CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
UCHAGUZI MKUU UTAFANYIKA TANZANIA NA SIO NJE!
Ukitizama vyama vya CHADEMA na ACT unaweza kudhani uchaguzi mkuu utafanyika Ulaya na Marekani! Utadhani watakaopiga kura ni wazungu, benki ya dunia, BBC, VOA, DW, Amnesty International, n.k. Yaani wamewekeza nje! Wanafanya kampeni nje! Na huu ndio mwaka wanaita wa mageuzi!
Lissu yuko nje na hataki kurudi japo aliahidi mara tu madaktari wake watakapomruhusu atarudi! Zitto naye kahamia nje na ukimsikiliza anaanza hadithi za Lissu! Usalama! Huyu naye siku si nyingi tutasikia sirudi mpaka nisindikizwe! Akiwa Toronto alitamka eti hamuogopi Magufuli! Sijui Magufuli kamtisha lini? Lakini anasema haogopi huku anadai anahisi atakamatwa akirudi! Labda atakamatwa ili aulizwe ni lini Magufuli alitaka amuogope?
Sasa Mzee wa Kiberiti naye alitaka asepe! Kakwaa kisiki cha mahakama. Mangi Makene anadai alikuwa aende kibiashara lakini badala ya mfanyabiashara kulalamika anayelalamika ni msemaji wa chama! Wanatoa siri ya safari! Sio ya kibiashara!
Niwakumbushe tu wakati nyie mmehamishia kampeni mpaka na vikao nje ya nchi wenzenu wa chama kikuu na vingine wanahangaika na wapiga kura!
Tulidhani hiki ni kipindi mngesaka wanachama, kuhuisha madaftari yenu ya wanachama, kujenga ofisi, kutongoza wa CCM nao wahamie kwenu (hata mkiwanunua si mbaya), mngekubaliana namna ya kuachiana majimbo na nani agombee wapi, nani awapeperushie bendera, mikutano wakati wa kampeni ifanyikie wapi (sio kila mahali panafaa), n.k.
Siku mkikumbuka shuka mtakuta mna malaria plus plus!