Wapuuzeni wanaodai CCM haijafanya kitu

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
Watanzania wapuuzeni wapinzani wanaodai kwamba Serikali ya Chama Cha Mapinduzi haijafanya maendeleo yoyote , wapinzani hao wanawapotosha na kuwadanganya wananchi hali ya kuwa wananchi wenyewe ni mashahidi wa jinsi nchi inavyopiga hatua ya kimaendeleo siku baada ya siku.

Nashangazwa na watu hao wanaosema hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana wakati wanatembea katika barabara za nzuri za lami zilizojengwa na CCM, wanakunywa maji yaliyoletwa na CCM wanatumia nishati ya umeme ulioletwa na CCM na hata wakiumwa wanapata matibabu kwenye hospital zilizojengwa na CCM.

Siku hizi vijiji vingi vina huduma ya Maji na Umeme wa REA ,Hospitali na Vituo vya Afya na Zahanati, Mashule kila kona, Wanafunzi wanasoma bure , Mikopo ya Elimu ya
Juu inatolewa, Viwanda vinajengwa, Vijana na Wanawake wanakopeshwa fedha na Serikali ya CCM, Wazee juu ya miaka 60 wanatibiwa bure katika Hospitali za Serikali, Wakulima wanapewa ruzuku za pembejeo za kilimo, kwa mara ya kwanza CCM inajenga reli ya kisasa ya kimataifa itakayotumiwa ns treni ya umeme, Mtandao wa barabara za lami umepanuka hivyo sio jambo la kiungwana kwa mtu kudai kwamba hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi

Ni ukweli kwamba maendeleo ya mwanadamu hayana mwisho. Hata Tanzania ikifanikiwa kwa kiwango kikubwa kiasi gani, bado hayo hayatakua maendeleo ya mwisho, yaani maendeleo ya juu kabisa.

Kila hatua katika maendeleo ya mwanadamu, huvutia hatua nyingine tena na huendelea hivyo hadi mwisho wa maisha yetu ambapo hujitokeza vizazi vingine na kuendeleza pale tulipoishia.

Kutokana na msingi huo, ndio maana hata nchi zilizoendelea sana duniani, hazijawahi kufika mahali zikaridhika na maendeleo yake bali kila Siku Serikali zao zinajitahidi kupasua vichwa kuona ni vipi wafanye ili waweze kuendelea zaidi.

Ni jambo la wazi kuwa mambo mengi mazuri ambayo yana manufaa makubwa kwa taifa letu na yamefanywa na Chama Cha Mapinduzi hivyo kinafaa kuungwa mkono na wananchi wote.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) bado hakijabadilisha asili ya kuanzishwa kwake ambayo ni kuwa chama cha kijamaa kinachojishughulisha na kutatua shida za watu na hivyo kitaendelea kuweka juhudi ili kutatua kero na kuleta maendeleo kwa wananchi kwa wakati husika na kwa kulingana na mahitaji ya kipindi hiko.

Wasalaam,
Augustino Chiwinga.
0659438889.
 
Hizo barabara ziko wapi, maji yako wapi? . hapa dar capita city bado watu wanakunywa maji ya dimbwi, mvua za juzi zimetuonyesha tulivyo bado sana kimiubdombinu na mipango miji. we kwa exposure yako ndogo ndo unaona tumeendelea
 
Hivi toka 1961(1977) mpaka 2018 unategema kweli ccm ikose cha kufanya hata viwili vitatu. Swali sasa tujiulize je hivyo walivyofanya vinakidhi!? Vinaendana na muda.

Haiwezekani uamke toka alfajiri upike chai tu, halafu ujinasibu kuwa umefanya kazi, hali ya kuwa vyombo vichafu, nguo chafu, nyumba chafu, kuna mahitaji ya ndani hujaenda kununua, halafu ujidai umetenda kazi, huu ni upopoma wa ISO
 
CCM hawajafanya kitu? Wamefanya saaaana aiseee, tena Sana tu. Mifano ipo mingi, Uuaji wa Viwanda, mfano Tanga Viwanda vyote vikubwa havipo tena, Mfano mwingine, ununuzi wa vitu feki kama Ndege, vivuko n.k, kwenye sekta ya Rushwa hapo ndio nyumbani kwao, EPA, na ndugu zake!! Ujenzi sasa wa substandard roads!!

Halafu mpuuzi mmoja Anasema CCM hawajafanya kitu? Kweli? Hata kubadilisha mfumo wetu wa Elimu hatujaona? Expansion joint huzijui wewe?? Hivi isingekua CCM ungejulia wapi Kuwa Jangwani ppangeweza kugeuzwa stand kuu Ya UDART huku ukiwaondosha wenyeji kwa nguvu ukidai Unataka kuokoa maisha yao na wakati huo huo ukienda kujenga hapo hapo??

