Waraka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA; fanyeni haya...!

Binafsi naona kuna mambo mazuri,lakini tatizo la mtoa hoja pia ana chuki binafsi na dr slaa. Pia neno zitto limetamkwa sana,hii imepunguza maana ya huu ushauri na kuonekana kama ushabiki na majungu!

mia mia ujumbe wake nimeshndwa kuelewa ameanza vizur mwishon chuki binafsi hoja yake imekuwa hovyo kwa sentens za mwisho
 
Great mkuu, ni jambo jema sana kuwa na watu ambao angalau wanachukua hoja za adui na kuzitumia kuboreshea kwao. Maana kuna watu humu kazi yao ni kuponda chochote kinachotoka CCM. Sometimes hawa CCM wanaweza kutoa hoja za maudhi lakini zenye kuwa-alert ili mchukue tahadhari. Binafsi napenda sana kusoma ujumbe wa magamba ili kujua na wenyewe wana mitizamo gani dhidi ya CHADEMA.

Hizo sio hoja. Hizo ni propaganda. Hii ni mara ya pili nakuona unaingia kichwa kichwa na hoja za kipuuzi. nnapata wasiwasi.
 
Haya uwanja ni wenu wanazi wa ccm. nilitegemea ni ushauri wenye maana kumbe ni akili zizile za ccm kama mtu kapurukushwa usingizini. unaposema ccm wanashighulikiamapungufu yao hivo kutaka cdm wawaige ccm wakati ni ukweli ulio dhahiri kuwa ccm wameshindwa kuhimili mikiki ya dr. slaa na m4c una maana gani kama c propaganda.
narudia tena uwanja ni wenu manake mnaandika na kujibiana ionekane eti hii nayo ni hoja. yaani mnafanya maigizo kwenye jukwaa la great thinkers? stupids. wenye bongo zetu ngoja tutafute hoja za wenye akili.
 
@Tandale Kwa bi Nyau!
Yaani wewe kwa haraka haraka una Elimu ya UPE, Pili umezeeka,huna uwezo wa kujenga hoja bali unasikia stori za maghamba wakiongea unazi-copy afu unashindwa ku-paste,uwezo wako wa kufafanua mambo ni mdogo,Ndo maana unadiliki kutaja mambo ya machache yaliyofanywa na CCM bila kufikiria the duration of Time Elapsed!
 
Tandale mwenyewe ni ghamba
 
ujinga uliopitiliza huitwa UMBUMBUMBU....!
 
Upuuzi mtupu!

Kawaulize waliokutuma; kama ya CDM hayafai mbona mnaya-copy na kuya-paste?

kukopi na kupesti unakujuwa weye au unajiandikia tu?

Hoja za mkaguzi mkuu wa serikali aliyepewa meno na Kikwete, kushikiwa bango na chadema, huko ndiko ku kopi na kupesti, tena kopi uchwara.
 
Nalazimika kuandika kwa Uhai wa Taifa hili, nimeyakumbuka maneno ya Muasisi wa taifa hili aliyepata kusema kuwa bila kwa kuwa "Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba" na kwa hali ya sasa ya kisiasa ndani ya Taifa hili linaloundwa na nchi mbili ya Bara na Visiwani, ni vema kauli hiyo pia ikipewa tafsiri nyingine kwa maana "bila upinzani makini na wenye nguvu CCM itakuwa si madhubuti na hivyo nchi yetu itayumba" hii inamaanisha kazi ya kuistua CCM na kuikumbusha majukumu yake hufanywa vyema na wapinzani, na hivyo kuifanya ibaki madhubuti.

Leo nitaandika waraka huu kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA nimtajie baadhi ya Tofauti za msingi baina ya Chadema na CCM.,na nini CHADEMA wafanye kama wapinzani ili kuleta Upinzania Makini hapa nchini, nitaanza kuzitaja tofauti hizo na kisha kuifafanua moja baada ya nyingine;

(i) NAMNA YA KUSHUGHULIKIA CHAGAMOTO NDANI YA CHAMA;

CCM wanapovumbua ukweli ambao unawatafuna kama tatizo la mafisadi, rushwa kwenye chaguzi zao, upendeleo n.k mara moja hutafuta suluhisho la matatizo yao na hivyo huwaponya na kuwaondoa katika misukosuko waliyokuwa nayo.

Walipata matatizo makubwa kwenye uchaguzi 2010 kutokana na kuboronga kwa Makamba na Sekretarieti yake, mara moja wakavunja sekretarieti ile na kuunda nyingine chini ya Mukama.,na baada ya mwaka mmoja wa utendaji na kuonekana kuwa CDM inapata nguvu kwa ulegelege wa sekretarieti hiyo Mwenyekiti akapitishia azimio la kuunda sekretarieti mpya chini ya Mzee Kinana kada wa muda mrefu wa chama cha mapinduzi na mwanasiasa nguli mwenye kufahamu chama na wanachama.,pembeni yake Mangula.,asiyeongea bali hutenda.,asha-rose migiro Mama mwenye jina kimataifa akakabidhiwa kazi ya kufanya lobbying and she is pretty lobbyist unategemea taswira ya CCM itakuwaje chini yake.,pembeni mama Zakhia mchumi mzoefu aliyeeendesha na kusimamia uchaguzi wa CCM 2010, uchaguzi ambao ulitumia kiasi kikubwa cha pesa lakini hakuyumba kuzitafuta na kuzipangia matumizi.

Haya yanafanyika ili kuinua hadhi na kuongeza kasi ya chama ili kiimarike zaidi na kuendelee kushika dola.,haya hayakufanywa ila baada ya CCM kukiri na kuyakubali mapungufu yao kama taasisi ya siasa na kufanya SWOT analysis ya kina hivyo kubaini udhaifu wao na kuutafutia dawa hii.,na hivi sasa kila mwanaCCM na hata asiye mwanaccm bali mtanzania mwenye fikra za sawa sawa anakiri kuwa safu hii ni ukuta wa chuma. Tofauti na CDM.

CDM watakufa kifo cha kimya kimya kwa uzito wa kufikiri na kujifanyia tathmini.,kwa maana wanapobainishiwa tatizo wao hawajadili juu ya kuondokana na tatizo hilo na badala yake hubaki wakijipa moyo na kukithiri kwenye propaganda.,walikuja na mtaji wa kutaja mafisadi hoja ambayo kwa sasa haina mashiko wala nguvu miongoni mwa critical thinker kwa kuwa wanataja na kisha hawathibitishi wala hawaendi mbele kuyasimamia madai yao lakini pia wanakosoa kwa Unafsi zaidi kwa maana wanapinga kila kitu ambacho serikali ya Chama Cha Mapinduzi wamekuja nacho, maendeleo yote wakadai hakuna kilichofanyika, na watu wanaona shule, hospitali mabarabara, treni za mjini na majengo ya fahari makubwa yakijengwa na serikali.,wanaona kufufuliwa shirika la nyumba na mengineyo.,watu wa tanzania sio mazezeta wanaona haya na watahukumu kwa haya.

matokeo ni kuwa CDM inaendelea kujisahaulisha mapungufu yake na kujitoa ufahamu wa kasoro zake.,haya ya kupanga safu za wachaga vyuoni ni gumzo lililopo sasa hivi huku katika vyuo vya elimu ya juu na watu wanaambiwa haya ili wajirekebishe na kujipanga upya kuelekea 2015.,wao wanakanusha na kujitoa ufahamu. watakuja kuona impact ya jambo hili baada ya 2015 pale watakapolalama kuwa wameibiwa kura na kuendelea kudai kuwa kuna kontena za kura zimeingizwa nchini kama alivyodai 2010. Ni ujinga na kujipunguza ufahamu kuyafanya haya. JIPANGENI.

Ondoeni tatizo la ukabila ndani ya chama Chenu, wahakikishieni wananchi kuwa chama chenu kina sura ya utaifa kwa kubadili muonekano wa sasa na taswira ya ukabila iliyotawala chama chenu sasa, haya yatawasaidia. Nendeni mtwara waambieni wamakonde kuwa hata BABA KUNDAMBANDA nae ana nafasi katika chama chenu.,wapo wamakonde wachache vyuoni groom them ama mmoja wao kisha mtumieni as icon kuwa anawa-represent watu wa kusini.,tafuta mpemba mmoja mpeni Uenyekiti wa tawi la chuo kikuu kimoja kisha fanyeni propaganda ya kutosha kuwa hata wapemba nao wamo chadema.

Waambieni makasisi na mapadri waache kuwaongelea hoja zenu.,waache kujihusisha na CHADEMA na pia nendeni kwa masheikh waambieni mko nao pamoja, pelekeni michango ya ziara zao na maulid yao kama wafanyavyo CCM, msifanye harambee makanisani pekee nendeni madrasa pia wafanyieni harambee wapo waislamu katika CDM kama zito mtumieni akayafanye haya na muache kumpiga vita na kumzushia mambo ya uongo kwa kudhihirisha chuki yenu kwake acheni kuyafanya hayo na waislamu watawapokea na kuwakubali kwa dhati ya mioyo yao., hiyo ndio SIASA.

