Waraka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA; fanyeni haya...!


TandaleOne

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Messages
1,619
Points
1,250
TandaleOne

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2010
1,619 1,250
Nalazimika kuandika kwa Uhai wa Taifa hili, nimeyakumbuka maneno ya Muasisi wa taifa hili aliyepata kusema kuwa bila kwa kuwa "Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba" na kwa hali ya sasa ya kisiasa ndani ya Taifa hili linaloundwa na nchi mbili ya Bara na Visiwani, ni vema kauli hiyo pia ikipewa tafsiri nyingine kwa maana "bila upinzani makini na wenye nguvu CCM itakuwa si madhubuti na hivyo nchi yetu itayumba" hii inamaanisha kazi ya kuistua CCM na kuikumbusha majukumu yake hufanywa vyema na wapinzani, na hivyo kuifanya ibaki madhubuti.

Leo nitaandika waraka huu kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA nimtajie baadhi ya Tofauti za msingi baina ya Chadema na CCM.,na nini CHADEMA wafanye kama wapinzani ili kuleta Upinzania Makini hapa nchini, nitaanza kuzitaja tofauti hizo na kisha kuifafanua moja baada ya nyingine;

(i) NAMNA YA KUSHUGHULIKIA CHAGAMOTO NDANI YA CHAMA;

CCM wanapovumbua ukweli ambao unawatafuna kama tatizo la mafisadi, rushwa kwenye chaguzi zao, upendeleo n.k mara moja hutafuta suluhisho la matatizo yao na hivyo huwaponya na kuwaondoa katika misukosuko waliyokuwa nayo.

Walipata matatizo makubwa kwenye uchaguzi 2010 kutokana na kuboronga kwa Makamba na Sekretarieti yake, mara moja wakavunja sekretarieti ile na kuunda nyingine chini ya Mukama.,na baada ya mwaka mmoja wa utendaji na kuonekana kuwa CDM inapata nguvu kwa ulegelege wa sekretarieti hiyo Mwenyekiti akapitishia azimio la kuunda sekretarieti mpya chini ya Mzee Kinana kada wa muda mrefu wa chama cha mapinduzi na mwanasiasa nguli mwenye kufahamu chama na wanachama.,pembeni yake Mangula.,asiyeongea bali hutenda.,asha-rose migiro Mama mwenye jina kimataifa akakabidhiwa kazi ya kufanya lobbying and she is pretty lobbyist unategemea taswira ya CCM itakuwaje chini yake.,pembeni mama Zakhia mchumi mzoefu aliyeeendesha na kusimamia uchaguzi wa CCM 2010, uchaguzi ambao ulitumia kiasi kikubwa cha pesa lakini hakuyumba kuzitafuta na kuzipangia matumizi.

Haya yanafanyika ili kuinua hadhi na kuongeza kasi ya chama ili kiimarike zaidi na kuendelee kushika dola.,haya hayakufanywa ila baada ya CCM kukiri na kuyakubali mapungufu yao kama taasisi ya siasa na kufanya SWOT analysis ya kina hivyo kubaini udhaifu wao na kuutafutia dawa hii.,na hivi sasa kila mwanaCCM na hata asiye mwanaccm bali mtanzania mwenye fikra za sawa sawa anakiri kuwa safu hii ni ukuta wa chuma. Tofauti na CDM.

CDM watakufa kifo cha kimya kimya kwa uzito wa kufikiri na kujifanyia tathmini.,kwa maana wanapobainishiwa tatizo wao hawajadili juu ya kuondokana na tatizo hilo na badala yake hubaki wakijipa moyo na kukithiri kwenye propaganda.,walikuja na mtaji wa kutaja mafisadi hoja ambayo kwa sasa haina mashiko wala nguvu miongoni mwa critical thinker kwa kuwa wanataja na kisha hawathibitishi wala hawaendi mbele kuyasimamia madai yao lakini pia wanakosoa kwa Unafsi zaidi kwa maana wanapinga kila kitu ambacho serikali ya Chama Cha Mapinduzi wamekuja nacho, maendeleo yote wakadai hakuna kilichofanyika, na watu wanaona shule, hospitali mabarabara, treni za mjini na majengo ya fahari makubwa yakijengwa na serikali.,wanaona kufufuliwa shirika la nyumba na mengineyo.,watu wa tanzania sio mazezeta wanaona haya na watahukumu kwa haya.

matokeo ni kuwa CDM inaendelea kujisahaulisha mapungufu yake na kujitoa ufahamu wa kasoro zake.,haya ya kupanga safu za wachaga vyuoni ni gumzo lililopo sasa hivi huku katika vyuo vya elimu ya juu na watu wanaambiwa haya ili wajirekebishe na kujipanga upya kuelekea 2015.,wao wanakanusha na kujitoa ufahamu. watakuja kuona impact ya jambo hili baada ya 2015 pale watakapolalama kuwa wameibiwa kura na kuendelea kudai kuwa kuna kontena za kura zimeingizwa nchini kama alivyodai 2010. Ni ujinga na kujipunguza ufahamu kuyafanya haya. JIPANGENI.

Ondoeni tatizo la ukabila ndani ya chama Chenu, wahakikishieni wananchi kuwa chama chenu kina sura ya utaifa kwa kubadili muonekano wa sasa na taswira ya ukabila iliyotawala chama chenu sasa, haya yatawasaidia. Nendeni mtwara waambieni wamakonde kuwa hata BABA KUNDAMBANDA nae ana nafasi katika chama chenu.,wapo wamakonde wachache vyuoni groom them ama mmoja wao kisha mtumieni as icon kuwa anawa-represent watu wa kusini.,tafuta mpemba mmoja mpeni Uenyekiti wa tawi la chuo kikuu kimoja kisha fanyeni propaganda ya kutosha kuwa hata wapemba nao wamo chadema.

Waambieni makasisi na mapadri waache kuwaongelea hoja zenu.,waache kujihusisha na CHADEMA na pia nendeni kwa masheikh waambieni mko nao pamoja, pelekeni michango ya ziara zao na maulid yao kama wafanyavyo CCM, msifanye harambee makanisani pekee nendeni madrasa pia wafanyieni harambee wapo waislamu katika CDM kama zito mtumieni akayafanye haya na muache kumpiga vita na kumzushia mambo ya uongo kwa kudhihirisha chuki yenu kwake acheni kuyafanya hayo na waislamu watawapokea na kuwakubali kwa dhati ya mioyo yao., hiyo ndio SIASA.

Msitumie maandamano na kusababisha watu kufa bila sababu za msingi kwa woga wa kifo watu watashindwa kuwaunga mkono bali nendeni kwenye vijiwe vyao kaeni nao chini fanyeni strategic movement zenye malengo, zitawaimarisha kimya kimya bila kufa mtu bila damu kumwagika, yafanyeni hayo. January Makamba amekutana na wanabumbuli na kuwaalika wapigadebe na wauza kahawa pamoja na makuli wa k.koo kwa nembo ya wasambaa wanabumbuli lakini hili liliungwa mkono na makuli wote wa K.koo na wakamuona January kuwa ni mtu bora kwao. Mpeni nguvu zito atengeneze LEKA DUTIGITE nyingine yenye taswira kubwa zaidi ya muziki.,afanye kitu chenye maendeleo kama kuwakusanya wanakigoma kwa ajili ya harambee za kujenga mabweni ya shule, hospitali na kadhalika, haya yatawasaidia kukijenga chama chenu.,wajerumani wanawapa pesa NYINGI pamoja na serikali na vyama vingine kama labour ya uengereza.,make effective disbursement kwa makundi yenye nguvu katika jamii, sio kwa kununua ndege na helikopta.,ama kwa kufadhili movement zisizo na tija kama M4C ambayo imeshindwa kuzaa matunda hata baada ya kutumia hazina kubwa ya pesa za chama na wahisani. Fanyeni haya.,

Mwambieni BABU slaa kuwa NAPE ameshamchakaza sasa amwache Mnyika aongee zaidi na apambane na kijana mwenzake, wapiga kura wa leo wanataka sura inayofanana na wao, Mnyika ni mwenezi wa CHADEMA lakini kwanini BABU anapenda kuuza sura zaidi kwenye medias yeye kuliko mnyika, hata kama anapenda ujana kwa kuchelewa kuoa na kuzuga na uchumba wa miaka kibao bado hilo halimrudishii yeye sifa ya ujana. Eligible voters wa sasa ni vijana wapeni mtu atakaeongea nao katika lugha yao.

