Waraka kwa Pwagu and Pwaguzi and company & sons

Zionist

JF-Expert Member
Dec 5, 2017
1,830
2,881
Wasalaaam,
Mimi ni mzima wa afya, naendelea vyema na mihangaiko ya siku hadi siku katika ujenzi wa Taifa. Vipi mapumziko huko kwenu? Pembejeo zimeshafika kwa ajili ya matayarisho ya kilimo?

Nimetayarisha waraka huu, ili nikupe Mrejeo wa hatima ya yule kijana dereva taxi mleyemlea kwenye kampuni yenu ya pwagu and pwaguzi and company & sons.

Nafikiri unamkumbuka yaah nafikiri unamfahamu kwa sababu , yeye ndio dereva wa hili bus pekee jipya la yutong hapa mkoani kwetu. Nafikiri unakumbuka kipindi kile yeye dreva taxi nyinyi mlikua madereva wa Dallas dala.

Nafikiri unakumbuka kila mlipo shusha abiria vituoni mlimtumia yeye kuwafikisha abiria nyumbani, kwa kua mlimuamini na kumpa sifa kede kwa abiria wenu.

Kwa kawaida madereva wa dala dala wanafahmika kwa kuchomekea na kutanua barabarani, kusema ukweli mpaka leo sifahamu mlipokua mkilalamikiwa kwa rafu barabarani, mlikua mnamalizana vipi na maafande. Anyway, ngoja niendelee.

Yule kijana aliendelea vizuri na kujizolea umaarufu na uaminifu mkubwa, ingawaje mimi binafsi siamini mtu kuwa mtimilifu aslimia 100%. Ila kijana alikaza buti chini ya uangalizi wa kampuni yenu.

Sasa ndugu zangu, kuna siku nilimuuma sikio kidogo aniambie kwa nini hataki kujipandisha daraja angalau aendeshe daladala lenye abiria wengi ili ajulikane zaidi.

Nakumbuka alinijia juu na kuniambia hajazoea rafu barabarani , pia aligoma kulipia bia alizoniagizia kwa maana simtakii mema.

Wakati pwagu unaanza mapumziko kwenye kampuni yenu, na Pwaguzi akiwa bado anaendelea hamkuacha kumsifu kijana kwa utendaji wake.

Ndugu zangu, nafikiri mnakumbuka kile kipindi cha kupumzika dereva wetu ili achukuliwe dereva mpya wa basi kubwa kilivyokuwa, Nafikiri mnakumbuka mchakato wa kumpata dereva mpya nyinyi ndugu zangu wa pwagu and pwaguzi and company &sons, mlivyonusurika kutoana roho kwa ajili ya nafasi ya uderva.

Hatimae wakurugenzi watendaji walipoamua kumpendekeza yule kijana dereva taxi apewe basi ili kuisalimisha kampuni.

Nafikiri mnakumbuka jinsi mlivyomnadi dreva taxi kwenye interview zote alizopita ,
Kuanzia ninyi ndugu zangu, washika dau ndani ya kampuni, mpaka sons..
Hakuna dosari mliyoiweka juu yake

Mpaka waendesha interview wakaridhika pasipo shaka na kumkabidhi basi jipya yutong. Kama mjuavyo enyi ndugu zangu, kawaida dereva akikabihiwa basi kujichagulia kondakta na mtunza mizigo na usalama kwa abiria.

Kinachonisikitisha na nikaamua kuandika waraka huu, ni iweje sasa hivi muonyeshe kasoro zake...,? Ninavyosikia abiria wanamwamini wanasema ni mzoefu kuliko enzi zake kwenye taxi.

Wanasema hapendi vikwazo barabarani, akikikuta hushuka kukipiga teke na kuendelea na safari, eti kwenye kona analala na zote huku abiria wakishangilia, wanasema wanamuamini.

Je, mlishaonana na askari traki, au vyombo vinavyosimamia usafiri wa nchi kavu na majini ( sumatra)

Mwisho mkiona kuna ugumu jaribuni kuonana na R.T.O
Wasalaaam,
Mjomba
21.07.2019
 
Tatizo ni kwamba sheria za barabara ndizo zinamuongoza dereva lakini nyie mnamtaka avunje sheria hizo...
 
Mwanzo sikuwa namuelewa dereva, ila sasa nimenuelewa, hataki basi limilikiwe kiukoo.
 
Hebu piga/weka santuli ya "mwana meka...."

Hasa kile kipande
"ameshaonja asali...",
"ameshaumwa na nyoka akiona unyasi......."
 
Back
Top Bottom