Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
WAPINZANI WATAENDELEA KUSHIRIKI UCHAGUZI BILA KUSHIKA DOLA
Mwaka 2014, nilichekeshwa na makala kuhusu India, iliyoandikwa na mwandishi wa nchi hiyo, Rakesh Dubbudu. Aliandika kuwa vyama vya siasa nchini humo vinakua kwa kasi kuliko ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kichekesho ni kuwa India ni moja ya mataifa duniani ambayo uchumi wake unakua kwa kasi. Umaskini kama Taifa na kwa wananchi wake umeshaonyeshwa njia pana ya kutokea. Hata hivyo, eti vyama vya siasa vinazidi kasi ya uchumi kwa namna vinavyokua.
Tanzania ina vyama zaidi ya 20 lakini vinavyoshiriki na angalau kushinda ubunge na udiwani ni vitano.
Chadema ambacho ndiye kinara wa upinzania Tanzania, wamekuwa wakitumia mtindo wa operesheni lukuki kama M4C,Sangara,Ukuta,Kata funua na kuishia kuchukua wagombea kutoka CCM.
CUF nguvu kubwa ipo Zanzibar huku tegemeo likiwa ni Sefu, NCCR-Mageuzi chenye mbunge mmoja ni chama chenye homa za vipindi mara kipotee mara kiibuke.
ACT-Wazalendo kimeanza miaka michache iliyopita kina mbunge mmoja,madiwani kadhaa na kinaongoza halmashauri moja huko mkoani Kigoma.