Waraka kwa mwenyekiti CHADEMA: Sio wapiganaji wote wana hekima! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka kwa mwenyekiti CHADEMA: Sio wapiganaji wote wana hekima!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpingauonevu, May 6, 2012.

 1. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Muheshimiwa mwenyekiti kamanda wetu Freeman mbowe,
  Najua unapita humu ndani na wapambe wako wengi tuko nao
  Mimi ni mwanachama wako mtiifu na tuko pamoja kuikomboa nchi hii kutoka kwa hawa mapaka pori yanayotuibia hadi vifaranga vyetu yaani Chama Cha Magamba.
  Nimekuandikia waraka huu baada ya kuona kazi kubwa unayoifanya ya kunyoosha maneno. Ajali ya leo ya Nasary kusema Kaskazini itajitenga kama CCM wakiendelea na ubishi ni ajali mbaya sana kisiasa na nina hakika CCM wamepata pa kuanzia. Lakini nakumbuka hii si mara ya kwanza. Mikutano yote niliyohudhuria hapa Chadema Square Arusha mara nyingi umekuwa ukisimama na kukemea maneno makali na ya mzaha yanayoletwa na wapambanaji wako. Ukweli ni kwamba huwa unajipambanua kama Baba sana. Busara zako huwa zinasaidia sana. Lakini matatizo haya hayakomi. Kwanini?
  1. Si kweli kwamba kila mkutano wa CDM lazima wote walioko meza kuu waongee. Ninyi mnajuana kiwango cha hekima na ingekuwa busara wale wenye hekima tu ndio wakapewa nafasi. Mfano leo Diwani aliyetoka CCM - Mawazo ameonyesha kabisa kwamba bado ana hulka za kilusinde za CCM. watu wengi hatukupendezwa na maneno yake. Hata Ole millya hakuvutia umati wa watu bado busara ni ndogo sana.
  2.Kuna watu wanaweza kuwa na busara ya kutenda lakini sio busara ya kuongea mbele za watu. Mimi naamanini utendaji na uwezo wa kuongea mbele ya hadhara ni vitu viwili tofauti.
  3. Kuna watu wanafaa kwa propaganda za wakati na mahali fulani tu mfano Nasary na Lema. Wao ni wazuri sana nyakati za uchaguzi.
  Kwa maelezo haya mafupi mwenyekiti ningeomba
  A. CCM wanachuo chao cha Magogoni cha siasa - CDM pia tunapaswa kuwa na mahali tunapowapikia watu wetu ili wawe wanasiasa bora zaidi.
  B. Kuwe na semina nyingi za ndani ili kuwekana sawa na kukumbushana namna ya kuwasilisha hoja bila mafarakano ya maneno ambayo unapaswa kukemea kila mara.
  C. Uongozane na watu wenye uwezo wa kuwasilisha hoja kwa nguvu lakini kwa taratibu bila jazba na busara ikitawala mfano John Mnyika na Hallima Mdee ili vijana wanaoinukia wapate mfano (role models) wa kujenga hoja.
  AHSANTE KWA KUNISIKILIZA
   
 2. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapo kweye rangi sidhani kama bado kuna kitu kinaitwa chuo cha siasa
   
 3. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Ahsante mkuu. Sina hakika kama bado kipo ama kimebadilishwa matumizi but content yangu ni kuwa na kitu kinachoweka team nzima ya chadema katika muono mmoja. Thanks for correcting me.
   
 4. Makete Kwetu

  Makete Kwetu JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  well said
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  :argue:
   
 6. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,923
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Naungana na mpingauonevu 100% mara kadhaa Nasari amekuwa akiongea bila mpangilio, na ajue wengi tumeiondoa ccm Meru si kwa ubora wa Nasari bali kwa kuichukia ccm. Nasari amekuwa akiongea masuala yanayotakiwa yasemwe na Mbowe au Slaa, mfano wa jana kusema atamyima Kikwete asije Meru. Wengi tunategemea Nasari atupatie majibu ya ardhi asituletee uhuni.
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu wanaita responsibility. Mbowe kama mwenyekiti wa CDM ni mtu responsible sana. Kwa kweli watu kama kina Mbowe ndiyo wanaifanya CDM iendelee kupata imani ya watu makini. Frankly speaking three years ago nilikuwa ninashabikia tu lakini moyoni nilikuwa nasema bado sana wapinzania kuweza kubeba dhamana ya kuongoza serikali.

  Lakini leo hii ninaweza sema kabisa kuwa upinzani Tanzania umeiva katika kuongoza na wasiwasi wangu kuhusu nchi kuteteleka imetoweka kabisa. Tena ninaona kwa sasa hivi CDM inaonekana ina busara zaidi za kiuongozi kuliko CCM. Kauli za makamanda ambao bado wapo learning curve ya siasa si za kutilia shaka sana kwani watu hujifunza kutokana na makosa. Ninaamini kabisa kuwa CDM itatoa mafunzo elekezi kwa wasemaji wao wa majukaani.
   
 8. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nassary kwa kuwa unapita humu Om ba msamaha kama hujui cha kuongea kabla hujapanda jukwaani au kuongea kwenye umati Omba busara kwa wenzio,Matamko yako ni kitanzi chako,sie wote wapiganaji ila hatujapata tu bahati ya kukamata jukwaa kama wewe,unachuja haraka sana kwa muda mfupi sana ukiwa na umri mdogo sana,skuwepo mkutanoni nipo Tanga ila nilipigiwa simu na makamanda wengine waliokuwa Mkutanoni kwa kweli umekiangusha sana Chama,uliza Chales Mwera yuko wapi,CDM ni makini sana usishangae 2015 akasimamishwa mtu mwingine hapo Meru.
  Ita waandishi Omba msamaha yapite ukikaa kimya imekula kwako.
   
 9. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Siasa ni mchezo mgumu, ukinukuu kila kitamkwacho yaweza kukusumbua, wamachinga mbeya wanamwita Joseph Mbilinyi a.k.a sugu kuwa ni rais wa mbeya! Je, ndivyo ilivyo?? Ccm imetamka mengi sana mabaya kwa wapinzani, waache watu wapumue juu yao, watu wa hovyo sana hao. Ila cdm isipite viwango, rais Jk ni rais wa Tz na Arumeru mashariki pia! Dogo janja, acha upuuzi wa kitoto.
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mmmmhhhhh........ Nimekumbuka nassary kazaliwa mwaka 1985 lazima awe chini ya uangalizi wa mtu Kama mboye au hata Mnyika bado ni kinda
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Nassari kwa niaba ya sociologist wote, wenye kuamini umoja ni nguvu utengano ni dhaifu, omba radhi kwa wananchi na wapenzi wako wote walioko tanzania nzima. kumbuka, ushindi wako si juhudi zako, bali ni juhudi za wadau na wanaharakati tanzania nzima. michango iliyotolewa, haikuitoka arusha pekee, ilitoka tanzania nzima hadi zanzibar walikuchangia. hivyo tanguliza busara zaidi kuliko jazba. Karl Marx, Spencer, A. Gidens, A. Frank, Durkeim, Weber Max, Hobert, na scholars wengine, hawajakufundisha uliyoyatamka.

  Pili ni kwa Dr. Slaa. Maneno yako uliyoongea Mwanza, yanawaweka askari hadi wapenzi wa CHADEMA wanapopita mitaani, baadhi ya vijana, tena wengi walevi wanatishia, tutavamia kituo, na tutaanza na nyie.

  Sakata la ILEMELA, wanafahamika waliolisimamia, kwa nini hao wasishughulikiwe na badala yake kutangaza kuvamia kituo cha polisi ambacho kwa wakati mwingine unakitaka kikusaidie mambo yako?

  hapa slaaa naye aliteleza kama nasari
   
 12. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena vema,tushukuru kuwa viongozi wa chadema wanaweza kukemea kauli mbovu za makada wao,magamba hawawezi Lucinde aliropoka ndo kwanza wakashangilia,Tumsamehe Nasari,bado kijana,taratibu atakua,chadema wamlee vizuri,naamini hatayeye kama ametafakari vizuri amegundua kuwa amejaribu kuvuka tope kwa kandambili!
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  May 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nasikia CDM wana mpango wa kujenga kitu kama hicho kwa msaada wa Mzee Sabodo labda itasaidia kama ulivyosema. Mkuu umenena vyema. Kuongea mbele za watu ni talanta na si kila mtu ana talanta hiyo. Umemshauri vyema sana Mwenyekiti.
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  May 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nadhani ataomba msamaha. Nakumbuka Regia (RIP) aliwahi kufanya kosa lakini baadaye akaomba msamaha bungeni kama sikosei. Huyu kijana naye aombe msamaha na atamke wazi kwamba hayo yalikuwa ni maneno yake na kwa jinsi yoyote ile hayana uhusiano na msimamo wa chama chake.
   
