Wapo Wanawake wanajiheshimu na kuheshimu ndoa zao..... Huyu ni mmoja wao

Hongera sana Bwana Gerrad kwa kupata mke mwema. Naamini kua na wewe ni mume mwema pia sababu mume mjinga anaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuharibu ndoa pia.
Mara nyingi napenda kukumbushia kua wenye kuleta habari hapa sio representative sample. Ni sawa na kwenda kukaa gate ya hospitali alafu useme kumbe watu wengi duniani wanaumwa...
Asante kwa story yako.
Ukisoma vizuri hapo juu nimeeleza kuwa sredi nyingi hapa za malalamiko na manung'uniko ambazo nyingi zinatoka kwa sisi wanaume ni one sided..... Wanaume wengi tunajenga nyumba za tope ambazo hubomolew na wake zao
 
Gerrard,asante sana kwa thread yako,imeangalia na kuainisha pande zote zinazohusika na ndoa yaani mke na mume na kwamba ina discourage assumptions kwamba si kila ndoa ni mbaya.Tumezaliwa kuja kuujaza ulimwengu,kwa kufuata mafunzo ya either dini zetu ni kwamba lazima tuoe pengine ili tusitende dhambi ya kuzini kwa sababu ni either uoe,u-abstain au utende dhambi.Na kwa mila zetu za kiafrika inabidi tuoe hata kama humu kwenye javi tutasema wanandoa wa kiume wanaongoza kwa nyumba ndogo,wanandoa wa kike wanaongonza kwa serengeti boys au wanandoa wanagombana kila siku hata wanandoa wa kiume wanarudi majumbani saa tisa usiku.Watu wataoana tu kwa sababu ni imani,ni mila,na hata pia ni desturi na utaratibu.
Lakini usichukulie juu juu kwamba kama RUSSIANROULLETE alivyosema kwamba usiende kwenye geti la hospital ukaona wingi wa watu hospitalin ukazani kila mtu hapa duniani ni mgonjwa.Na usichukulie sample moja ya kwako basi ukasema kwamba wakwako pamoja na kukuzidi kipato,pamoja na mazuri yote aliyokutendea kwamba basi mpira umeshavuka goal line kuwa goli.Miaka sita na minne ya uchumba tu,bado safari ndefu,mshukuru mungu wako kila siku unayoisha ukiwa hivyo kwani hujafa hujaumbika waswahili wanasema.Kama kusema tungeweza basi siku ya kuingia kabulini ndio siku ya kusema asante mungu kwani ulinipa mke/mme mwema.
Huwa tunabadilika,am talking through experience.Ten yrs ya relationship ya seconday and college,ten yrs of marriege mkiwa hamna kitu,two lovely kids and at last god open up everything in your life,lakini ndoa inaanguka beyond repair.Na mungu wenu mmemtanguliza kwa kila kitu mnachofanya lakini shetani yuko nyuma anasubiri nafasi yake.I think we live sometimes to make history.Nice weekend guys,kumbuka tusio oa tusiache kwa sababu javini kuna story,tulio oa to make effort ndoa zisiangukie kwenye mikono ya shetani,tulio kwenye matatizonina ndoa mwangalie shetani aweza kuwa begani kwa hiyo haraka tubu kuokoa ndoa yako
Uko sawa sawia Mkuu.... Jambo la msingi ni kumwomba Mungu huku tukimkataa shetani na kazi zake zote.... Nilikuwa najaribu kutoa upande wa pili wa shilingi baada ya jukwaa kujaa habari za malalamiko kila siku dhidi ya ndoa
 
Hongera sana Gerald, mshukuru MUNGU kwa kukupatia mke mwema na endelea kumwomba MUNGU aendelee kukusaidia msijebadilika.

Ila tu napenda kukukumbusha kuwa kwa sasa hivi si kila mwanamke avunjae ndoa yake ni mpumbavu... Na pia si ndoa zote zinavunjwa na wanawake tu.
Hope unakubaliana na mimi kwamba zinavunjwa na wanandoa wenyewe. Otherwise thanks kwa angalizo zuri
 
wanawake wana udhaifu, sawa tunakubali
huo udhaifu wanaufanya na nani?

Rais.
Uko vere close na what I wanted to say yaani wanawake wema wapo lakini kimaumbile wanawake wana udhaifu fulani na hawataki kuukubali. Hapo sasa ndio maana naweka dots ................................. kwasababu ukiwapa ukweli wanaona unawadhalilisha
 
wanawake wana udhaifu, sawa tunakubali
huo udhaifu wanaufanya na nani?
Huo udhaifu unakuwa triggered na wanaume baada ya kuwa exposed na wanawake.
Dont go too deep kongosho wadada watakuja juu na nitapoteza tuzo ya lawyer bora wa JF mwaka huu.
 
