Wapo Wanawake wanajiheshimu na kuheshimu ndoa zao..... Huyu ni mmoja wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapo Wanawake wanajiheshimu na kuheshimu ndoa zao..... Huyu ni mmoja wao

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SG8, Dec 16, 2011.

 1. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,200
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Habari za ku elekea weekend Wana JF.

  Imekuwa ni kawaida ya hapa JF hasa jukwaa pendwa la MMU kila siku kusikia lawama na manung'uniko miongoni mwa wanandoa hasa Wanaume wakiwalalamikia Wake au wachumba zao. Hii kwa kiasi fulani na kwa maoni yangu inaweza kuwaathiri Wanandoa wapya/watarajiwa kiasi kwamba mtu anaingia kwenye ndoa akiwa na attitude moja..... ndoa ni mateso, ugomvi, vurugu, usaliti na madhila mengine yanayofanana. Leo nimeona niwe miongoni mwa mashuhuda wa namna ndoa ilivyo tamu, raha, na ya amani hasa ukimpata mtu sahihi.
  Mimi nimeoa, nina ndoa ya miaka 6 na mtoto mmoja. Kabla ya kufunga ndoa na Mke wangu tulikaa kama Wachumba kwa miaka Minne (4).
  Naamini ni miongoni mwa watu hapa duniani ambaye nimebahatika kupata "Mke Mwema". Pamoja na Elimu yake ya kutosha tu, mshahara wake unaozidi wangu kama mara mbili na vitu vingine bado ndoa yetu imekuwa salama, tulivu na ya kufurahia kwa miaka yote tuliyoishi kama wana ndoa.

  Kwa hulka ya Wanawake wa sasa hivi.... naamini ninaye Mke ambaye sijui ni sifa gani ambazo zinapungua ili aitwe Mke Mwema. Nawasihi Wanawake wengine hapa JF na kwingineko waelewe kuwa "Mke Mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe"

  Wale ambao hawajaoa na kuolewa wasidhani kuwa ndoa ni misukosuko na vurugu kwani "mvunja ndoa ni mwana ndoa mwenyewe" na amini usiamini migogoro mingi inayoripotiwa hapa ni stori za upande mmoja tu yawezekana sisi wananume ni sehemu ya matatizo.

  Mtaniwia radhi niliowakwaza lakini naamini nimetoa uzoefu wangu
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Unajuaje kama hamegwi pembeni? Au hujui ila "unaamini" kuwa hamegwi?
   
 3. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,200
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Kwa kuwa sijui.... hakuna tatizo. Jambo usilolijua unahangaika nalo la nini?
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Whoever said ignorance is bliss hit it right on the money!
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa ushuhuda.
   
 6. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Asanteee kaka gerrard...Personally,nitafanyia kazi ushauri wako.
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hongera sana Gerald, mshukuru MUNGU kwa kukupatia mke mwema na endelea kumwomba MUNGU aendelee kukusaidia msijebadilika.

  Ila tu napenda kukukumbusha kuwa kwa sasa hivi si kila mwanamke avunjae ndoa yake ni mpumbavu... Na pia si ndoa zote zinavunjwa na wanawake tu.
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Nimechoka na kusikia mke mpumbavu hubomoa nyumba yake

  ila ujue mme mwehu hujenga nyumba ya tope ambayo mkewe anaweza ibomoa

  yadi yadi yadi yadi
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mkeo yupo JF?
   
 10. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Wanawake wema wapo kibao lakini ........................................... (nikimalizia huo ukweli hapo kwenye dots naamini kitalipuka hapa kwavile wengi wetu tumezowea kupambwa kwa uongo).
  Kwa usalama wa hii sredi nimeamua kuuchuna
   
 11. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  hahahahahaha! Waambie hao.
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Hamkawii kuja hapa na siredi za ushauri!
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Katika zama hizi za dotcom kumpata mke au mume mwema ni sawa na kutafuta needle in a haystack. Binafsi siamini yeyote yule aliye mdotcom. Yaani wale ambao twitter wapo, facebook wapo, JF wapo, Wayn wapo, gmail wapo, myspace wapo, hi5 wapo, tagged wapo, na kwingineko dotcom.

