Wapo wazee wanachuma laana ya Taifa awamu hii

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Wapo watu walikuwa wanafanya shughuli zao za ualimu wa chuo na kazi nyingine na walikuwa wanaishi na kuzungumza ukweli wakilitetea Taifa letu,Hadi 2015 endapo MWENYENZI MUNGU angewachukua wangeondoka bila laana ya maamuzi juu ya Taifa letu.

Baada walipoteuliwa wakaona maisha yamebadilika na wanaishi kwenye makazi Bora,wanalipwa vyema, wanabebwa na kukalishwa viti vya mbele kila waendako na kikubwa zaidi wamevaa uheshimiwa. Pamoja na vyote hivi walivyopewa wamenyang'anywa kitu kikubwa zaidi maishani mwao ,wameporwa amani yao, wamerwa haki, wameporwa kusema ukweli na wamevaa ngozi ngumu ya kuamua mabaya na mazuri kwa wake au waume zao,watoto na ndugu jamaa zao.

Kupitia vikao halali vya vyama, serikali na Bunge tumeshuhudia maamuzi ambayo ni mazuri ila yapo maamuzi ambayo ni mabaya kwa kesho ya Tanzania.

Vikao hivi vimewapa waalimu na watendaji wengine waliokuwa wasafi 2015 kutoa maamuzi ya kuitengenezea migogoro,uadui na uasama nchi yetu. Kukubali kwao mashangingi na kukaa viti vya mbele karamuni kumewapa pia masharti ya kutulipa ubaya waajiri wao. Kukaa kwako mbele karamuni kumefanya wasishauri vyema kuhusu Tanzania Bali washauri vyema kuhusu kesho ya chama Cha siasa.

Wamesau Tanzania inaweza kuwepo bila vyama vya siasa ila vyama vya siasa haviwezi kuwepo bila Tanzania. Wamesau kuwa wao wanaweza wasiwepo kesho ila Tanzania itaendelea kuwepo milele, wamesau kwamba Tanzania salama ni kwaajili ya vizazi vyao na si kwaajili yao, wamesau kwamba hata wanayemsikiliza na kumkalia kimya akilipeleka Taifa mrama ipo siku atakaa kwake akisubiri kuongozwa lakini pia ipo siku atarejea mavumbini.

Niwakumbushe, waliotangulia wangeharibu hii nchi kwa kasi wanayoiribu Leo wao wao wasingeweza kuongoza.

MAENDELEO yenye watu ni Jambo kubwa kuliko MAENDELEO yenye mtu, siku akiondoka huyo mtu watu watayavuruga na kutafuta MAENDELEO yao.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Walaniwe na wafe vifo vya mateso makubwa!

Sijui hawa watu huwa wanafuata nini katika madhabau ya bwana ili hali wanatenda uovu repeatedly tena bila kujutia.
 
Back
Top Bottom