Wapo wenye kumuelewa Magufuli, hebu tuwasikilize na wao

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
".........Kwa kweli nashukuru Mungu kutuletea Magufuli.
Unajua hawa mabwana walikuwa wanatufanyisha kazi kama vibarua na kulikuwa hakuna muda maalum wa kazi wala ujira unaoeleweka! Ila nashukuru kuanzia January walikuja maofisa wa serikali Mara mbili na kumuamuru boss wetu atupe mikataba, tuwe na mshahara unaojulikana na tuwe na NSSF, na overtime tulipwe kama tutafanya kazi zaidi ya saa 12 ...."

Hayo ni maneno ya kijana mmoja muosha magari katika moja ya petrol station jijini, ambaye anafurahia neema wanazozipata sasa kwa kuwa na ndoto mpya kabisa ambazo hakuwahi kuzipata maisha yake yote.

Baada ya mazungumzo na huyu mtu mmoja wa aina hii nikajua kwamba katika hizi social media labda ni group la watu wa level fulani tu ndio tunaoongea sana, labda kwa kuwa ndio tumeumizwa na huyu bwana mkuu.

Yawezekana maisha yasiwe mepesi kwetu sote (nchi nzima) Ila hicho si kigezo cha kumlaumu raisi. Labda tunaumia kweli lakini si kwa ubaya wa boss mkuu ila inawezekana wengi tulikuwa na njia zisizo rasmi kuendesha maisha yetu, hivyo kurudi kwenye haki ndio shida kuu kwetu! Hapa tutakuwa tunaumizwa na zile methali za kiswahili tu: MZOEA VYA KUNYONGA.....
 
Utetexi kwa Magu umekuwa mkubwa sana! Sincerely, Magufuli ameattract criticism mapema mno!
Unajua kuna cohort tofauti ktk jamii, hii yetu ya JF ni ile ya middle na upper class lakini ktk forums tofauti wapo wanaoona raisi anawapendeza sana!
Mimi mtumishi wa umma nitapenda nini kwa hivi ninavyobanwa?
Lakini wapo waliokuwa wakinyonywa na makabaila wanaona malaika amewashukia!
Critism ni za kawaida kwa politicians/kiongozi! Na hii ni one aspect Mimi naisifia lkn zipo angle nadhani hafanyi vema, haiwezakani raisi akae madarakani hasifanye lolote, huu utulivu uliopo tu ni sehemu ya kazi za raisi! Hata huoni kitu chochote huko kutoona jambo ni jambo jema la raisi, maana watu kama Syria , Congo, Burundi wanaishi walivyo kama mshahara wa matatizo ya viongozi wao!
 
Back
Top Bottom