Watu bwana, zikiletwa thread za mke kacheat, mume ana nyumba ndogo, familia inesahaulika mnashabikia ila akija mtu kuelezea the positive side of ndoa from experience mnajitahidi kweli kumvunja moyo.

Gerrard hongera kwa kua na ndoa yenye upendo na amani mpaka wakati huu, kuna watu hata wiki hawamalizi. Muhimu wewe na mkeo wote mjitahidi kulea ndoa yenu.Msimsahau Mungu wenu either, shetani asije akawapitia maana hua anawapitia wengi kweli.
 
Haaaaaasaaaaa Madam nilikuwa nakusubiri wewe uje hapa. Ni ajabu sana kwamba watu wanapendelea thread za minyukano ya ndoa lakini wanapoambiwa upande wa pili hawaamini. Dunia imefikia pabaya sana Dada Lizy lakini tufanyeje sasa zaidi ya kumwomba Mungu? Nimetumia experience pia ya jamaa zangu wanaonizunguka kwamba kila siku ni vululu vululu lakini hata kwa miaka hiyo michache kwangu tumeishi kwa amani tele.... ile niliyoitarajia wakati naingia katika ndoa... napata kile nilichotarajia na nina hakika hata Mwenzangu naye anapata kile alichotarajia kukipata toka kwangu.
Nawasihi Jamaa zangu ndoa zilizotulia zipo, wanawake waliotulia wapo.... Wanaume waliotulia wapo..... tusiwe na sweeping statement kwamba ndoa ni jela au jehanam hayo sio makusudi ya Mungu bali ni ya shetani na kazi zake

Ubarikiwe sana Dada Lizy kwa mchango wako
 
Tunashukuru kwa ushuhuda Gerrald mungu awatie nguvu katika safari yenu ya ndoa ,ningependa pia kupata ushuhuda toka kwa wife kuhusu wewe kama na wewe ni mme mwema ama mkeo anakuvumilia tu Mbarikiwe sana
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Rais.
Uko vere close na what I wanted to say yaani wanawake wema wapo lakini kimaumbile wanawake wana udhaifu fulani na hawataki kuukubali. Hapo sasa ndio maana naweka dots ................................. kwasababu ukiwapa ukweli wanaona unawadhalilisha

my friend, hakuna binadamu asiye na udhaifu, wewe pia una udhaifu na udhaifu wako ni ...
 
Habari za ku elekea weekend Wana JF.

Imekuwa ni kawaida ya hapa JF hasa jukwaa pendwa la MMU kila siku kusikia lawama na manung'uniko miongoni mwa wanandoa hasa Wanaume wakiwalalamikia Wake au wachumba zao. Hii kwa kiasi fulani na kwa maoni yangu inaweza kuwaathiri Wanandoa wapya/watarajiwa kiasi kwamba mtu anaingia kwenye ndoa akiwa na attitude moja..... ndoa ni mateso, ugomvi, vurugu, usaliti na madhila mengine yanayofanana. Leo nimeona niwe miongoni mwa mashuhuda wa namna ndoa ilivyo tamu, raha, na ya amani hasa ukimpata mtu sahihi.
Mimi nimeoa, nina ndoa ya miaka 6 na mtoto mmoja. Kabla ya kufunga ndoa na Mke wangu tulikaa kama Wachumba kwa miaka Minne (4).
Naamini ni miongoni mwa watu hapa duniani ambaye nimebahatika kupata "Mke Mwema". Pamoja na Elimu yake ya kutosha tu, mshahara wake unaozidi wangu kama mara mbili na vitu vingine bado ndoa yetu imekuwa salama, tulivu na ya kufurahia kwa miaka yote tuliyoishi kama wana ndoa.

Kwa hulka ya Wanawake wa sasa hivi.... naamini ninaye Mke ambaye sijui ni sifa gani ambazo zinapungua ili aitwe Mke Mwema. Nawasihi Wanawake wengine hapa JF na kwingineko waelewe kuwa "Mke Mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe"

Wale ambao hawajaoa na kuolewa wasidhani kuwa ndoa ni misukosuko na vurugu kwani "mvunja ndoa ni mwana ndoa mwenyewe" na amini usiamini migogoro mingi inayoripotiwa hapa ni stori za upande mmoja tu yawezekana sisi wananume ni sehemu ya matatizo.

Mtaniwia radhi niliowakwaza lakini naamini nimetoa uzoefu wangu

Mkwe wako ndio huyo hapo juu? Kazi kweli kweli!
 