Msitumie maandamano na kusababisha watu kufa bila sababu za msingi kwa woga wa kifo watu watashindwa kuwaunga mkono bali nendeni kwenye vijiwe vyao kaeni nao chini fanyeni strategic movement zenye malengo, zitawaimarisha kimya kimya bila kufa mtu bila damu kumwagika, yafanyeni hayo. January Makamba amekutana na wanabumbuli na kuwaalika wapigadebe na wauza kahawa pamoja na makuli wa k.koo kwa nembo ya wasambaa wanabumbuli lakini hili liliungwa mkono na makuli wote wa K.koo na wakamuona January kuwa ni mtu bora kwao. Mpeni nguvu zito atengeneze LEKA DUTIGITE nyingine yenye taswira kubwa zaidi ya muziki.,afanye kitu chenye maendeleo kama kuwakusanya wanakigoma kwa ajili ya harambee za kujenga mabweni ya shule, hospitali na kadhalika, haya yatawasaidia kukijenga chama chenu.,wajerumani wanawapa pesa NYINGI pamoja na serikali na vyama vingine kama labour ya uengereza.,make effective disbursement kwa makundi yenye nguvu katika jamii, sio kwa kununua ndege na helikopta.,ama kwa kufadhili movement zisizo na tija kama M4C ambayo imeshindwa kuzaa matunda hata baada ya kutumia hazina kubwa ya pesa za chama na wahisani. Fanyeni haya.,

Mwambieni BABU slaa kuwa NAPE ameshamchakaza sasa amwache Mnyika aongee zaidi na apambane na kijana mwenzake, wapiga kura wa leo wanataka sura inayofanana na wao, Mnyika ni mwenezi wa CHADEMA lakini kwanini BABU anapenda kuuza sura zaidi kwenye medias yeye kuliko mnyika, hata kama anapenda ujana kwa kuchelewa kuoa na kuzuga na uchumba wa miaka kibao bado hilo halimrudishii yeye sifa ya ujana. Eligible voters wa sasa ni vijana wapeni mtu atakaeongea nao katika lugha yao.

Mwambieni John Heche kuwa ameshindwa kazi na anahitaji kupumzika, amesahau kuwa kazi yake ni kuwaunganisha vijana wa chadema na kuwajengea matumaini ya kuchukua nchi na kuleta mabadiliko ya kweli, bali asitumie platform ya BAVICHA kupanga safu ya utawala ndani ya CHADEMA kwa kuimarisha kundi fulani la wakubwa fulani ndani ya Chama hicho. Mwambieni kazi yake ni kuiunga CHADEMA sio kuimarisha makundi, asiyaige yale ya UVCCM ya Beno Malisa. Wekeni wazi kwa vijana wenu kuwa vijana wote wanathamani si wasomi pekee ama wanafunzi wa vyuo vikuu.,siasa ya vijana haipo vyuoni pekee ingawa ni sehemu muhimu pia, bali mtaani kuna wengi zaidi kuliko wale wa vyuoni. Mwambie Lema amfundishe HECHE namna ya kudeal na vijana wa mtaani, na mwambieni SUGU kuwa amesahau asili vijana wa mtaani hawamuelewi.,ameshindwa kuwatafutia vijana wa mbeya machinga wenye hali ngumu sehemu yenye kueleweka na yenye hati ya kisheria kufanya biashara zao, na anaendelea kuacha wanateseka kwa kupigwa na kuteswa na mgambo.,mwambieni anajisahau..,

Msimzibe mdomo Zitto mwambieni wakiridhia wanachadema atagombea urais kisha mtatumia vizuri na klushirikiana na nyinyi katika vita hii nzito bila kujigawa, msiendelee kumjengea uadui mkamfanya ajiimarishe yeye zaidi dhidi yenu, bali mwambieni kuwa afanye kazi ya chama wanachadema wakiridhia kwa kazi yake ndani ya Chama watampa ridhaa, then mnajua mtakachofanya kwenye utaratibu wa kura za maoni ya kuchagua Mgombea, ninyi bado mnayo nguvu kuliko yeye, hasa kwa safu mliyoipanga hivi sasa katika vyuo vikuu na BAVICHA.

Yawezekana kusikia hamsikii lakini hata haya MAANDISHI HAMYAONI..???[/QUOTE
Siku zote waliofilisika kiakili hukaa na kujadili mambo yasiyokuwa na maana kama UDINI,UKABILA NK ambazo kwa kiasi kikubwa muasisi wake ni viongozi wa CCM na ndio wamekutuma uandike upuuzi huu ulioandika hapa kama udini CCM ndio wanaongoza kwa udini viongozi wote wa juu ni dini gani?
Haikuwatosha sasa hivi mnarithishana Baba,Mama na watoto wote ni viongozi Shame on you unaepewa posho ili uandike pumba humu kwa kutegemea fadhila za kupewa ukuu wa Wilaya lakini tunataka hizo nafasi zigombewe kwa sifa sijui utapewa nafasi gani Ajabu ni kwamba hata muandike Watanzania hawadanganyiki kama mlivyozoea mnajifurahisha tu mshaeleweka kuwa nyie ni puppets wanaochumia tumbo tu
 
wakati wa waraka huu kufanyiwa kazi umefika kutokana na kile kinachoendelea kwa sasa ndani ya chadema..,"..baniani mbaya kiatu chake dawa.."
 
