Waraka kwa bwana Malecela the Mutuz, na watoto wote wa wakubwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka kwa bwana Malecela the Mutuz, na watoto wote wa wakubwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by collezione, Feb 15, 2012.

 1. c

  collezione JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Wasalam,

  Kwanza nianze na kumpongeza bwana Malecela, Le Mutuzi. kwa wazo lake zuri la kurudi Tanzania na nia ya kuwakombia waTanzania. Nimefurahi kusikia unaenda vijijini Dodoma kusikiliza kero za wananchi. Big up for this.

  Swali linakuja, hivi ni lazima uwe mbunge ili uwakomboe waTanzania? Ambao wanaandamwa na umaskini, maradhi, na ukosefu wa ajira?

  Sio wewe tu, hata bwana Makamba junior, ametoka ughaibuni na kukimbilia siasa. Ni kweli mnataka kuwakomboa waTZ au mnakimbilia hizo posho?

  Mimi nilidhani, na mategemeo yangu makubwa ningeona mnatumia profession zenu mlizosomea uko ughaibuni kuwasaidia waTz walio kwenye shida, kama nyinyi wenyewe mnavyodai. Sina uhakika kama watoto wote wa wakubwa mmesomea political science. Mpaka wote mtake jiingiza kwenye siasa.

  Kwa experince ya kuishi ughaibuni naamini mmejifunza mambo mengi mazuri. Ambayo hayaitaji kuwa mwanasiasa ili uikomboe TZ yetu. Tuseme Kila mTz mwenye opportunity kama nyinyi akiwa mwanasiasa wa kuongea majukwaani. kina nani watakuwa ma-professional kutokana na fani zao. Mimi naamini tunaweza ijenga Tz sio kwa kutengeneza wanasiasa wengi. Bali kutengeneza wajuzi wa mambo. Siasa haiwezi tengeneza ajira. Wala kupunguza maradhi. Sana sana utakuwa unafaidi wewe na ndugu zako. Kwa hizo posho.

  Let's say Bwana Malecela nimesikia kuwa wewe ni mtaalamu wa computer. Kwanini usitumie talent ako kubadili maisha ya waTz. Kina Jobs na bwana Bill gates walianzaje? Wale jamaa wangekuwa wanasiasa leo tusingekuwa na apple wala microsoft.

  Ni ukweli usiopingika, familia zenu zina influance hapa Tz. Leo hii ukianzisha kampuni, utaenda tambalale, kuliko mimi ambae wazazi wangu hawajulikani popote. Cha kwanza pesa sina.

  Hapa siongelei biashara za kujuana au kifisadi. Au biashara za kuwaonea waTz. Bali Kutokana na fani ya computer au fani biashara uliyosemea nje, pamoja na experince ya maisha ya huko. unaweza kuanzisha kampuni kubwa, ambayo itaajiri watu wengi. Kuliko kuwa mwanasiasa. Pia Ungewafundisha watu wengine hapa nchini ambao hawajahi kutoka nje ya nchi kuwa wajasilia mali. Vile vile kuona opportunity zilizopo kwao, kuliko kutegemea serikari kuwaajiri.
  Au kusubiri wazungu na wachina kuja kutufundisha jinsi ya ku-explore nchi yetu.

  Nampongeza sana bwana Bhakresa na Reginard Mengi. Hawa ni wajasilia mali ambao sekta zao zinatoa ajira kwa watu wengi sana hapa Tz. Tunahitaji watu kama hawa 10 hapa Tz. Am sure swala la ajira litapungua sana.

  Mimi sipingi swala lenu la kutaka kuwa wabunge. Ila naamini mnawanyima waTz resources ambazo mnazo, na experince ambayo mmepata uko ughaibuni.
  kukubali kuwa mwanasiasa wa majukwaani. Naweza sema mmekuwa wabinafsi.

  Kuwa mwanasiasa sio njia pekee ya kubadili maisha ya waTz. Ingali waTz wengi hawana elimu wala ajira.

  Hapa Tanzania kuna changamoto nyingi. Unemployment, idadi ndogo ya education institutional. Poor Health services. Haya yote hayaitaji wanasiasa kuyabadili. Ila tunahitaji watu wenye influance and with valid professions, kama nyinyi.

  Asante
   
 2. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena!....good words!!
  kama ni msikivu atasikia na kuacha hizi propaganda mara moja!
  kuwasaidia watanzania..my a$$!
   
 3. c

  collezione JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mkuu,
  Tunategemea hawa jamaa kutengeneza ajira kutokana na fani na influance yao. Sio kukimbilia siasa. Watakuwa wabinafsi wachoyo kwa waTz wenzao.

  Sio lazima tuwasubiri wachina na wazungu watufundishe ku-explore Tanzanian. Wakati tuna big people like them
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ni mawazo mazuri, lakini kila mtu ana dreams zake regardless ya profession aliyonayo.
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu hujasikia yule mbunge aliyefariki arumeru mtoto wake anataka kurithi??hivi hao viongozi woote ukimtoa nyerere walishindwa kuwajengea watoto wao uwezo wa kufikiri????wanatumia sana matak'o kuwaza'manake sasa wanataka nini?wanafikiri wanaweza kubadilisha maisha ya mtanzania kama baba zao walishindwa?
   
 6. c

  collezione JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana wewe, it might be dreams.

  Lakini huoni kuwa wanatafuta sehemu tambarare pa kula. And lack of responsible creativity mind.

  Ni ukweli usiopingika, siasa ndo kwenye hela Tz. Najua siasa isingekuwa inalipa, wasingekimbilia uko.

  Na kama lengo ni kuwasaidia waTz kama Mutuz anavyodai. Basi dawa sio kuwa mwanasiasa. Kuna challenges nyingi sana hapa Tz ambazo yeye mwenyewe anazijua kutokana na experince ya ughaibuni. Kuwa mwanasiasa sio solution
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wengi baba zao walikuwa mafisadi sasa wanashindana jinsi ya kurithi ufisadi wa baba zao!! January ndio huyo mjomba kastaafu kamtengenezea njia kwa pesa za wakina Manji!!
   
 8. c

  collezione JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nimesikia kaka,

  Watoto wa wakubwa wa nchi hii wanataka kukimbilia siasa ili kukomboa nchi. Is this true?

  Mimi nilitegemea mambo makumbwa kutoka kwao na sio siasa.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu labsa nikufahamishe tu ya kwamba vijana wanaotka Ulaya au nje na kurudi nyumbani ni asilimia chini ya moja wanajiingiza ktk siasa.
  Wengi wao wameajiriwa ama kufungua mashirika yao binafsi kwa hiyo sisi wanajamii hasa ktk ukumbi huu tunatakiwa sana kuwapongeza na kikubwa zaidi kuwaelekeza siasa za Bongo na hali halisi iliyopo.

  Tatizo kubwa naloliona kwa vijana hawa ni pale wanapojaribu kurekebisha vitu ndani ya msafara wa mamba.

  Nachowashauri wachuke muda kusoma alama za wakati, watu na Mazingira yanayohusiana na sehemu wanazotaka kuingia.
  Siasa za bongo ni unafiki na uchawi mwingi sijui kama watafanikiwa bila wao kupitia nyayo hizo hizo!
   
 10. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Moja Kati ya dalili za Ujinga ni kumchagua kiongozi Mtu asiyekua miongoni mwenu.(mtalii). Ni sawa na kuwa na kapteni wa timu Mtu ambaye hamfanyi nae mazoezi. Hawa watalii kutoka mijini na Newyork imefika wakati wa Kuwakataa kwa nguvu.
   
 11. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Viongozi kurithisha watoto wao madaraka sio sawa hata kidogo; kwani kuna ulazima gani? hakuna wengine wenye uwezo zaidi ya wao? I hate it bull shit!
   
 12. c

  collezione JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hiyo ndo mbaya zaidi, isije pakachimbika mbeleni kila mtu atapotaka kuwa mwanasiasa
   
 13. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 516
  Trophy Points: 280
  Ukombozi wa watanzania maskini na walalahoi utatokana na maskini na walalahoi wenyewe. Watoto wa vigogo hawana jipya zaidi kwani wazazi wao walilewa na wanaendelea na ulevi wa madaraka kwa kujipendelea wenyewe, na matokeo yake ni kushuka kwa ubora wa huduma katika taasisi za jamii kama shule, hospitali n.k.
  Wameamua kujiuzia nyumba za serikali, hadi walizojenga wakoloni kwa sababu tu ya ubinafsi na ulevi wa madaraka. Je hawa watoto wanaweza kuwa na mawazo ya kupinga mfumo unaowapendelea na kuwanyonya walalahoi?
  Kama wazazi wao ambao walianza maisha kwa ugumu na wanajua hali halisi ya watanzania walio wengi lakini bado wameasi misingi ya ukombozi kwa wote, itakuwaje kwa watoto waliozaliwa na kukuzwa katika mazingira yasiyo na shida?
  Je hawa watoto wa vigogo wanajua kwamba wenzao walalahoi wanaenda shule bila kunywa chai?
  Wanajua adha ya kukaa chini kwa kukosa madawati?
  Wanajua adha ya kukosa karo ya shule, uniform, nauli n.k?
  Wanajua adha ya kukosa dawa hospitalini?
  Wanajua adha ya kukosa umeme, mafuta ya taa kupanda bei n.k?

  Tunapaswa kujiuliza, utawezaje kutatua matatizo ambayo huyajui?
  Sana sana hawa watoto wa vigogo wanatakiwa kuhudumia jamii kwa njia nyingine mbadala wa siasa kama kweli wanaipenda jamii ya watanzania.
   