Mwambieni John Heche kuwa ameshindwa kazi na anahitaji kupumzika, amesahau kuwa kazi yake ni kuwaunganisha vijana wa chadema na kuwajengea matumaini ya kuchukua nchi na kuleta mabadiliko ya kweli, bali asitumie platform ya BAVICHA kupanga safu ya utawala ndani ya CHADEMA kwa kuimarisha kundi fulani la wakubwa fulani ndani ya Chama hicho. Mwambieni kazi yake ni kuiunga CHADEMA sio kuimarisha makundi, asiyaige yale ya UVCCM ya Beno Malisa. Wekeni wazi kwa vijana wenu kuwa vijana wote wanathamani si wasomi pekee ama wanafunzi wa vyuo vikuu.,siasa ya vijana haipo vyuoni pekee ingawa ni sehemu muhimu pia, bali mtaani kuna wengi zaidi kuliko wale wa vyuoni. Mwambie Lema amfundishe HECHE namna ya kudeal na vijana wa mtaani, na mwambieni SUGU kuwa amesahau asili vijana wa mtaani hawamuelewi.,ameshindwa kuwatafutia vijana wa mbeya machinga wenye hali ngumu sehemu yenye kueleweka na yenye hati ya kisheria kufanya biashara zao, na anaendelea kuacha wanateseka kwa kupigwa na kuteswa na mgambo.,mwambieni anajisahau..,

Msimzibe mdomo Zitto mwambieni wakiridhia wanachadema atagombea urais kisha mtatumia vizuri na klushirikiana na nyinyi katika vita hii nzito bila kujigawa, msiendelee kumjengea uadui mkamfanya ajiimarishe yeye zaidi dhidi yenu, bali mwambieni kuwa afanye kazi ya chama wanachadema wakiridhia kwa kazi yake ndani ya Chama watampa ridhaa, then mnajua mtakachofanya kwenye utaratibu wa kura za maoni ya kuchagua Mgombea, ninyi bado mnayo nguvu kuliko yeye, hasa kwa safu mliyoipanga hivi sasa katika vyuo vikuu na BAVICHA.

Yawezekana kusikia hamsikii lakini hata haya MAANDISHI HAMYAONI..???
 
B

blueray

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Messages
2,219
Points
0
B

blueray

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2012
2,219 0
Upuuzi mtupu!

Kawaulize waliokutuma; kama ya CDM hayafai mbona mnaya-copy na kuya-paste?
 
DALLAI LAMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Messages
8,612
Points
1,500
Age
37
DALLAI LAMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2012
8,612 1,500
Duh gamba lililovaa kilemba cha Kikamanda kumbe ni KADA..pointless
 
P

politiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Messages
2,376
Points
1,250
P

politiki

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2010
2,376 1,250
"CCM wanapovumbua ukweli ambao unawatafuna kama tatizo la mafisadi, rushwa kwenye chaguzi zao, upendeleo n.k mara moja hutafuta suluhisho la matatizo yao na hivyo huwaponya na kuwaondoa katika misukosuko waliyokuwa nayo."

KAMDD
KKama vile walivyomshughulikia fisadi Chenge na wenzake ktk issue ya Radar ....Good, kagoda waliwakamata wahusika wote akiwemo MAMA ZAKIA MEGHJI alyeuambia umma wa watanzania kuwa pesa zimetumika jeshini wakati zimekwenda SA, au kama vile walivyomshugulikia KINANA aliyetajwa na Kamati ya Bunge(1992) kampuni yake kujiusisha na biashara ya vipusa. na vile vile kampuni yake kukamatwa tena mwaka huu (2012) na kukutwa na nyara... ilimshugulikia Mangula kwa kujiusisha na issue ya wizi wa pesa hazina kwa ajili ya kampeni ya CCM alishugulikiwa na hivi sasa yuko jela. Hongera sana CCM kwa kutupa maisha bora kila mtanzania
 
LiverpoolFC

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Messages
11,021
Points
1,250
LiverpoolFC

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2011
11,021 1,250
Tulianza na MUNGU na tutamaliza naye!


ccm wao wana pesa nasi tuna MUNGU na hakika yu hai!
 
W

WATANABE

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
1,091
Points
1,195
Age
59
W

WATANABE

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
1,091 1,195
Ama kweli umdhanie kumbe siye. leo nimejifunza jambo moja kuwa chukua muda msikilize au soma mada za mkosoaji wako utajifunza kitu. Nilikuwa nikiona jina la TANDALE ONE tu hupata kinyaa kwa jinsi alivyokuwa akiegemea upande mmoja. Lakini yote uliyosema katika mada hii ni ukweli mtu pua hususan suala la CCM kufanya SWOT ANALYSIS na kuchukua hatua haraka kurekebisha hali hiyo.

Nafikiri hata CDM sio malaika wana mapungufu kibao na kwa kuwa wapo pale walipo kutokana na kodi zetu ni lazima na wao tuwakosoe ili Tanzania ya leo na kesho iweze kuwa na sysytem of "ADEQUATE CHECKS AND BALANCES". Na TANDALE ONE kama mmoja wa wapinzania w CDM mkubwa sana leo nakuppongeza kwa kufanya kitu kinachoitwa "CONSTRUCTIVE CRITICISM" ukionyedsha udhaifu na namna ya kuurekebisha. Hivyo ndivyo watanzania tunavyopaswa kuwa na kubehave badala ya kuwa na ushabiki wa kisiasa usio na tija.


Nakupongeza sana na kukuombe moyo wa uvumilivu kama amabavyo sisi wakosoaji wa CCM, utatukanwa na kudhalilishwa na hata kuchukiwa wakikufahamau lakini kwa kuwa unatekeleza dhamira yako BID UP!!!
 
W

WATANABE

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
1,091
Points
1,195
Age
59
W

WATANABE

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
1,091 1,195
"CCM wanapovumbua ukweli ambao unawatafuna kama tatizo la mafisadi, rushwa kwenye chaguzi zao, upendeleo n.k mara moja hutafuta suluhisho la matatizo yao na hivyo huwaponya na kuwaondoa katika misukosuko waliyokuwa nayo."

KAMDD
KKama vile walivyomshughulikia fisadi Chenge na wenzake ktk issue ya Radar ....Good, kagoda waliwakamata wahusika wote akiwemo MAMA ZAKIA MEGHJI alyeuambia umma wa watanzania kuwa pesa zimetumika jeshini wakati zimekwenda SA, au kama vile walivyomshugulikia KINANA aliyetajwa na Kamati ya Bunge(1992) kampuni yake kujiusisha na biashara ya vipusa. na vile vile kampuni yake kukamatwa tena mwaka huu (2012) na kukutwa na nyara... ilimshugulikia Mangula kwa kujiusisha na issue ya wizi wa pesa hazina kwa ajili ya kampeni ya CCM alishugulikiwa na hivi sasa yuko jela. Hongera sana CCM kwa kutupa maisha bora kila mtanzania
Anachokuambia TANDALE ONE ni kuwa CDM tuklyasema hayo yote wao CCM huyasafisha na kuyaondoa uchafu kama vile Serikali ya Tanzania ilivyoshirikiana na ya Uiongereza kusafisha kashfa ya Radar. TANDALE ONE anatukumbusha jambo moja la msingi kuwa binadamu ameumbiwa kusahau ndio maana hata akimpoteza mzazi, mtoto wake baada ya hjusahau na uchunngu hupotea. Ni kweli kuwa 2010, watanzania walio wengi walikuwa na uchungu wa UFISADI unaoutaja. lakini hivi sasa EPA, KAGODA, MEREMETA n.k ni sawa na ukitaja suala la nduli Iddi Amin si wengi wanoshituka na kusiskia mishipa ya damu ikijaa.


Lakini nafasi ya kuhakikisha haya yote yanashughulikiwa kisheria ni kwa wapinzania kukamata dola. na hili kukamata dola ni lazima kufanya mambo fulani fulani ili kukukabalika Tanzania nzima.
 
Ngagarupalu

Ngagarupalu

Senior Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
156
Points
0
Ngagarupalu

Ngagarupalu

Senior Member
Joined Oct 13, 2012
156 0
Tandale One: Hongera kwa mchango wako. haya uliyo yatoa hapa ni muhimu sana, hata kama hayatafanyiwa kazi, ila msg send! Kwa kweli CDM kuna sehemu wanashindwa kupagusa, sasa ni wakati wa kukaa na kujitathimini nini wamepata kwenye M4C, najua wamepata mambo mengi sana, mikoani vijana wameibuka na wanataka mabadiliko, hii pia imewatisha wao na CCM pia. Na hisi CDM imekua kwa kasi kiasi hawawezi amini, hivyo badala ya kujipanga wanaweweseka.

