Waraka kutoka kwa Bob.C. Wangwe kuhusu Rais mstaafu Ally.H. Mwinyi

Eng Nyahucho

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
688
1,148
MWL. NYERERE KWENYE KITABU CHA 'UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA' !

----------------------------------------------------------

Julai 18, 2017

"Awali viongozi wa chama wameanza kampeni za kutaka Rais Mwinyi aongezewe vipindi vya muda wa kuwa Rais. Nilipotambua hivyo nilikuwa nimekwenda kwa Rais mara moja na kumhsihi azizime mara moja kampeni hizo; na viongozi wahusika nilitafuta nafasi nao nikawaomba wasilifufue jambo hili. Nikadhani tumeelewana hivyo.

Kwahiyo nilishituka niliposikia kuwa kumbe suala hilo la vipindi vya urais bado linazungumzwa, ati bado uamuzi wa vipindi vingapi haujafikiwa!

Kwahiyo nilirudia tena kueleza umuhimu wa kukubali kwamba suala hili tumekwisha kuliamua, na hatari ya kuanza kulizungumza upya.

Sababu ya kufanya muda ambao mtu yeyote anaweza kuwa Rais utamkwe na uwe ni sehemu ya katiba, ilikuwa ni kuutoa uamuzi huo mikononi mwa Rais mwenyewe, au kikundi chochote cha chama au dola. Si uwamuzi mwepesi, kwa Rais wala washauri wake.

Plato, Myunani wa kale, alipendekeza kuwa wanafalsafa ndio wanafaa kuwa watawala wa nchi, maana wanasifa mbili muhimu: kwanza, wana uwezo wa kutawala na pili hawapendi kutawala.

Kwahiyo, Jamuhuri ya Plato ilikuwa na sheria ya kuwalazimisha wanafalsafa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikiisha, atafurahi sana kurudia kazi zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazipenda.

Lakini nchi zetu hazitawaliwi na wanafalsafa wa Plato; watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala hata kama hawana uwezo wa kutawala, na wakisha chaguliwa hawatoki kabisa bila kulazimishwa. Si busara kuwaachia wao wenyewe ndio wawe waamuzi wa lini waache kuwa watawala.

Lakini hata kwa viongozi wanaotambua kuwa uongozi ni wajibu, na ukisha timiza wajibu wako ni vizuri kuondoka, si rahisi kuamua kama wajibu wako ni kuondoka au kuendelea.

Na sababu za kusita zinaweza zikawa nzuri kabisa. Na katika hali halisi ni vigumu zaidi washauri wa Rais kumwambia kuwa amekwisha kutimiza wajibu wake na kwa maoni yao inafaa aondoke, amuachie mtu mwingine.

Wao wanazo sababu nyingi zaidi, nzuri na mbaya, za kumtaka aendelee, na watamshauri hivyo. Kwahiyo, ni jambo la busara kabisa uamuzi wa muda wa kuwa Rais ufanywe mara moja, na ukisha kufanywa, uwe ni sehemu ya katiba ya nchi na uheshimiwe.

Na hivyo ndivyo tulivyofanya. Suala hili lilikwisha kuamuliwa zamani na sasa ni sehemu ya katiba yetu. Uamuzi huo unafaa uheshimiwe.

Rais Mwinyi ndiye Rais wa kwanza kuchaguliwa kwa mujibu wa katiba hiyo. Yeye akisema kuwa vipindi viwili havitoshi na akataka viwe vitatu; Rais wa pili atasema vipindi vitatu havitoshi na atataka viwe vinne; na kadhalika na kadhalika mpaka tufike Ngwazi wa Tanzania. Hilo si jambo la kuzungumzwa, na limefanyiwa uamuzi wa mwisho."

Mytake:
Ni wazi kuwa Rais Mwinyi aliteleza kutoa mawazo ya aina ile ya kutaka Rais Magufuli aongoze milele. Hii inaonesha kabisa, vugu vugu la kutaka aendelee kuwa madarakani wakati ule aliliasisi yeye, na isingekuwa Mwl Nyerere kuingilia kati, angejiongezea muda wa kuongoza licha ya kuwa pendekezo la tume ya Mark Bomani la vipindi viwili lilikuwa na baraka za chama chake.

Wapo wenye mawazo ya aina hii na wengine wameyasema hadharani, lakini wengi tuliwapuuza kwa kuamini kabisa wako sahihi kwasababu ni wajinga wa historia ya nchi yetu.

Ni muhimu wenye mawazo haya wakayahifadhi kwasababu nchi hii tumetoka siku nyingi kwenye zama hizo.

Viongozi wetu wakate mawazo ya hovyo bila kujali yanatoka kwa nani. Wafuate matamanio ya Kansela wa Ujerumani Bi Angela Kasner Merkel aliyepata kusema "I don't want to be a half-dead wreck when I leave politics".

Tuheshimu katiba yetu na tuheshimu historia yetu na nyakati zetu ili hata viongozi tunaopenda waendelee kuongoza vizuri ili wasiwe na mwisho mbaya.
 
Mwinyi alisema nanukuu " Kama Katiba isingeweka ukomo wa Vipindi, basi Ningependa JPM atawale milele".

Mwinyi katika kauli yake kaonyesha kuwa kuna katiba inayoweka kizingiti, Kwa hiyo msimuonee mzee wa watu!!. Hakuna mahali aliposema katiba ibadirishwe!!
 
Mwinyi alisema nanukuu " Kama Katiba isingeweka ukomo wa Vipindi, basi Ningependa JPM atawale milele".

Mwinyi katika kauli yake kaonyesha kuwa kuna katiba inayoweka kizingiti, Kwa hiyo msimuonee mzee wa watu!!. Hakuna mahali aliposema katiba ibadirishwe!!
Mkuu huwa wana anza hivyo hivyo. Yaani yeye anasema katiba ni kikwazo, anakuja mwingine anasema kama katiba ni kikwazo kwa nini isibadilishwe? Angeweza kumsifu bila kutupeleka huko.
 
Mkuu huwa wana anza hivyo hivyo. Yaani yeye anasema katiba ni kikwazo, anakuja mwingine anasema kama katiba ni kikwazo kwa nini isibadilishwe? Angeweza kumsifu bila kutupeleka huko.

Nyerere mwenyewe tunayemnukuu yeye binafsi hakujiwekea kizingiti cha term limits, lakini angalia hapo anavyomtaka mwenzie aviheshimu!!
 
Mwinyi alisema nanukuu " Kama Katiba isingeweka ukomo wa Vipindi, basi Ningependa JPM atawale milele".

Mwinyi katika kauli yake kaonyesha kuwa kuna katiba inayoweka kizingiti, Kwa hiyo msimuonee mzee wa watu!!. Hakuna mahali aliposema katiba ibadirishwe!!
Kiswahili chenyewe shida ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom