Huyu anayejiita Mzee wa Upako simfahamu vizuri hivyo siwezi kuchangia lolote kuhusu upeo wake, ingawa 'Mchukia Fisadi' amedokeza kwamba tatizo lake kubwa ni kwamba hana elimu. Tutamsamehe kwa hilo. Lakini Makwaia wa Kuhenga namfahamu fika! Huyu ni mwandishi wa habari wa siku nyingi. Ila ana chuki sana na Kanisa Katoliki. Sijui ni kwa nini! Ila namuonya iwapo ataendeleza chuki hiyo nitashusha tuhuma zake nzito kuhusu mwenendo wake unaotia shaka.