Natamani viongozi wa chadema wangelikubali kufuata ushauri huu, kwa kuwa haya yanayotokea yasingelijitokeza. Leo tunaona migogoro iliyokithiri ndani ya chama hiko na kusababisha hali ya sintofahamu kwa kiasi kikubwa baina ya viongozi wakuu na hata kwa wafuasi na mashabiki wa chama hicho.
 
the horse, mwendo wa chadema kuelekea kwenye mageuzi ya kweli ni mzuri sana, mtu yeyote wa ccm kuja kutoa ushauri hapa wakati chama chake mwenyewe kinaelemewa vibaya sana na chama hiki hiki anachokipa ushauri ni uhuni wa kupitiliza.

kuna mambo ya kufanya hapa na ambayo ni muhimu, chadema iendelee kujitambulisha na wanyonge, basi!
nguvu ya chadema iwe kwa watu wanyonge na iendelee kutenda haki kwa wengine.

Hayo mawili yataiinua chadema, na sio kuwalea watu kwa mujibu wa dini zao au makabila yao. Mpaka sasa ubunifu wa viongozi umeifanya chadema kuwa imara na chama kikubwa cha upinzani katika historia ya nchi hii.

Jambo ninalokubaliana nalo kwa kiasi na huyu kada wa ccm ni suala la chadema kumtumia vizuri zitto, sielewi ni kwanini zitto hasimami kukitetea chama chake kwa dhati na kwa sauti dhidi ya propaganda za udini., tumeona zitto anakubalka sana mtwara na tanga ambako kuna waislam wengi, mi nashauri zitto aende huko mara kwa mara ili kujibu maswali yaliyo mioyoni mwa watu kuhusu chadema ambayo wameambiwa na maadui wa chadema kuwa kinafungamana na ukristo na wakristo, kwa kuwa hakuna wa kutoa majibu kwa maelezo haya, wengi wanaamini hivyo na ni lazima wajibiwe na mtu wanayemwamini sio yeyote tu, na kwangu zitto na prof safari wanafaa zaidi kufanya kazi hii, chadema wakishinda propaganda ya udini, hakuna kizuizi kwao kushinda uchaguzi ujao
 
Mm nashangaa hakuna mbunge wa ccm aliyepita kura za maoni bila kutoa rushwa....hili ni janga wananchi wenyewe wanasema wziwazi ....ccm wananunua madaraka
 
Mnashangaa rushwa wabunge ccm,wakati mmenunuliwa chama kizima,mmewekwa kwenye gunia na kuuzwa kwa mwenye magunia sasa mnaburuzwa tu,kwa bei msioijua..Muulizeni Mbowe kavuta ngapi?
 
the horse, mwendo wa chadema kuelekea kwenye mageuzi ya kweli ni mzuri sana, mtu yeyote wa ccm kuja kutoa ushauri hapa wakati chama chake mwenyewe kinaelemewa vibaya sana na chama hiki hiki anachokipa ushauri ni uhuni wa kupitiliza.

kuna mambo ya kufanya hapa na ambayo ni muhimu, chadema iendelee kujitambulisha na wanyonge, basi!
nguvu ya chadema iwe kwa watu wanyonge na iendelee kutenda haki kwa wengine.

Hayo mawili yataiinua chadema, na sio kuwalea watu kwa mujibu wa dini zao au makabila yao. Mpaka sasa ubunifu wa viongozi umeifanya chadema kuwa imara na chama kikubwa cha upinzani katika historia ya nchi hii.

Jambo ninalokubaliana nalo kwa kiasi na huyu kada wa ccm ni suala la chadema kumtumia vizuri zitto, sielewi ni kwanini zitto hasimami kukitetea chama chake kwa dhati na kwa sauti dhidi ya propaganda za udini., tumeona zitto anakubalka sana mtwara na tanga ambako kuna waislam wengi, mi nashauri zitto aende huko mara kwa mara ili kujibu maswali yaliyo mioyoni mwa watu kuhusu chadema ambayo wameambiwa na maadui wa chadema kuwa kinafungamana na ukristo na wakristo, kwa kuwa hakuna wa kutoa majibu kwa maelezo haya, wengi wanaamini hivyo na ni lazima wajibiwe na mtu wanayemwamini sio yeyote tu, na kwangu zitto na prof safari wanafaa zaidi kufanya kazi hii, chadema wakishinda propaganda ya udini, hakuna kizuizi kwao kushinda uchaguzi ujao

Hawana kauli mbele ya jahilia na dikteta mcheza Disco aliyetoa hatimiliki ya chama kwa Jamaa yake
 
Back
Top Bottom