Wapotea msafara wa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapotea msafara wa JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TIQO, Mar 23, 2012.

 1. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,836
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  baadhi ya magari yaliyokuwa katika msafara wa rais Kikwete leo yakielekea uwanja wa ndege Nduli


  [​IMG]
  [​IMG]
  WIKI ya maji yamalizika kwa kituko cha mwaka mkoani Iringa baada ya viongozi waliokuwa katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete kupotea mjini Iringa.

  Tukio hilo limetokea Leo majira ya 9.30 alasiri baada ya viongozi hao kutoka katika chakula cha mchana na Rais Kikwete katika ukumbi wa St Dominic ulipo eneo la RETCO kata ya Gangilonga.

  Viongozi hao wakiwemo viongozi wa Manispaa ya Iringa pamoja na wale wa kitaifa waliofika katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa ,Sherehe zilizofanyika mkoani Iringa walijikuta wakipotea badala ya kuelekea Ikulu wao walielekea uwanja wa Ndege Nduli nankulazimika kugeuza .

  Mbali ya viongozi hao kupotea pia askari polisi wa FFU na wanahabari waliokuwemo msafara huo nao walijikuta wakipotezwa na viongozi hao baada ya kuelekea uwanja wa Ndege Nduli na kugeuza eneo la FM Abri na kuelekea Ikulu.

  Mmoja kati ya viongozi waliokuwemo katika msafara huo alisema kuwa kupotezana kwa viongozi hao katika msafara huo ni kutokana na magari kugawanyika kwa yale ya Manispaa ya Iringa kuelekea uwanja wa Nduli na msafara wa Kikwete kuelekea Ikulu na askari aliyekuwepo eneo hilo kushindwa kujua magari yanayokwenda Ikulu ni yapi na yanayokwenda uwanja wa Ndege kabla ya Rais ni yapi.

  Mwandishi wa habari hizi ambaye pia alikuwemo katika msafara huo alishuhudia kupotezana huko kwa magari hayo yaliyokuwemo katika msafara wa Rais Kikwete huku baada ya magari yakilazimika kupita njia za vichochoroni ili kutokea Ikulu kuungana na msafara wa Rais Kikwete ambaye alikwenda Ikulu ndogo ya mkoa wa Iringa kwa mapumziko mafupi.

  Source:
  http://www.francisgodwin.blogspot.com/
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,836
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Hawa mafisadi walivimbiwa pilau na ulanzi wakawa na kiherehere kukimbilia nduli badala ya Ikulu ndogo
   
 3. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,148
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hahahahaaa!!!
  Kwamba walipiga Mdindifu wakataka kwenda Kihesa gesti hausi au?
   
 4. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,096
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Au mjomba alikuwa anataka kupaa majuu!? Si unajua tena mambo ya airport?
   
 5. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,176
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Wana maruweruwe ya usaliti kwa wananchi wao!
   
 6. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,836
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Jamaa waligida mdindifu na pilau wakasahau jukumu lao la kumshangilia rais wao wakawa wanakimbilia Nduli
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kwani nini hawakufahamishwa ratiba ya mkuu wao?
   
 8. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,094
  Likes Received: 398
  Trophy Points: 180
  wangepotea hata wakianguka na ndege hawana faida ..mabolizozo tu qmmae zao
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,114
  Likes Received: 2,216
  Trophy Points: 280
  Wapoteee tu wanatulia kodi zetu hao!
   
 10. Jambazi

  Jambazi JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2016
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 11,893
  Likes Received: 8,561
  Trophy Points: 280
  Mbona magari ni mengi sana!
   
Loading...