Wapinzani watambue wana dhima katika usalama wa taifa

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
NA ELISA MUHINGO

Mfumo wa vyama vingi ulikuja kuimarisha dhana ya upinzani kwa makusudi ya kuwapa wananchi kuchagua moja kati ya njia kadhaa katika kuwaletea maendeleo. Ni baada ya nchi za magharibi kuchoka kusaidia nchi maskini bila kuendelea kiuchumi.

Waingereza hivi karibuni walichagua kati ya kuendelea kubaki umoja wa Ulaya au kujitoa. Mchuano ulikuwa mkali. Mwisho wengi wakachagua kujitoa. Kwa sasa waingereza wote kwa pamoja wanajadiliana namna ya kujitoa Umoja wa Ulaya. Mtu akijitokeza na kuanza kusema tusijitoe watamshangaa.

Wamarekani mwaka huu wataamua kati ya Sera za Clinton na Trump. Mchuano ni mkali. Wamarekani wako makini kuwasikiliza wagombea na mijadala ni mikali. Wanatafuta kujua serikali ijayo iweje. Baada ya uchaguzi kelele zote zitakoma na wamarekani watakuwa wamoja nyuma ya mshindi.

Ni kweli kuwa mataifa hayo mawili niliyoyataja hapo juu yanabishania agenda. Baada ya watu kuchagua moja kati ya mawili, wote wanaheshimu na kutumikia maamuzi ya wananchi wao. Lakini wanaheshimu na maamuzi yanayotolewa na kiongozi wao.

Kutokana na Marekani kuwa na agenda ndiyo maana miaka miwili iliyopita Rais Mstaafu Bush na Rais Obama walikutana hapa Tanzania na kushiriki shughuli fulani. Yapo mambo ya msingi ambayo pamoja na agenda ya taifa hutegemea kiongozi aliyepo.

Kama wamarekani watamchagua Trump, watakuwa wamechagua kujenga ukuta kati yake na Mexico. Wanaweza kuwa hawapendi hilo lakini kwa kuwa anayo mengi wanayoyataka basi wakawa tayari kuvumilia ujenzi wa ukuta huo wasioutaka. Wasiotaka watakaa kimya au watakuwa wananong’ona tu.

Nikirudi kidogo hapa kwetu naona kuna mwanya mkubwa wa kujifunza kwa wenzetu kwa makusudi ya kujenga taifa letu.

Kuna wakati Tanzania iliingia mtafaruku na Rwanda. Rais wetu kwa kuzingatia mazingira inayokumbana nayo wakimbizi wanapojitokeza, aliishauri Rwanda kuongea na makundi hasimu.

Jambo hili lilikuwa chukizo na mabadilishano ya maneno makali yakatokea. Watanzania wazalendo wote waliungana sambamba na rais wetu, kama ambavyo wanyaRwanda wazalendo waliungana na Rais wao.

Cha kushangaza baadhi ya vyama vya upinzani vilijitokeza kupinga. Hii ilifanya tuulize hata sera za nje za vyama hivyo na havikutoa majibu. Lakini katika mijadala ilikuwa wazi kuwa vyama hivyo vinapinga kwa sababu ya kutaka kupinga msimamo wa serikali.

Kipindi hicho kulikuwa na mambo mengi ya kupinga na wananchi tulikuwa upande wa vyama hivyo. Ufisadi, ubadhilifu, Ukwepaji kodi, kuchakachua mawazo ya wananchi mchakato wa katiba; kulitawala na wakati wote wananchi tulikubaliana na mikakati ya kufanya mabadiliko.

Lakini kupinga huko kwa vyama vya upinzani sina uhakikia kama nchi ingeingia vitani wapinzani wasingetumiwa na adui. Hapo usalama wan chi ungekuwa hatarini na vyama vikajiona vimefanya kazi yake (ya kupinga serikali).

Tumeingia uchaguzi mwaka jana na uchaguzi ukafanyika. Kwa kadri upepo ulivyokuwa mabadiliko Tanzania yalikuwa hayaepukiki. Ndicho kilichotokea.

Baada ya uchaguzi inatarajiwa watu na taasisi zote kuungana kutekeleza mabadiliko hayo. Lazima kila mtu/taasisi itashiriki kwa nafasi yake. Haitarajiwi vyama vya upinzani vivumilie makosa hata kama ni madogo, kama isivyotarajiwa watawala kujikosoa hadharani. Haitarajiwi pia vyama vya upinzani kupinga kila kitu.



Mambo matatu yamejitokeza:

1) Uongozi mpya umejikita kuyashughulikia matatizo yaliyowakwaza wananchi kwa miaka mingi. Ukusanyaji kodi umeimarishwa; Matumizi yasiyo na tija yamedhibitiwa. Nidhamu ya watumishi imeimarika. Watumishi wanaoshukiwa wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa mfumo uliopo ambao ulikuwa hautumiki.

Kuwahamasisha wananchi kuchangia madawati. Kama kuna jambo lilitia aibu ni Tanzania yenye miti ya mbao kukosa madawati. Yapo yanayofanyika kuandaa misingi ya kufanya mambo muhimu.

Mfano huwezi kushirikiana na watu wanaodhaniwa ni wezi au mafisadi kuweka mifumo ya kudhibiti wizi. Lakini kuna yanayofanyika kwa sababu muda wa kuyafanya ulishapita na bila sababu, mfano kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma.



2) La pili lililojitokeza ni wananchi na viongozi wa nchi za nje kuuona uongozi wa Tanzania ni wa kuigwa. Wakati wa uchaguzi wa Uganda kuna wagombea waliojitangaza kama wao ni ‘’Magufuli’’ wa Uganda.

Wakenya walimshauri Rais wao kuiga wa Tanzania na kadhalika. Nchi nyingi zilitamka na bado zinatamka matamshi ya kutia moyo watanzania kuwa na matumaini ya kujikomboa kutoka kwenye dimbwi la umaskini.



3) La tatu ni baaadhi ya vyama vya siasa kubeza na kupinga kila kitu. Pale waliposhindwa kupinga wakakaa kimya. Hii inauumiza upinzani wenyewe kwani machoni pa watu wenye akili wanaonekana (wapinzani) hawaoni kinachoonwa na wengine.

Wapinzani wamebeza mpaka juhudi za kuondoa tatizo la madawati na kusema wangeanza kuongeza mishahara ya walimu (japo mishahara haiwezi kulipwa kwa fedha za michango). Wamebeza na kuhamia Dodoma na sijui nini watasema kama serikali itahamia huko.

Wabunge wa upinzani wakiwa na nia ya kuidhalilisha serikali kupitia bunge mubashara, na serikali kwa kutambua hilo ikaamua kuzima matangazo kwa sababu ilizozitoa. Ukweli uliowazi ni huo kuwa kwa lengo la kuishauri na kuisimamia serikali wapinzani walitaka kuishambulia hadharani na kuikasirisha.

Matunda ya mambo hayo ni mtafaruku uliojitokeza. Nao ukaja na mambo makubwa haya:

  • Serikali kuamua kuonyesha uwezo wake kuwadhibiti wapinzani. Polisi wamezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa kutumia kipengere cha kuombwa ulinzi wakati wa mikutano. Rais kuzuia mikutano ya uanaharakati hadi kipindi cha kampeni.
  • Vyama vya upinzani vikaamua kutangaza mgogoro na serikali na kutangaza maandamano na mikutano ambayo haiendi kwa sheria. Tuiite civil disobedience. Wanatarajia wananchi wawe upande wao kama ilivyokuwa miaka ile.
  • Serikali ikaamua kuonyesha vyombo vyake inavyovitumia kulinda demokrasia. Polisi wakaonyesha ujuzi wao. Majeshi yakajiandaa kuadhimisha kuanzishwa kwake.
  • Mtafaruku ukaongezeka. Waandamanaji wakapungua. Kwa bahati haitadhihirika. Hiyo itasaidia kila upande kushinda huko tuendako. Bila shaka anayeshinda na anayeshindwa anaanza kutafuta pa kutokea.
  • Bahati nzuri wakajitokeza viongozi wa Taasisi mbalimbali kutaka ‘kusuruhisha’. Serikali ikatoa msimamo wake. Haioni cha kujadili katika usuruhishi. Vyama vikaamua kupumulia hapo. Vimetangaza kusitisha maandamano kupisha usuruhishi. Humu twaweza kupata muafaka. Ingekuwaje bila usuruhishi? Lakini pia itakuwaje katika usuruhishi? Wasuruhishi kuwaambia wabunge waliosusia bunge kuwa peleka mashtaka kwa Spika? Hili linasubiriwa wabunge wetu waambiwe na Masheikh na wachungaji. Kuelezwa kuwa matendo yanayotendwa na serikali ya awamu ya tano yanasifiwa na wengi msiyapinge? Ndiyo. Maaskofu watawaeleza.
Ni muhimu kuelekeza upinzani wetu kuchangia usalama na maendeleo ya nchi zetu.

Japo kama taifa hatujawa na agenda lakini ni muhimu wapinzani kuyapima wanayoyatenda yanachangia kwa kiasi gani kutatua matatizo ya msingi ya watanzania. Labda serikali hii kabla ya kumaliza mhula wake wa pili ihakikishe Tanzania ina agenda.

Agenda ambayo vyama vyote vitaitumikia. Kitakachoipinga kiitwe mhaini na kushtakiwa kwa kosa hilo. Vyama vitumike kulinda agenda ya maendeleo na usalama wa Taifa letu.

Tunaona kubeza juhudi za kulikomboa taifa kutoka ufisadi na rushwa. Hii ifike mahala iitwe uhaini. Hayo yatahitajika kuingizwa kwenye katiba mpya. Kinyume chake upinzani huu tunaouona unaweza kutupeleka kwingine tusikotaka. Mtu akikataa kuuvumilia unashindwa umzuieje.

Chanzo Rai
 
Makala nzuri na inafunza...ngoja wanywa viroba waje uone pumba zao
 
Hata wezi kwa wezi wanapofanya mabadiliko ktk uongozi mkuu wa wezi, nayo ni mabadiliko!

Hicho ndicho kilichotokea Tanzania mwaka jana trh 25/10/2015 kwa kutaka kutuaminisha kwamba CCM wamekuja na mabadiliko = wezi kubadilishana uongozi miongoni mwa wezi wao wenyewe then wanatu fool kuwa hayo ndiyo mabadiliko watanzania waliyokuwa wanayataka!!

This is not the change the majority of Tanzanians wanted.

You can't fool us. We are still fighting for the real changes, specifically throwing CCM out of power!
 
Back
Top Bottom