Waraka kwa CCM na TLP juu ya meya Arusha Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka kwa CCM na TLP juu ya meya Arusha Mjini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nanyaro Ephata, Jul 21, 2012.

 1. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 965
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  [FONT=&amp]WAHESHIMIWA MADIWANI,[/FONT]
  [FONT=&amp]CCM NA TLP[/FONT]
  [FONT=&amp]HALMASHAURI YA MANISPAA YA ARUSHA[/FONT]

  [FONT=&amp]YAH: MGOGORO WA MEYA ARUSHA MJINI[/FONT]

  [FONT=&amp]Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Sisi Madiwani wa CHADEMA tumefikiri na kutafakari kwa kina kuhusu mustakabali wa maendeleo ya wananchi wa Manispaa ya Arusha Mjini. Kwa nafasi yetu ya wawakilishi na utetezi wa wananchi Arusha kwa umoja wetu ni vema tufikiri na tutafakari kwa kina kwa pamoja hasa kipaumebele ikiwa ni kutanguliza HAKI na MAENDELEO katika kumlenga kila mkazi wa aliyepo katika Halmashauri yetu. NI vema tukawa WAKWELI na WAZELENDO kwa wananchi wetu wa Arusha, huku wote tukijua kwa kina kile kilichotokea Arusha.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa muda mrefu kumekuwa na mgogoro wa Uchaguzi wa MEYA wa manispaa ya Arusha, ambayo ilitokana na ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uchaguzi wa Meya ambayo akidi yake ilikuwa haijatimia. Ikumbukwe kuwa Mhe. Kivuyo ambaye katika sakata hilo alijikuta akichaguliwa kwa hila kuwa NAIBU MEYA, alifikia hatua ya kujizulu nafasi hiyi na kukiri mbele ya waandishi wa habari na wananchi wa Arusha kuwa uchaguzi uliofanyika haukuwa wa haki na yeye alipewa nafasi hiyo kwa hila, kitu ambacho baada ya tafakari ya kina aliamua kujiuzulu ili asiwe sehemu ya dhambi hiyo na kujikuta anakalia KITI CHA DAMU. Jambo hili pia limekuwa likisemwa na baadhi ya madiwani wa CHAMA CHA MAPINDUZI pindi tunapokutana nao kuwa mfumo wa chama cha CCM unazuia kuyatamka haya lakini ukweli ni kuwa huo uchaguzi wa meya uliofanyika na Mhe Gaudence Lyimo kupata nafasi hiyo ulikuwa batili kwa mujibu wa kanuni, lakini mbaya zaidi, umepelekea damu kumwagika, jambo ambalo ndio baya.[/FONT]

  [FONT=&amp]Wote tunashuhudia jinsi ambavyo mgogoro huu ulivyo na madhara makubwa sana kwa wananchi wetu na sisi pia ambao ni sehemu ya jamii hiyo hiyo. Mbali na kusababisha watu watatu kupoteza maisha, pameendelea kutokea sintofahamu kubwa kutoka kwa wananchi jambo ambalo limeendelea kuzidisha hasira kwa wananchi kwa serikali. Jambo hili ni vema likafanyiwa kipimo maana mchezo huu na hila hii inaweza kuzaa balaa ambalo sio rahisi kulimudu tena. [/FONT]

  [FONT=&amp]Dharau na makusudi yanayofanywa na chama cha mapinduzi, mathalani Mhe Gaudence Lyimo na MKURUGENZI wa halmashauri katika kupuuzia wito wa CHADEMA kuwa HAKI haikutendeka, KANUNI zilivunjwa na hivyo uchaguzi wa MEYA ufanyike upya kwa kufuata kanuni sasa inafika mahali haivumiliki na hapo ndipo itakuwa mikononi mwa wananchi na sio CHADEMA tena. [/FONT]