CCM mmmmmmgggh Wamefanya mengi Sana aiseee, Umesahau hata bomba la gesi au kesi?? Liliondoka na nafsi ngapi?? Hahahahaa good job, keep it up CCM. Go CCM, go gooo
 
Kwa jinsi unavyotokwa povu ni wazi unajua ukweli kuwa CCM ni failure material. In such a case, challenge yenu kubwa ni kuhakikisha bajeti iwe trillioni hamsini na iwe ni cash, ili muone mwanga, other wise you just, just noisy neighbor
 
CCM hawajafanya kitu? Wamefanya saaaana aiseee, tena Sana tu. Mifano ipo mingi, Uuaji wa Viwanda, mfano Tanga Viwanda vyote vikubwa havipo tena, Mfano mwingine, ununuzi wa vitu feki kama Ndege, vivuko n.k, kwenye sekta ya Rushwa hapo ndio nyumbani kwao, EPA, na ndugu zake!! Ujenzi sasa wa substandard roads!!

Halafu mpuuzi mmoja Anasema CCM hawajafanya kitu? Kweli? Hata kubadilisha mfumo wetu wa Elimu hatujaona? Expansion joint huzijui wewe?? Hivi isingekua CCM ungejulia wapi Kuwa Jangwani ppangeweza kugeuzwa stand kuu Ya UDART huku ukiwaondosha wenyeji kwa nguvu ukidai Unataka kuokoa maisha yao na wakati huo huo ukienda kujenga hapo hapo??

CCM mmmmmmgggh Wamefanya mengi Sana aiseee, Umesahau hata bomba la gesi au kesi?? Liliondoka na nafsi ngapi?? Hahahahaa good job, keep it up CCM. Go CCM, go gooo
Acha kujitoa ufahamu,ratio ya mafanikio ni 30% which means ccm ni failure material.
 
Kwa nini kutumia nguvu kuyaelezea? Kama yamefanyika kweli si wananchi wanayaona nini wasiwasi mwingiii
 
Mleta mada muda wote uliotumia kuandika 'hizi kero' ungetumia kumsaidia mkeo (kama huna mke basi hawara yako) kwenda kuchota maji ungekuwa umefanya jambo la maana sana kuliko upuuzi huu. Dar yenyewe zaidi ya asilimia 60 hawana maji!
 
Matatizo ni yale yale ya tangu uhuru, ni miaka zaidi ya 50, hamjatatua hata moja. Halafu eti mnasema mmefanya kitu.

Ukilinganisha muda ambao CCM imekuwa madarakani na kilichofanyika ni sawa na haijafanya kitu. Kwenye wizi na ufisadi ndio CCM imefanikiwa sana, na sasa mmeweka rekodi mpya ya wizi wa 1.5Trilion kwa mkupuo.
 
ccm hoyeee....
20180506_163813.jpg
 
CCM ilitumia pesa zake kutoka kwenye miradi yake au ilitumia pesa toka kodi za wananchi kujenga hivyo ulivyovitaja?
 
hebu kabla ya yote tujilinganishe ba wale tuliopata nao uhuru pamoja km malaysia, korea, na china wenzetu wamefikia wapi kiuchumi na sisi tuko wapi?

unazungumzia kuhusu barabara ambazo karibia 80% zimejengwa kwa mikopo ambao watoto na wajukuu zetu watakuja kuteseka kulipa licha ya rasilimali kibao tulizonazo

elimu nayo ipo hoi hta tatizo la madawati tumeshindwa kulimaliza!

vipi kuhusu walimu? wanadai malimbikizo mpaka washakata tamaa, mazingira ya kufanyia kazi yapo ovyo morali yao imeporomoka ikichangiwa na mishahara midogo

maji bado ni janga la taifa

sekta ya afya nayo ipo hoi licha ya serikali kutukata kodi lkn gharama za matibabu still zipo juu sana

kwa kifupi km ni mtihani ccm nawapa 20% wamefeli kbsa
 
CCM hawajafanya kitu? Wamefanya saaaana aiseee, tena Sana tu. Mifano ipo mingi, Uuaji wa Viwanda, mfano Tanga Viwanda vyote vikubwa havipo tena, Mfano mwingine, ununuzi wa vitu feki kama Ndege, vivuko n.k, kwenye sekta ya Rushwa hapo ndio nyumbani kwao, EPA, na ndugu zake!! Ujenzi sasa wa substandard roads!!

Halafu mpuuzi mmoja Anasema CCM hawajafanya kitu? Kweli? Hata kubadilisha mfumo wetu wa Elimu hatujaona? Expansion joint huzijui wewe?? Hivi isingekua CCM ungejulia wapi Kuwa Jangwani ppangeweza kugeuzwa stand kuu Ya UDART huku ukiwaondosha wenyeji kwa nguvu ukidai Unataka kuokoa maisha yao na wakati huo huo ukienda kujenga hapo hapo??

CCM mmmmmmgggh Wamefanya mengi Sana aiseee, Umesahau hata bomba la gesi au kesi?? Liliondoka na nafsi ngapi?? Hahahahaa good job, keep it up CCM. Go CCM, go gooo
Nimeipenda hii, ufafanuzi mzuri sana wa juhudi zilizofanywa na ccm kwa kipindi kirefu.
Ni sawa na mtoto aliyeshika nafasi ya mwisho darasani anayejinasifu kuwa ni namba moja kutokea mwisho na yeye na wazazi wake wanatembea kifua mbele kwa mafanikio hayo.
Ccm hoyee!
 
Back
Top Bottom