Wapo wanawake 'katili'. Amuua mumewe, amkata vipande, na kumchemsha jikoni!

Yaani toka jana napata picha mikono, masikio na vidole vya marehemu vikiwa vimezidi sufuria huku vinachemka halafu mama anakuja na pilipili hoho, tangawizi na mdalasini... hii dunia hii...
 
Hii mada imegusa hisia......FUNDISHO : Fikiria kabla hujatenda jambo lolote.Mfikirie mwenzio atajiskia vipi, reaction yake itakuwaje na hata wewe mtenda unajiweka kwenye hatari gani.
 
Hii ni ya kawaida tu, mbona Asha Mkwizu? pale Upanga alifanya kitu kama hii???

Nilikuwa najaribu kukumbuka case kama hii hapa kwetu TZ, though mapishi hayakuhusika. Mimi nafikiri binadamu wote tuna hali ya unyama ndani yetu. Kwa hiyo inategemea na degree ya maudhi na mapokeo ya binadamu kunapokuwa na tukio fulani. Ila mwisho wa yote kuna majuto juu ya matokeo ya matendo yetu baadaye. Niliwahi kusoma mahali kuwa kuna kijana alijinyonga baada ya kudhulumiwa gunia la maharage. Hapa tunaweza kujiuliza kuwa gunia moja tu mtu anajimaliza? Mimi ninaamini kijana angepewa nafasi ya kurudi duniani asingefanya jaribio la kujimaliza tena. Dada mwingine yeye alimchoma mumewe na maji ya moto mwilini, baada ya hapo alikuwa akihadithia tukio lile alikuwa anajiuliza mara kadhaa kuwa aliwezaje kufanya vile?
Kwa sasa ninaweza kusema huyu mama ni katili, lakini sina uhakika kitendo alichotendewa yeye kingetokea kwangu ningechukua hatua gani, labda hiyo hiyo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom