Wapita njia warukishwa kichurachura Posta Kawe!

Walivyo

Member
Dec 8, 2009
11
1
Jamani kuna siku nilidokeza kuhusiana na eneo la Posta Kawe kuendelea kuzuiliwa na Jeshi baada ya Londa kuingia na kulisawazisha bila kuitaarifu kambi la Lugalo.

Sasa eneo hilo limekuwa hatari kwa wasiofahamu kinachoendelea, kwani wamekuwa wakirukishwa kichurachura, kupigishwa magoti na wanajeshi kila wanapokatiza eneo hilo.
 
Wanajeshi si ni kama robbots tu!...Wanapiga kwanza,then maelezo mbele ya safari.!... Sijui wasomi walioko huko hawatoi elimu kwa makoplo na maMP kutumia komoni-sensi japo kidogo!
 
BINAFSI SIPENDI TABIA YA WANAJESHI WETU WATZ KUJIONA WAO NI KAMA MIUNGU WATU, WAKO JUU YA SHERIA, WANANIKERA SANA.....Tangu aondoke Gen.Waitara hali imekua tata sana kwa watu wanaoishi jirani na kambi za jeshi.
 
Inawezekana mambo kama haya ndiyo yanasababisha jeshi lichukiwe, ndio maana mimi huwa simpi lifti askari yeyote, na sitafanya hivyo daima, na hii inatokana na tabia zao kama hizi.
 
Swali ni kua..

Je kuna jipya hapa..?

Kwani kulitegemewa wanajeshi wataacha ubabe na kuanza kuheshimu sheria za nchi??
 
Bora ndugu yangu, maana hawa dhamini raia hata kidogo, siku moja waliwahi kutukamata mimi na mwenzangu tukiwa kwenye foleni ya pale lugalo wakadai eti tumepita pembeni, Mwanajeshi akapanda eti anatupeleka police, tulivyofika mwenge karibu na kambi yao akasema simamisha hapo, tulivyosimama akashuka akidae eti msirudie tena, kumbe jamaa alikuwa anataka lifti akatumia kigezo cha kutukamata.
 
Ndio faida ya ku-recruit wahuni kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Lakini Je kulitegemewa kitu tafauti?
 
Kwani wao ni nani hadi wasiheshimu sheria za nchi?
Huu upofu wa kuamini kuwa wanajeshi wako juu ya sheria ndio unakuponza na kuanza kuushabikia ujinga wa wanajeshi.
 
Ni lazima watumie njia hiyo maana hakuna raia hata mmoja anayeweza kumsaidia askari yeyote kamwe.
 
Jamani kuna siku nilidokeza kuhusiana na eneo la Posta Kawe kuendelea kuzuiliwa na Jeshi baada ya Londa kuingia na kulisawazisha bila kuitaarifu kambi la Lugalo.

Sasa eneo hilo limekuwa hatari kwa wasiofahamu kinachoendelea, kwani wamekuwa wakirukishwa kichurachura, kupigishwa magoti na wanajeshi kila wanapokatiza eneo hilo.

ni eneo la wazi au la jeshi??kuna kibao chochote kinachokataza tresspassing?? tusilaumu tujue situation ikoje,mara ngapi tumeona watu wanakaa au kufanya biashara maeneo yanayokatazwa na vibao vipo?
 
Kwani wao ni nani hadi wasiheshimu sheria za nchi?
Huu upofu wa kuamini kuwa wanajeshi wako juu ya sheria ndio unakuponza na kuanza kuushabikia ujinga wa wanajeshi.

Lakini jipya ni lipi hapa..gret sinka anaposhindwa kuelewa the simplest of the sarcasm??
 
Ndio faida ya ku-recruit wahuni kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Lakini Je kulitegemewa kitu tafauti?

Naku-support mkuu 100%, kazi ya jeshi na polisi zimekuwa kazi za watu walioshindwa shule, waliokosa mwelekeo wa maisha, hata wakubwa wengi wa jeshini wakiona watoto zao wamevurugikiwa na mibangi suluhisho huwa ni kuwatupia jeshini, kwahiyo kinachotokea ni matunda ya tulichopanda.
 
Hapana mkuu, siku hizi jeshi linajitahidi sana kuajiri wasomi.
haya mambo yataisha tu mkuu.
 
Back
Top Bottom