 15. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Busara yake itapimwa kupitia maonyo na maelekezo mabali mbali anayopewa na Makamanda humu JF
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  May 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Tunatambua ile kauli yake ilitokana na maudhi ya serikali kiziwi ya ccm. Wakati mwingine naweza kusema alikuwa sahihi kutia kauli yenye hamasa, kutokana na CCM kuwadharau watu wa kaskazini. Kama mnakumbuka kauli ya uvccm mkoa wa pwani waliposema Rais wa 2015 hatatoka kanda ya kaskazini. Cha ajabu ile kauli hakuna aliyeikanusha mpaka leo.
   
 17. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu sina la kuongezea! BUSARA, BUSARA, BUSARA, ...., jamani BUSARA! Ni turufu muhimu sana ya kisiasa. Unaweza kuwa safi kila idara lakini neno moja tu la "mropokaji" mmoja ndani ya Chama likaharibu move nzima. Hata kama ni suala la "damu kuchemka" mnatakiwa kuwa makini na maneno na matendo yetu muwapo kwenye majukwaa ya kisiasa.

  Maneno au hulka zozote, hata kama si za kweli au ilikuwa hamasa tu, lakini zinazoweza kutafsiriwa kipotofu na adui au makuwadi wao na "kuwalisha" wananchi yapasa ziepukwe au zizungumzwe kwa tahadhari kubwa na mzungumzaji aelewe anachokizungumza na athari zake ni zipi na sio kuropoka ili tu kufurahisha hadhara kwa wakati huo enyi watu!

  CHADEMA eleweni uelewa wa watanzania ni mdogo na uelewa huu mdogo hutumiwa sana na adui kama silaha na turufu muhimu sana kisiasa! Ukimwacha Mwenyekiti, Mh. Mbowe, mbona wengine hamuelewi hilo? Hebu jifunzeni kwa Mwenyekiti wenu!

  By the way, hivi kile chuo cha uongozi kimefikia wapi? Ni muhimu sana vijana na makada wenu wakapata kozi fupi za namna ya kuongea majukwaani au angalau semina elekezi. Majukwaa ya kisiasa ni tofauti na majukwaa kama "Revolution Square" pale UDSM na vyuo vingine! Daima kwenye siasa adui hutafuta penye UDHAIFU na usitegemee ataeleza mema au uzuri wako hata mara moja. Eleweni hili na badilikeni.
   
 18. M

  MC JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mkuu Mpingauonevu,

  Nimelipenda bandiko lako, ni kweli kabisa kuna watu wanatakiwa kuwekwa chini na kuelezwa nini cha kusema na wapi waseme nini!! nini niko Dar na nilisikiliza hotuba zile kupitia web link.

  Mheshimiwa Mbunge Nassari alinikwaza sana kwa maneno yake, imani huja kwa kusikia na kuna matamshi mengine si mazuri kwenye mkusanyiko kama ule ukizingatia watanzania wengi walikuwa wanafuatilia, hatuna sababu ya kuwanufaisha magamba kwa mambo yanayoepukika, wao (magamba) ni mabingwa wa kuzusha mambo kuwarubuni watanzania.
   
 19. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Mkuu lakini adui akiku-provoke na wewe badala ya kutulia ukaingia kichwa kichwa kwa hasira, badala ya kujenga, unakuwa unajimaliza wewe mwenyewe. Nasary angeweza kutumia maneno mengine kupangua kauli na maneno hayo ya UVCCM na mengineyo au hata kuichana CCM lakini si kwa hoja alizotoa ukizingatia uelewa wa wananchi na jinsi adui anavyoweza kugeuza kibao. Kumbukeni CCM ni mabingwa wa kugeuza hoja kuonesha wengine ndio wenye makosa na sio wao!
   
 20. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Makamanda wa CDM wanapopanda jukwaani watangulize busara, haya maneno ya vijiweni wayaache vijiweni. Tunashukuru Mbowe kwa busara zako na kuliweka sawa kabla hujaendelea na hoja nyingine jana
   
Loading...