CDM, wanatakiwa sasa kupiga underground kwanza kabla ya kwenda angani kwa tukutuku!! wajenge uwezo kwa Vijana waliopo mtaani, ambao wakiamua wataleta mabadiliko ya dhati na kweli!! watoe mafunzo na mihadhara ya kutosha. Vijana kimikoa, ki wilaya wapewe uwezo wajichague, (ingawa lazima wasimamiwe) Kisha wawe na sura ya kitaifa. Ngoja tuone ziara ya secretariate ya CCM mikoani inazaa nini, pengine watafunua ukurasa wako, na wakosaji wengineo.

Wana cdm wa humu jf mje na majibu ya hoja ya mapungufu ya CDM, utengano wa Zitto na chama, uingizaji wa wanachama wapya na mikakati ya ukuaji wa chama kwenye grass route, tunataka majina mapya, sura mpya hasa mikoani!!

Hivi CDM wana idara ya kina-mama? na ipo chini ya nani? hata muundo wa CDM jaribuni kuubadilisha , usiwe sawa na sisiem
Wakatabahu
 
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Messages
15,855
Points
2,000
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2009
15,855 2,000
M4C imepata manufaa makubwa,kwa sasa kila kona bendera ya cdm inapepea!IENDELEE KWA NGUVU ZOTE
 
F

FredKavishe

Verified Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,091
Points
1,195
F

FredKavishe

Verified Member
Joined Dec 4, 2010
1,091 1,195
Mambo haya yakuyafanyia kazi tuache dharau kiongozi imara ni yule anayejifunza kutokana na makosa
 
M

Mnyonge Namba1

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Messages
402
Points
0
M

Mnyonge Namba1

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2012
402 0
Jamaa kajaza pipa mbili za povu la mate. Pro magambas wanataabika sana aisee
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,658
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,658 2,000
cdm itakufa kabla ya 2015-wassira
naona vijana wake wamechachamaa sana humu jf
 
Lukolo

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
5,149
Points
1,250
Lukolo

Lukolo

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
5,149 1,250
Upuuzi mtupu!

Kawaulize waliokutuma; kama ya CDM hayafai mbona mnaya-copy na kuya-paste?
Huu ndiyo uendawazimu wa wanachadema. Hivi umesoma vizuri message iliyomo ndani ya hiyo makala? Au umekurupuka tu kujibu ilimradi uonekane umejibu. Kwa utaratibu huu wa kutokujali ushauri mnaopewa na watu wengine, hamtakaa mshike nchi? Na mtaendelea daima kuwa wasindikizaji tu wa CCM na mwisho wa siku chama chenu kitakufa kama kilivyokufa CUF. Huyu bwana ana hoja makini sana kama zikizingatiwa. Naamini viongozi wa CHADEMA ni makini na wasikivu, kwa hakika watamwelewa TandaleOne anasema nini, na watafanyia kazi mawazo yake. Achaneni na itikadi zake, chukueni ujumbe wake.
 
Last edited by a moderator:
Expedito Mduda

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Messages
380
Points
225
Expedito Mduda

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2009
380 225
Ngoja niseme vizuri ili nielewe ndo niseme
 
T

the horse

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Messages
579
Points
225
T

the horse

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2011
579 225
Kama kuna wakati na kama kuna mtu wanatakiwa wampe shukrani zao za dhati ni tandaleone kwa hili., ameonyesha ni kwa kiasi gani wananchi wa nchi hii wanatakiwa waishi kama watu wa taifa moja.,kwa kuonyesha ni kwa kiasi gani watu wa taifa hili tunategemeana hata kama tunapingana na kukinzana katika baadhi ya mitazamo na hoja.
 
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2010
Messages
4,891
Points
0
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined May 10, 2010
4,891 0
Mbona hujibu ile orodha yako ya viongozi wa miaka mitano wa chadema vyuo vikuu?

Mjomba tanda vipi au wewe unalipwa kwa post mpya tu?

Uliyoyasema yanaweza kuwa na ukweli ila ni sawa na kumfuta adui yako na kmwambia mtoto wake ana njaa na chakula unacho unaomba kumlisha.
Kweli anajua mtoto ana njaa ila kumbuka ulishamtangazia ama zake ama zako.
 
Bigirita

Bigirita

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
15,629
Points
2,000
Bigirita

Bigirita

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
15,629 2,000
Insanity is a talent to some of you.
 

Forum statistics

Threads 1,294,755
Members 498,034
Posts 31,187,163
Top