Tunashukuru kwa ushuhuda Gerrald mungu awatie nguvu katika safari yenu ya ndoa ,ningependa pia kupata ushuhuda toka kwa wife kuhusu wewe kama na wewe ni mme mwema ama mkeo anakuvumilia tu Mbarikiwe sana
Atakuja siku moja labda.... Kwani The One alitarajia kama Wife wake angekuja hapa kujibu mapigo? Other wise Senks!
 
nakubaliana na wewe haswaa
ndo mana mie sredi za kudumisha mahusiano huwa sichangii sana
uaminifu kwenye ndoa its a value
we dont learn values over one night
its a life time lesson
na darasa la kuanzia hilo ni kwenu
hapa tunajazana mastori ya town tu
ya kubeba hapa sijui??

kwa akina dada nipotezeeni hapa
mwanamke anafunzwa uaminifu kwao
hasa kwa tabia za mama yake
kama aliheshimu ndoa from heart, na mabinti tunajifunza hapo
kama alikuwa chakaramu chances za binti kuwa chakaramu ni kubwa mno
kadhalika na wanamme nadhani
maneno mazito haya ,incase alikuwa kicheche na akakiri alikuwa kicheche ila now hawezi kurudi nyuma...mafunzo ya mama yatakuwa yanahusika hapo.
 
nakuwa na wasiwasi, huyu si the one anajiliwaza baada ya mke kumwaga mboga.nukta
Kabla ya kufananisha watu uwe unafanya utafiti, The one alijiunga hapa lini na mimi niliingia JF lini otherwise mchango wako ni nonsense kabisaaaaaaaaa!!!!!!!!
 
Uaminifu ni value kama ilivyo dini
you either believe in uaminifu or not
kwa believers wa uamninifu
haijalishi eti partner wake ni mwaminifu or not
wao huwa ni waaminifu tu
sababu tabia mbaya ya mwingine haisababishi wewe usiamini unachoamini
kuwa kicheche inategemea sababu, labda alikuwa anakaa na partner anamwacha afu anatafuta mwingine
akaishia jikuta kajaza basi
lakini kwa mtu aliyekuwa anaweza kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja at per
usitegemee atabadilika
atapumzika tu
ukim-push to edges anacheat sana
kwa kisingizio mbona wewe una nyumba ndogo? Au una kidumu

kuna exceptional case ambao wana learn from bad experience wanabaki na ile picha ya uchungu na kuamua kuwa waaminifu
mfano mzazi cheater na mkatili
labda akasababisha tatizo kubwa home
labda maradhi kwa partner wake au kilema

i tell u you learn this at home
maneno mazito haya ,incase alikuwa kicheche na akakiri alikuwa kicheche ila now hawezi kurudi nyuma...mafunzo ya mama yatakuwa yanahusika hapo.
 
my friend, hakuna binadamu asiye na udhaifu, wewe pia una udhaifu na udhaifu wako ni ...

ha ha ha thats my FA, nakubaliana na post yako na yep nina mauzaifu kibao sio mmoja tu lakini udhaifu niliokuwa nauzungumzia mimi ni ule wa kimaumbile na ambao uko common somehow. In short wanawake wana udhaifu wao na pia wanaume wana udhaifu wao lakini the tricky natural instinct ni kwamba mwanamke ndio anashika mpini most of the time na ndio maana nikasema udhaifu wa mwanamke ndio unaotrigger udhaifu wa mwanamme (hapa naongelea mahusiano yasio rasmi).

Umewahi kujiuliza kwanini miaka ya zamani ilikuwa kumpata mwanamke ni vita tosha? Namaanisha haikuwa kazi ndogo, Ukipata jibu la hili suala nadhani utanipata nilikuwa namaanisha nini rafiki.
 
Watu bwana, zikiletwa thread za mke kacheat, mume ana nyumba ndogo, familia inesahaulika mnashabikia ila akija mtu kuelezea the positive side of ndoa from experience mnajitahidi kweli kumvunja moyo.

Gerrard hongera kwa kua na ndoa yenye upendo na amani mpaka wakati huu, kuna watu hata wiki hawamalizi. Muhimu wewe na mkeo wote mjitahidi kulea ndoa yenu.Msimsahau Mungu wenu either, shetani asije akawapitia maana hua anawapitia wengi kweli.
Lizzy bana! sijui wengine lakini mimi nilianza na post yangu kwa kusema "kweli wanawake wema wapo" (na I am proud kusema hata mimi ninae mmoja), lakini tu nikaongezea kwa kumpa nasaha kijana asijisahau sana na hili liulimwengu. Nadhani kuna mada ya "kulinda penzi" hizi vitu tulizifafanua kiasi haina haja ya marejeo.
 
Kloro wakati mwingine hongera tu na kutakiana heri kunatosha kabisa.Sio mtu anaanza kumwambia/toa comment za kumvunja mhusika moyo au za kumpa wasiwasi. Kama ipo siku atarudi kwaajili ya msaada basi isubiriwe hiyo siku, hamna haja ya kumwombea itokee na kuanza kumfananisha na watu wengine wasiomhusu.
 
Back
Top Bottom