Waraka kwa mwenyekiti CHADEMA: Sio wapiganaji wote wana hekima!

Ni kweli Mkuu lakini adui akiku-provoke na wewe badala ya kutulia ukaingia kichwa kichwa kwa hasira, badala ya kujenga, unakuwa unajimaliza wewe mwenyewe. Nasary angeweza kutumia maneno mengine kupangua kauli na maneno hayo ya UVCCM na mengineyo au hata kuichana CCM lakini si kwa hoja alizotoa ukizingatia uelewa wa wananchi na jinsi adui anavyoweza kugeuza kibao. Kumbukeni CCM ni mabingwa wa kugeuza hoja kuonesha wengine ndio wenye makosa na sio wao!

sawa, na pia kama tulisikiliza vizuri, ile kauli ya dogo janja ilikuwa crashed pale pale. Mbowe alisema si kauli ya chama makini kama chadema, ile ilikuwa kauli ya hamasa ya kwake yeye kama Nassari.
 
Pia CDM mtambue hata kama upo kwenye mkutano wa mtaa maneno yenu yanapaa kwa kasi ya mwanga kitaifa, busara iwe kitu cha kwanza, jazba sio itikadi yetu!
 
Sishangai sana,sipendezwi wala sijachukizwa na maneno ya kijana wangu Mwenye uwezo mkubwa katika siasa kutoa tamko kama hilo,mawazo yake yanaendana kabisa na watu anaowaongoza,yeye si mbunge wa Tanzania bali Arumeru,Arusha na kanda nzima ya Kaskazini imedhihakiwa na kufanyiwa vitendo vya aibu tokea enzi za Nyerere hadi leo hii tumekua tukitengwa na kudharauliwa,TUWAAMBIE KABISA TUMESHACHOKA.........Joshua ni chaguo la wana Arusha na Arumeru kiujumla na yale anayoyanena yananenwa pia mitaani.
 
sawa, na pia kama tulisikiliza vizuri, ile kauli ya dogo janja ilikuwa crashed pale pale. Mbowe alisema si kauli ya chama makini kama chadema, ile ilikuwa kauli ya hamasa ya kwake yeye kama Nassari.

Sawa, lakini kwanini uharibu ili Bosi aweke mambo sawa? Mweneyekiti atahangaika na mambo mangapi? Suppose Mwenyekiti asingekuwepo? Ni mikutano mingapi akina Nasary wanafanya bila Mwenyekiti kuwepo na si ajabu kauli kama hizi ni za kawaida kwao? Nani huwa anazikanusha kama alivyofanya Mbowe jana?

Inawezekana wakati viongozi wakuu wakihangaika kukijenga chama kuna wengine huku chini, zaidi kwa kutojua, wanaharibu! Mwenyekiti yuko kwenye paa anapaua akiamini nyumba inaelekea kukamilika mara anashangaa inatitia - mchwa wamekula nguzo! Hebu penye ukweli tuambiane bila kuoneana haya bana!

Ndio yale yale ya Mtei bila kutambua upepo wa kisiasa uliopo anaongea ovyo. Nilishawahi kusema kwenye thread nyingine, mambo ya kuongea ovyo ni ya mashabiki kama sisi na sio wao viongozi. Kwa nafasi yake (Nasary) alitakiwa awe na busara ikiwezekana watu aina hii wapelekwe kozi ya namna ya ku-control jukwaa la kisiasa.
 
Pia CDM mtambue hata kama upo kwenye mkutano wa mtaa maneno yenu yanapaa kwa kasi ya mwanga kitaifa, busara iwe kitu cha kwanza, jazba sio itikadi yetu!

Kweli kabisa Mkuu! Jazba zimeimaliza CUF hivi hivi. Matusi, vitisho (Ngangari Vs Ngunguri), takbir, n.k. vimeifuta kabisa CUF. Na Chadema kama wanataka kuelekea huko huko waendeleze jazba za kijinga - nasisitiza jazba za kijinga.
 
Nassary acha hizo kaka yangu jua kwamba kauli 1 humghalimu kiongozi, kumbuka kauli ya jk kwa walimu ilimghalimu vp kwenye uchaguzi wa 2010, kumbuka kauli mbalimbali za kaka yako zitto kabwe juu ya chama chake zimemfanya mpaka leo watu wasimwamini kabsa ndani na nje ya chama chake even if kabwe atafanya jambo la maana lakin bado watu watamtilia mashaka,
na kwa kauli kama yako nassary utafanya vijana wenzio wenye umri kama wako wakose nafasi 2015 pia utafanya vijana tusiaminike ndani na nje ya jamii.
NASSARY FATA NYAYO ZA MBOWE ACHANA NA KUIGA MAMBO YA SLAA KWANI SLAA YY CCM WASHAMSINDWA.
 
Tunatambua ile kauli yake ilitokana na maudhi ya serikali kiziwi ya ccm. Wakati mwingine naweza kusema alikuwa sahihi kutia kauli yenye hamasa, kutokana na CCM kuwadharau watu wa kaskazini. Kama mnakumbuka kauli ya uvccm mkoa wa pwani waliposema Rais wa 2015 hatatoka kanda ya kaskazini. Cha ajabu ile kauli hakuna aliyeikanusha mpaka leo.

Acha kutetea maovu wewe kisa kasema Chadema mwenzako.
 
Sawa, lakini kwanini uharibu ili Bosi aweke mambo sawa? Mweneyekiti atahangaika na mambo mangapi? Suppose Mwenyekiti asingekuwepo? Ni mikutano mingapi akina Nasary wanafanya bila Mwenyekiti kuwepo na si ajabu kauli kama hizi ni za kawaida kwao? Nani huwa anazikanusha kama alivyofanya Mbowe jana?

Inawezekana wakati viongozi wakuu wakihangaika kukijenga chama kuna wengine huku chini, zaidi kwa kutojua, wanaharibu! Mwenyekiti yuko kwenye paa anapaua akiamini nyumba inaelekea kukamilika mara anashangaa inatitia - mchwa wamekula nguzo! Hebu penye ukweli tuambiane bila kuoneana haya bana!

Ndio yale yale ya Mtei bila kutambua upepo wa kisiasa uliopo anaongea ovyo. Nilishawahi kusema kwenye thread nyingine, mambo ya kuongea ovyo ni ya mashabiki kama sisi na sio wao viongozi. Kwa nafasi yake (Nasary) alitakiwa awe na busara ikiwezekana watu aina hii wapelekwe kozi ya namna ya ku-control jukwaa la kisiasa.

naungana na wewe 100%. Ila ninachoamini ni kwamba vijana kama akina Nassary pamoja na mimi tumejifunza kitu, naamini ametambua. Hata hivyo naamini haitapungaza hii kasi ya mabadiliko. Mwenyekiti ana kazi nyingi, na kuhakikisha makamanda wanakuwa kwenye chain ni moja ya responsibilities zake.
 
Tunatambua ile kauli yake ilitokana na maudhi ya serikali kiziwi ya ccm. Wakati mwingine naweza kusema alikuwa sahihi kutia kauli yenye hamasa, kutokana na CCM kuwadharau watu wa kaskazini. Kama mnakumbuka kauli ya uvccm mkoa wa pwani waliposema Rais wa 2015 hatatoka kanda ya kaskazini. Cha ajabu ile kauli hakuna aliyeikanusha mpaka leo.
Mkuu, kosa moja halihalalishi kosa jingine!
 
Nasari unauwezo gani wa kuigawa nchi wewe?

Una jeshi la kukulinda kwa kauli mbaya kama hii?

Mie sikufaham na ujue wewe ni case study kwa vijana, sasa kwa maneno hayo chalii yangu umetupa wakati mgumu vijana wenzio hatutaminika ktk majimbo. Wataogopa kutupa dhamana kuwa tutakuwa na hulka na uropokaji kama wewe chalii!
CDM inahitaji watu wenye upeo wa kutafakari sana. hujaona mbele Nassari! So jikague kama uliteleza jipange kufuta kauli na kama hukuteleza niko hai nasubiri siku utakapoitenganisha Kaskazn na Tanzania.
 
Muheshimiwa mwenyekiti kamanda wetu Freeman mbowe,
Najua unapita humu ndani na wapambe wako wengi tuko nao
Mimi ni mwanachama wako mtiifu na tuko pamoja kuikomboa nchi hii kutoka kwa hawa mapaka pori yanayotuibia hadi vifaranga vyetu yaani Chama Cha Magamba.
Nimekuandikia waraka huu baada ya kuona kazi kubwa unayoifanya ya kunyoosha maneno. Ajali ya leo ya Nasary kusema Kaskazini itajitenga kama CCM wakiendelea na ubishi ni ajali mbaya sana kisiasa na nina hakika CCM wamepata pa kuanzia. Lakini nakumbuka hii si mara ya kwanza. Mikutano yote niliyohudhuria hapa Chadema Square Arusha mara nyingi umekuwa ukisimama na kukemea maneno makali na ya mzaha yanayoletwa na wapambanaji wako. Ukweli ni kwamba huwa unajipambanua kama Baba sana. Busara zako huwa zinasaidia sana. Lakini matatizo haya hayakomi. Kwanini?
1. Si kweli kwamba kila mkutano wa CDM lazima wote walioko meza kuu waongee. Ninyi mnajuana kiwango cha hekima na ingekuwa busara wale wenye hekima tu ndio wakapewa nafasi. Mfano leo Diwani aliyetoka CCM - Mawazo ameonyesha kabisa kwamba bado ana hulka za kilusinde za CCM. watu wengi hatukupendezwa na maneno yake. Hata Ole millya hakuvutia umati wa watu bado busara ni ndogo sana.
2.Kuna watu wanaweza kuwa na busara ya kutenda lakini sio busara ya kuongea mbele za watu. Mimi naamanini utendaji na uwezo wa kuongea mbele ya hadhara ni vitu viwili tofauti.
3. Kuna watu wanafaa kwa propaganda za wakati na mahali fulani tu mfano Nasary na Lema. Wao ni wazuri sana nyakati za uchaguzi.
Kwa maelezo haya mafupi mwenyekiti ningeomba
A. CCM wanachuo chao cha Magogoni cha siasa - CDM pia tunapaswa kuwa na mahali tunapowapikia watu wetu ili wawe wanasiasa bora zaidi.
B. Kuwe na semina nyingi za ndani ili kuwekana sawa na kukumbushana namna ya kuwasilisha hoja bila mafarakano ya maneno ambayo unapaswa kukemea kila mara.
C. Uongozane na watu wenye uwezo wa kuwasilisha hoja kwa nguvu lakini kwa taratibu bila jazba na busara ikitawala mfano John Mnyika na Hallima Mdee ili vijana wanaoinukia wapate mfano (role models) wa kujenga hoja.
AHSANTE KWA KUNISIKILIZA

Naungana nawe mkuu
 
Nasari unauwezo gani wa kuigawa nchi wewe?

Una jeshi la kukulinda kwa kauli mbaya kama hii?

Mie sikufaham na ujue wewe ni case study kwa vijana, sasa kwa maneno hayo chalii yangu umetupa wakati mgumu vijana wenzio hatutaminika ktk majimbo. Wataogopa kutupa dhamana kuwa tutakuwa na hulka na uropokaji kama wewe chalii!
CDM inahitaji watu wenye upeo wa kutafakari sana. hujaona mbele Nassari! So jikague kama uliteleza jipange kufuta kauli na kama hukuteleza niko hai nasubiri siku utakapoitenganisha Kaskazn na Tanzania.

Mkuu najua umekereka sana, nami pia. Naamini kijana aliteleza. Hata hivyo kama ni wa kusikia atakuwa amesikia, kwanza kutoka kwa Kamanda Mbowe alipomsahihisha kiakili na hata na mchango wa JF.
 