  [FONT=&amp]Sambamba na hali hii, pia mgogoro huu unatumiwa na watendaji wa Halmashauri kufanya mambo yao yasiyo ya kiuadilifu kwani hakuna udhibiti wa kabisa katika uendeshaji wa halmashauri yetu. Waheshimiwa madiwani, katika ukweli huu, MKURUGENZI na huyo anayeitwa MEYA watatoa wapi ujasiri na kujiamini “moral authority” ili hali wao wameshiriki dhambi mbaya ya kuchakachua kanuni za kufanya uchaguzi wa meya isivyo halali na mbaya zaidi Mhe Gaudence kuendelea kung’ang’ania nafasi hiyo kwa kiwango cha damu ya watu kumwagika bila hata kujali??[/FONT]

  [FONT=&amp]Hata hivyo, hata kama Mhe Gaudence Lyimo hatajali wito huu ambao kwetu ni wito wa mwisho kwake na chama chake, jambo hili tunaliacha kwa MUNGU mwenye HAKI atashughulika nae kwa wakati wake na muda si mrefu tutapata majibu ya maombi yetu. Pili tunaliacha jambo hili kwa wananchi ili waamue kwa sababu wameshajua wazi kuwa Mhe Gaudence Lyimo na chama chake waliamua na wameendelea kuwafanyia uhuni katika mji wao. Sisi tumeliacha kwao waamue watakavyoamua.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tunafahamu kabisa katika nafsi na mioyo yenu mnafahamu uchaguzi haukuwa halali lakini mnashindwa kusimamia ukweli kwa sababu ya ubinafsi na kukosa uzalendo kwa wananchi wa Arusha kwa kutanguliza maslahi yenu mbele, kitu ambacho tusingependa kipewe tafsiri hiyo.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Tunawasihi kwa dhati kabisa tuamue kwa pamoja kwa manufaa ya Arusha tukubaliane kama viongozi wazalendo, wapenda maendeleo na wenye hofu ya MUNGU tufanye uchaguzi wa MEYA wa Halmashauri ya Arusha ambao utakuwa ni halali kwa vyama vyote. [/FONT]

  [FONT=&amp]Nchi nyingi za Afrika kumekuwa na vita vya wao kwa kwao kwa sababu ya uchu wa madaraka. Hili limetokea pia hapa Arusha watu wamekufa kwa sababu ya MEYA, hii ni aibu na ni dhambi kwa kung’ang’ania madaraka ambayo si haki. [/FONT]

  [FONT=&amp]Waheshimiwa madiwani wenzetu hata juhudi za serikali kufanya maendeleo wananchi wengi wa Arusha bado hawana imani na serikali yao kwa sababu ya MEYA tu. Hivi sasa kuna mradi wa ujenzi w barabara unaondelea ukweli ni kwamba jambo hili ni zuri lakini wananchi wanalibeza sana kama vile linafanywa kwa hila. Kwa nini iwe hivi?? [/FONT]

  [FONT=&amp]Kimsingi tunataka MEYA ambaye yupo huru kutembelea kata zote kwa ajili ya maendeleo bila kujali itikadi ya chama chake. Hatutaki MEYA anayevizia misiba na harambee.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Mwisho tunamwomba Mh. Gaudence Lymo atafakari kwa kina kwa kumuomba MUNGU wake ampe hekima na ujasiri wa kuchukua maamuzi magumu ya kujiuzulu nafasi ya UMEYA na uchaguzi wa kidemokrasia ufanyike kwani utampa heshima na amani katika maisha yake yote.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Tunaomba Waheshimiwa Madiwani wenzetu kwa pamoja tuseme dhambi hii imetosha na tutubu kwa kufanya uchaguzi wa haki na Amani. Na kwa dhati kabisa yeyote atakayechaguliwa hata kama ni Mh. Gaudence tutampa ushirikiano wa dhati kabisa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tunaomba ushirikiano wenu katika jambo hili ambalo ni la msingi kwa maendeleo ya watu Arusha. Kila mmoja kwa imani yake aombee jambo hili kwani halitaki ushabiki linahitaji utulivu wa akili.[/FONT]

  [FONT=&amp]WAHESHIMIWA MADIWANI, FANYENI TAFAKARI YA KINA, ZINGATIENI JINSI WANANCHI KATIKA KATA ZENU WANAVYOWATAZAMA, ni matumaini yetu kuwa tutafanya uchaguzi wa MEYA ndipo tufanye uchaguzi wa Naibu MEYA. Na jambo hili litakuwa ni ushindi na sifa iliyotukuka kwa MADIWANI WOTE na sio kundi fulani la watu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Asanteni sana[/FONT]

