Wapinzani watambue kuwa Uchaguzi Mkuu utafanyika Tanzania na sio nje

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
UCHAGUZI MKUU UTAFANYIKA TANZANIA NA SIO NJE!

Ukitizama vyama vya CHADEMA na ACT unaweza kudhani uchaguzi mkuu utafanyika Ulaya na Marekani! Utadhani watakaopiga kura ni wazungu, benki ya dunia, BBC, VOA, DW, Amnesty International, n.k. Yaani wamewekeza nje! Wanafanya kampeni nje! Na huu ndio mwaka wanaita wa mageuzi!

Lissu yuko nje na hataki kurudi japo aliahidi mara tu madaktari wake watakapomruhusu atarudi! Zitto naye kahamia nje na ukimsikiliza anaanza hadithi za Lissu! Usalama! Huyu naye siku si nyingi tutasikia sirudi mpaka nisindikizwe! Akiwa Toronto alitamka eti hamuogopi Magufuli! Sijui Magufuli kamtisha lini? Lakini anasema haogopi huku anadai anahisi atakamatwa akirudi! Labda atakamatwa ili aulizwe ni lini Magufuli alitaka amuogope?

Sasa Mzee wa Kiberiti naye alitaka asepe! Kakwaa kisiki cha mahakama. Mangi Makene anadai alikuwa aende kibiashara lakini badala ya mfanyabiashara kulalamika anayelalamika ni msemaji wa chama! Wanatoa siri ya safari! Sio ya kibiashara!

Niwakumbushe tu wakati nyie mmehamishia kampeni mpaka na vikao nje ya nchi wenzenu wa chama kikuu na vingine wanahangaika na wapiga kura!

Tulidhani hiki ni kipindi mngesaka wanachama, kuhuisha madaftari yenu ya wanachama, kujenga ofisi, kutongoza wa CCM nao wahamie kwenu (hata mkiwanunua si mbaya), mngekubaliana namna ya kuachiana majimbo na nani agombee wapi, nani awapeperushie bendera, mikutano wakati wa kampeni ifanyikie wapi (sio kila mahali panafaa), n.k.
Siku mkikumbuka shuka mtakuta mna malaria plus plus!
 
ANC wakati inamshikisha adabu kaburu ukiacha viongozi kama Mandela na baadhi waliokuwa jela wengine wengi walikuwa nje ya nchi kwa sababu Makaburu walikuwa wauaji, wabambika kesi na wasiojali utu wa wengine. Tabia ambazo CCM ya sasa inazo.
Kuhusu wapiga kura, wapinzani wanao wa kutosha Ila kwa sababu hawako hadharani mnadhani hawapo.
Hebu angalia maadhimisho ya CCM 43 jinsi yalivyokuwa, ilikuwa ni furaha ya mashaka kwa viongozi tuu lakini hao muwaitao wanyonge hakuna aliyeonyesha mvuto na kinachoendelea. Hivyo weka Tume huru ya uchaguzi uone CCM inavyogeuka historia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuokoa gharama, itabidi ccm ifanye ule mchujo wake wa kupata wagombea, baada ya hapo, waliopita ndiyo watangazwe kama madiwani, wabunge na Rais.

Pesa iliyokuwa ielekezwe kwenye uchaguzi, ipelekwe kujenga SGR na Stigler Gorge.

#tukovizurimsiogope.
 
kwani ratiba ya mikutano imeishatolewa? au hukusikia wakati bunge linahairishwa alivyosema mtendaji mkuu wa serikali? acha kujisahaulisha . Hapa nyumbani kazi hiyo bado!!
 
Hakuna Kimaro mwenye akili za kuunganishiwa.. Kilichoandikwa ni ushahidi wa ninachosema..
 
Hayo unayotaka wafanye hapa ni kupitia jukwaa gani litakaliheshimiwa na awamu ya tano ?!. Utaendesha hizo campaign kwa wapiga kura unaowasema kimya kimya ?!. Kwamba hujui makamanda na na DC wameagizwa nini !!. Wewe kama ni ccm usiwachagulie wapinzani wako njia ya kupita.
 
Back
Top Bottom