Hata mimi nilikuwepo pale na nilishikwa na butwaa Nassari alipo tamka yale maneno. Naomba Nassar jirekebishe bado tunakuamini na tunakupenda
 
. Lakini matatizo haya hayakomi. Kwanini?
1. Si kweli kwamba kila mkutano wa CDM lazima wote walioko meza kuu waongee. Ninyi mnajuana kiwango cha hekima na ingekuwa busara wale wenye hekima tu ndio wakapewa nafasi. Mfano leo Diwani aliyetoka CCM - Mawazo ameonyesha kabisa kwamba bado ana hulka za kilusinde za CCM. watu wengi hatukupendezwa na maneno yake. Hata Ole millya hakuvutia umati wa watu bado busara ni ndogo sana.
2.Kuna watu wanaweza kuwa na busara ya kutenda lakini sio busara ya kuongea mbele za watu. Mimi naamanini utendaji na uwezo wa kuongea mbele ya hadhara ni vitu viwili tofauti.
3. Kuna watu wanafaa kwa propaganda za wakati na mahali fulani tu mfano Nasary na Lema. Wao ni wazuri sana nyakati za uchaguzi.
Kwa maelezo haya mafupi mwenyekiti ningeomba
A. CCM wanachuo chao cha Magogoni cha siasa - CDM pia tunapaswa kuwa na mahali tunapowapikia watu wetu ili wawe wanasiasa bora zaidi.
B. Kuwe na semina nyingi za ndani ili kuwekana sawa na kukumbushana namna ya kuwasilisha hoja bila mafarakano ya maneno ambayo unapaswa kukemea kila mara.
C. Uongozane na watu wenye uwezo wa kuwasilisha hoja kwa nguvu lakini kwa taratibu bila jazba na busara ikitawala mfano John Mnyika na Hallima Mdee ili vijana wanaoinukia wapate mfano (role models) wa kujenga hoja.
AHSANTE KWA KUNISIKILIZA[/QUOTE]

Joshua Nassari kumbuka ulikotoka jifunze athari za kauli
 
kuna watu wanasema wamekasirika sana kwa kauli ya nasary kana kwamba ni kawaida ya nasary kusema vile..kama unaguswa na harakati za ukombozi wa nasary ni busara ukamshauri kwa upole..ni kijana mwelewa sana.. inawezekana kabisa kateleza neno moja au mawili katika 50 aliyoongea..ieleweke ni binadam na si malaika, cha kufanya ni kumueleza ili kumuimarisha na sio kumkejeli na kumvunja moyo kama maoni ya baadhi yetu hapa.. hizi harakati zinaendelea kwa waliokuwepo jana pale walielewa hasa mbowe alivyoelekeza kuhusu kauli ile na nasary alielewa hata yule diwani..pia semina za mara kwa mara ni muhim kwa viongozi cdm maana kila mtu ana uwezo na busara tofauti na mwingine..
 
Naungana na mpingauonevu 100% mara kadhaa Nasari amekuwa akiongea bila mpangilio, na ajue wengi tumeiondoa ccm Meru si kwa ubora wa Nasari bali kwa kuichukia ccm. Nasari amekuwa akiongea masuala yanayotakiwa yasemwe na Mbowe au Slaa, mfano wa jana kusema atamyima Kikwete asije Meru. Wengi tunategemea Nasari atupatie majibu ya ardhi asituletee uhuni.

Ni kweli kabisa mkuu nadhani atakuwa amejifunza kutokana na makosa yake mwenyewe na sidhani kama hatokuwa msikivu na kuachana na kauli ambazo hatutegemei kutoka mdomoni kwa mpambanaji!
 
Bahati nzuri waliyo nayo CDM ni ukweli kuwa CCM hawana mahali pa kusemea kwa sasa. Wamebanwa mno na wananuka shombo kali kiasi hata wakiitisha maandamano na mikutano ya hadhra ili kumjibu Nassary, hakuna atakayekuja, na wataokuja kwa bahati mbaya, hakuna atayewaamini wasemayo. Things are terribly falling apart in the CCM camp. Hii haina maana kuwa CDM waendelee kuropoka! Wajihadhari tu lakini pia wajue kwa sasa CCM kama ni joka, uhai umebaki kichwani na ndicho chenye sumu. Kiwiliwili kimepigika haswa na wana harakati.
 
Back
Top Bottom