  [FONT=&amp]Doita Isaya Harri[/FONT]
  [FONT=&amp]Mwenyekiti madiwani wa CHADEMA[/FONT]

  [FONT=&amp]Nakala:[/FONT]
  [FONT=&amp]Katibu wa CHADEMA (M)[/FONT]
  [FONT=&amp]Katibu wa CCM (M)[/FONT]
  [FONT=&amp]Katibu wa TLP (M)[/FONT]
  [FONT=&amp]Mkurugenzi wa Halmashauri – Arusha Mjini[/FONT]
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Waraka huu ni wa zamani sana wakati mgogoro umepamba moto ingawa umeletwa hapa kama wa siku za karibuni..... hauna tarehe kulikoni?
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Maandishi mazito na mazuri kwa namna yake
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,898
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  mnamwandikia mwizi barua,kweli tanzania kuna demokrasia ya namna yake.
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hakuna kitu hapo
   
 6. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,929
  Likes Received: 2,994
  Trophy Points: 280
  No comment
   
 7. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,822
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha na kuuzunisha sana kuona mtu anataka kuzaa bila kubeba ujauzito.
   
 8. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,003
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  hivi rufaa ya mbunge wangu kamanda lema itasikilizwa lini wakuu,???:noidea:
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,153
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Wanasubiri wamalize ujenzi wa barabra, wanadhani watu wa Arusha ni wajinga kiivyo, wao wanaamini wangejenga barabara akiwa mbunge lema wangeipa sifa chadema...
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,153
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Wakizingua kamanda kinukisheni tu sisi vijana wa Arusha tutawasapoti...
   
 11. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,189
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Wamechemkaaaaa na watasubiri hadi 2015 uchaguzi mkuu!!
   
 12. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,003
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  si Arusha nnayoijua mimi mkuu,....tunawasubiri kwa hamu kwenye vote...
   
 13. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 17,338
  Likes Received: 3,615
  Trophy Points: 280
  Hujaeleweka EK!!
   
 14. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,328
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  Huyo anayejiita meya ni wa ukoo, familia na watoto wake. Arusha hatuna Meya. Full stop.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Chedema yasusia uchaguzi wa Naibu Meya Arusha
  MADIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Arusha wamechafua hali ya hewa kwa kususia uchaguzi wa Naibu Meya Halmashauri ya Manispaa ya Arusha, kitendo kilichosababisha uchaguzi huo kukwama kwa mara nyingine.

  Hatahivyo, katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya maofisa wa Usalama wa Taifa pamoja na askari wa Jeshi la Polisi wakiwa na magari yao, jana walionekana kwa wingi wakirandaranda nje na ndani ya ofisi hizo kitendo kilichoibua maswali mengi.

  Akifungua kikao cha Baraza la Madiwani kabla ya kuanza kujadili ajenda mbalimbali za kikao hicho, Meya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo alisema anashangaa ni kwa nini madiwani wa Chadema wasusie kikao hicho wakati walikubali mwafaka na kumtambua yeye kama meya.

  Pia, alisema awali madiwani hao walikubali mwafaka ili wawaletee
  maendeleo wananchi lakini alihoji watu hao hao waliokubali mwafaka leo hii kususia vikao na kumtishia maisha huku wengine wakisema hawamtambui yeye kama meya.

  Lyimo, alisema kuwa kikao hicho kilikuwa na ajenda tatu muhimu ambazo ni kuchagua wenyeviti wa kamati mbalimbali, kupitia taarifa za mapato na matumizi pamoja na uchaguzi wa Naibu Meya, ambaye alitakiwa kutoka Chadema, lakini cha ajabu chama hicho hawajaleta jina wala kuhudhuria kikao hicho.

  Alisema kutokana na madiwani wa Chadema ambao ni saba kususia kikao hicho walikubaliana na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuachana na ajenda hiyo mpaka kikao cha dharura kitakapoitwa kujadili suala hilo.