  That's why it's not a accident or just a mere coincidence that the divorce rate is higher in these days.
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Its getting on my nerve

  afu kuwa mwaminifu sio sifa ni wajibu wa watu waliopo kwenye mahusiano
  its not a favor
  wala huyu si exceptional
  waaminifu ni wengi mno
  na wala hawajitangazi

   
 15. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Bwana Gerrad kwa kupata mke mwema. Naamini kua na wewe ni mume mwema pia sababu mume mjinga anaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuharibu ndoa pia.
  Mara nyingi napenda kukumbushia kua wenye kuleta habari hapa sio representative sample. Ni sawa na kwenda kukaa gate ya hospitali alafu useme kumbe watu wengi duniani wanaumwa...
  Asante kwa story yako.
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  nakubaliana na wewe haswaa
  ndo mana mie sredi za kudumisha mahusiano huwa sichangii sana
  uaminifu kwenye ndoa its a value
  we dont learn values over one night
  its a life time lesson
  na darasa la kuanzia hilo ni kwenu
  hapa tunajazana mastori ya town tu
  ya kubeba hapa sijui??

  kwa akina dada nipotezeeni hapa
  mwanamke anafunzwa uaminifu kwao
  hasa kwa tabia za mama yake
  kama aliheshimu ndoa from heart, na mabinti tunajifunza hapo
  kama alikuwa chakaramu chances za binti kuwa chakaramu ni kubwa mno
  kadhalika na wanamme nadhani

   
 17. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Rais.
  Uko vere close na what I wanted to say yaani wanawake wema wapo lakini kimaumbile wanawake wana udhaifu fulani na hawataki kuukubali. Hapo sasa ndio maana naweka dots ................................. kwasababu ukiwapa ukweli wanaona unawadhalilisha
   
 18. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Gerrard,asante sana kwa thread yako,imeangalia na kuainisha pande zote zinazohusika na ndoa yaani mke na mume na kwamba ina discourage assumptions kwamba si kila ndoa ni mbaya.Tumezaliwa kuja kuujaza ulimwengu,kwa kufuata mafunzo ya either dini zetu ni kwamba lazima tuoe pengine ili tusitende dhambi ya kuzini kwa sababu ni either uoe,u-abstain au utende dhambi.Na kwa mila zetu za kiafrika inabidi tuoe hata kama humu kwenye javi tutasema wanandoa wa kiume wanaongoza kwa nyumba ndogo,wanandoa wa kike wanaongonza kwa serengeti boys au wanandoa wanagombana kila siku hata wanandoa wa kiume wanarudi majumbani saa tisa usiku.Watu wataoana tu kwa sababu ni imani,ni mila,na hata pia ni desturi na utaratibu.
  Lakini usichukulie juu juu kwamba kama RUSSIANROULLETE alivyosema kwamba usiende kwenye geti la hospital ukaona wingi wa watu hospitalin ukazani kila mtu hapa duniani ni mgonjwa.Na usichukulie sample moja ya kwako basi ukasema kwamba wakwako pamoja na kukuzidi kipato,pamoja na mazuri yote aliyokutendea kwamba basi mpira umeshavuka goal line kuwa goli.Miaka sita na minne ya uchumba tu,bado safari ndefu,mshukuru mungu wako kila siku unayoisha ukiwa hivyo kwani hujafa hujaumbika waswahili wanasema.Kama kusema tungeweza basi siku ya kuingia kabulini ndio siku ya kusema asante mungu kwani ulinipa mke/mme mwema.
  Huwa tunabadilika,am talking through experience.Ten yrs ya relationship ya seconday and college,ten yrs of marriege mkiwa hamna kitu,two lovely kids and at last god open up everything in your life,lakini ndoa inaanguka beyond repair.Na mungu wenu mmemtanguliza kwa kila kitu mnachofanya lakini shetani yuko nyuma anasubiri nafasi yake.I think we live sometimes to make history.Nice weekend guys,kumbuka tusio oa tusiache kwa sababu javini kuna story,tulio oa to make effort ndoa zisiangukie kwenye mikono ya shetani,tulio kwenye matatizonina ndoa mwangalie shetani aweza kuwa begani kwa hiyo haraka tubu kuokoa ndoa yako
   
 19. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,200
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Sina hakika kama yupo humu, hilo sijawahi kufuatilia
   
 20. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,200
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa hata mimi nilishawahi kuleta sredi ya ushauri wa namna ya kupata uhamisho, kwa ushauri wenu sasa nimefanikiwa na nina enjoy life na My Wife wangu
   
Loading...