 14. mwanamke shujaa

  mwanamke shujaa Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uyoo jamaa Hana jipyaa babaake alishindwa
  kuwasaidia watz ye ataweza achanganye
  makongoro yake ****...........
   
 15. c

  collezione JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ni kweli unayosema,

  Wazo langu ni kwamba, hawa jamaa watumie njia nyingine ya ukombozi na sio kisingizio cha kuwa mwanasiasa. Kama kweli wana moyo wa kusaidia watu.
   
 16. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Le Mutuz Ze Big Show@ Dodoma!
   
 17. D

  Deo JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mengine yote ni safi sana Naunga mkono hoja

  Lakini baba hapo kwenye red! Yaani hakuna statement mbovu na iliyoniudhi kama hiyo, na hasa inapotoka kwenye kinywa cha Willy.
  Yaani anasikiliza kero?Kusikiliza! Kutoka kwa nani. Yaani hajui? Kutoka US siyo kuwa umetoka sayari nyingine kiasi cha kusahau ulikotoka. Au anataka kusema kuwa hajui mpaka aambiwe? Angekuwa anafanya utafiti namna bora ya kutatua matatizo ya wananchi ningemwona wa maana. Kusikiliza? I have a very low esteem on people with such statements.

  Pili collezione usidanganyike na hawa watu wanaotoka ughaibuni, mara nyingi hakuna lolote kabisa. Ni sawa na mtu wa kijijini kama mimi na bibi yangu tunavyodanganywa na watu walioko mijini. Wanakuja na nguo nzuri, perfume na hata dawa ya meno inatuzengua, tunawachinjia kuku, mbuzi na tunaamini hawali vitu dhaifu kama vya kwetu kijijini. Fika uone anakoishi, utalia na kuona aibu. hali ni hiyo hiyo kwa wanaotoka ughaibuni. Nafuu sana wanaosoma, lakini kwa wengine! Mh! Fahamu kuwa hawa wenzetu ni wabaguzi na wanasystem imara ya kupeana kazi, mgeni anaishia kwenye kazi za kibarua kama kusafisha madanguro nk.

  Ujenzi wa taifa au hata kusidia wananchi kila mmoja anaweza bora atimize wajibu wake.
   
 18. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawa majamaa wanaojiita watoto wa vigogo wasituzengue na tusiwavumilie kamwa. Hawana jipya tofauti na mawazo ya kifisadi.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu sijui mila na desturi za kwenu zinasema nini lakini kwetu hakuna hazina kubwa kwa mwanadamu kama kuwa msikivu.. Mtu unayependa kusikiliza WATU zaidi ya wewe kuongea kama mjuzi wa shida zao. Kwa mfano wapo viongozi kibao huja hapa JF kusikiliza kero zetu, kina Marehemu Regia alifikia hadi kukusanya kero zetu na zoezi hilo linaendelea, hawa sii wajinga bali wanatumia busara kubwa sana kusikiliza kero za wananchi kupitia mtandao,Kuwa kiongozi nchini haina maana unayajua yanayo wakera wananchi... Acha wananchi hata mkeo/bwana nyumbani kwako huwezi kujua kero zake ikiwa hutachukua muda na kumsikiliza, kumuuliza na na kwa ujumla wake Kuongea kwa pamoja..

  Willy ni kijana alopata bahati ya kujuana na watu na pia mtoto wa Malecela hakutaka yeye iwe hivyo lakini ndivyo Mwenyezi Mungu mjuzi wa yote alivyopanga na leo hii kaweza kumfikisha kule ulikoshindwa wewe unayeishi miaka yote hapo Bongo kisha mnaanza mizengwe. Kama unachukia sana basi angalau fanya wewe basi kile unachokiona ni bora zaidi kuliko kumpiga vita mtu kwa sababu tu katoka Ulaya.. na sidhani hata unalo moja la kuonyesha. Na mkuu wangu yaani umeonyesha wivu wa ajabu kabisa kuhusiana na watu wanaotoka Nje..Nadhani unamhitaji Jesus maana hiyo chuki ya hata kutazama mavazi yao wanavyonukia ikakukera ni hatari sana kwa hata maisha yako..
   
 20. f

  frontline1 Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  itakua vyema kama tungepata wasifu wa kijana wa malechela tangu azaliwe mpaka hapo alipo, utendaji wake na hisia zake dhidi ya wa tz.

  waweza kuwa mtoto wa kigogo but ukawa msaada kwa wa tz kwa namna nyingi, ingekuwa vyema kama kijana wa malechela angetumia muda wake kujipanga kutumi rasilimali alizo nazo na za wazazi wake kuwekeza kwao na ifikapo 2015 akapitia kwenye mchakatoi sahihi akagombea.
   
Loading...