  "Kikao hiki kina washiriki 23 ambapo watano kati yao ni wabunge na 18 ni madiwani, ila kwa leo wapo madiwani 12, tumefika nusu ya kolamu, ila madiwani wa Chadema wameandika barua na kueleza sababu zao za msingi za kususia kikao hiki kuwa wanataka uchaguzi wa Meya ufanyike tena na kuitaka Serikali kukubali uchaguzi urudiwe ili apatikane Meya halali ndipo wao washiriki," alisema Lyimo.

  Alisema barua hiyo waliyoandika Chadema na kuipeleka kwa
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha, pia ilikuwa na ikitishia maisha watu iwapo hawatafanya uchaguzi wa Meya, jambo ambalo siyo halali.

  Alisema kuwa, anakishangaa chama hicho, iwapo kama wameona
  hawakutendewa haki, mahakama ndiyo sehemu ya kukimbilia, ambako hawataki kwenda badala yake wanagoma na kuwatishia watu maisha na kusisitiza ni Mungu pekee ndiye anayekuwa mlinzi wa watu aliyewaumba.

  Lyimo alisema, anakumbuka walifanya kikao Juni 20 mwaka jana 2011 na pande hizo mbili na kukubaliana mwafaka na kuwapa nafasi ya Naibu Meya Chadema, ila anashangaa kuona wamegeuka makubaliano hayo.

  Alisema kikubwa kilichopo ni kuwaletea wananchi maendeleo na siyo kulumbana, kwa sababu hawakuchaguliwa kuendesha malumbano.

  Upande wa madiwani wa CCM, wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Olasiti, Ismail Katamboi alisema kuwa, kwa sababu Chadema wamekataa kuleta jina la Naibu Meya wamevunja kanuni na maazimio ya mwafaka wao ambao walikaa na kupongezana basi iwekwe katika kikao kijacho kama ajenda na watoe uamuzi wao.

  Hali hiyo ilimlazimu, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Omary
  Mkombole kusimama na kuingilia kati na kuwataka madiwani kuacha kujadili suala hilo kwani siyo kikao cha kujadili suala la mwafaka na kushauri madiwani hao kujadili suala hilo kikao kijacho kitakachoitwa kwa dharura.

  Naye mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema, Isaya Doita, alitoa tamko kwa niaba ya madiwani wenzake saba kuwa hawatashiriki uchaguzi wa Naibu Meya kwa kuwa uongozi wa chama hicho ngazi ya Wilaya ya Arusha uliandika barua Julai 14 mwaka huu, yenye kumbukumbu nambari MD/E40/10/VOL 11 kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo wakimtaarifu kutoshiriki uchaguzi huo na kumtaka aitishe kikao cha uchaguzi wa Meya wa Arusha.

  Alisema Chadema hawawezi kuteua mtu kwa nafasi ya Naibu Meya wakati hawatambui na kutaka uchaguzi wa meya ufanyike kwa kuwa manispaa hiyo haina meya kwa sababu aliyepo alichaguliwa kinyume cha sheria.

  Doita alisema, baada ya kupeleka barua hiyo Ofisi ya Mkurugenzi Arusha ilipokewa na Julai 16 mwaka huu, ilijibiwa na Kaimu Mkurugenzi, Mkombole ambaye alisema kuwa kuhusu marudio ya uchaguzi hayuko tayari kwa sababu ofisi yake inatambua kuwapo kwa meya aliyechaguliwa kihalali kwa kufuata taratibu zote za kuendesha vikao.

  Alieleza kwamba, barua hiyo ilisema uchaguzi wa meya ulifanyika Desemba 17 na 18 mwaka 2010 ulifuata sheria na kanuni zote za manispaa na hivyo meya aliyepo kwa sasa ni halali.
   
 16. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 965
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  eti huu waraka ndio huyu anayejiita meya anadai kuwa umemtishia maisha
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,189
  Likes Received: 4,543
  Trophy Points: 280

  Binadamu tumepewa vichwa kwa ajili ya kufikiri na sio kufugia nywele.
   
 18. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #18
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 965
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  watakaotubeza na kutukejeli tunawasamehe
   
 19. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,266
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Arusha walisha lamba sukari ya cdm. Hutawaambia kitu tena.
   
Loading...