bado hayajafanyiwa kazi,badala yake zile kamati ndiyo zinaadhibiwa kwa kusema ukweli bungeni bila hata kuwatetea,hii ni hatari kwa UMOJA wenu.IPO siku wabunge wataogopa kuunda kamati kwa kuhofia vifo au hujuma ya aina yoyote.

  Asanteni kwa kusoma na kupokea waraka huu.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA !!
   
 2. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Trilion 14% naunga mkono hoja
   
 3. s

  sarawati Senior Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  aunga mkono hoja mia kwa mia'''
   
Loading...