Wapinzani wataendelea kushiriki uchaguzi bila kushika dola, Lowassa anajua, UKAWA wanajua

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
WAPINZANI WATAENDELEA KUSHIRIKI UCHAGUZI BILA KUSHIKA DOLA

Mwaka 2014, nilichekeshwa na makala kuhusu India, iliyoandikwa na mwandishi wa nchi hiyo, Rakesh Dubbudu. Aliandika kuwa vyama vya siasa nchini humo vinakua kwa kasi kuliko ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kichekesho ni kuwa India ni moja ya mataifa duniani ambayo uchumi wake unakua kwa kasi. Umaskini kama Taifa na kwa wananchi wake umeshaonyeshwa njia pana ya kutokea. Hata hivyo, eti vyama vya siasa vinazidi kasi ya uchumi kwa namna vinavyokua.

Tanzania ina vyama zaidi ya 20 lakini vinavyoshiriki na angalau kushinda ubunge na udiwani ni vitano.

Chadema ambacho ndiye kinara wa upinzania Tanzania, wamekuwa wakitumia mtindo wa operesheni lukuki kama M4C,Sangara,Ukuta,Kata funua na kuishia kuchukua wagombea kutoka CCM.

CUF nguvu kubwa ipo Zanzibar huku tegemeo likiwa ni Sefu, NCCR-Mageuzi chenye mbunge mmoja ni chama chenye homa za vipindi mara kipotee mara kiibuke.

ACT-Wazalendo kimeanza miaka michache iliyopita kina mbunge mmoja,madiwani kadhaa na kinaongoza halmashauri moja huko mkoani Kigoma.
 
Tegemeo na kiburi kikubwa cha ccm ni tume ya uchaguzi tu kwa sasa. na ww mleta mada unalijua hilo ndiyo maana umeandika haya uliyo yaandika.

vyama vya upinzani kwa sasa hv siyo tanzania tu vina nguvu kubwa mno. hii ni kutokana na changamoto za ongezeko la watu ambapo hakuna serikali ambayo inaweza kukamilisha matamanio ya watu inao waongoza.

sasa kwa afrika hata upinzani ufanye maajabu gani bado watawala wataamua yao kama tulivyoona gambia, uganda na sehemu nyinginezo
 
Huna akili.

Tume huru hamtaki alafu unaleta upuuzi wako hapa!

Tume sio huru na matokeo ya uraisi yakishatangazwa hayohijiwi mahali popote pale alafu bila aibu mnajisifu kushinda uchaguzi!

Mnafiki wa kiwango cha juu sana wewe!

Kweli bora mchawi kuliko mnafiki.
Mmiliki wa chadema Lowasa alisema tume ni huru na hataibiwa kura hata moja.

Salary slip lowasa alisema uongo??
 
..hio tume ya uchaguzi inayolalamikiwa na upinzani kwenye uchaguzi,kwa nini haivunjwi,au hairuhusiwi kisheria?
 
Wewe ni kapuuzi fulani. Hivi zile hadithi za kung'ang'aniza watumishi wa umma kuipenda CCM kwa lazima kama mlivyokuwa mnafanya kule Iringa umeacha?
 
Kama tume sio huru kwa nini upinzani mnakubari kuingia kwenye uchaguzi?? na kama tena tume huru haipo na hao wabunge wenu wa upinzani na majiji yaliyoshikwa na ukawa yamepatikaneje??
Acheni kuchanganyikiwa bwanaaa.
 
WAPINZANI WATAENDELEA KUSHIRIKI UCHAGUZI BILA KUSHIKA DOLA

Mwaka 2014, nilichekeshwa na makala kuhusu India, iliyoandikwa na mwandishi wa nchi hiyo, Rakesh Dubbudu. Aliandika kuwa vyama vya siasa nchini humo vinakua kwa kasi kuliko ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kichekesho ni kuwa India ni moja ya mataifa duniani ambayo uchumi wake unakua kwa kasi. Umaskini kama Taifa na kwa wananchi wake umeshaonyeshwa njia pana ya kutokea. Hata hivyo, eti vyama vya siasa vinazidi kasi ya uchumi kwa namna vinavyokua.

Tanzania ina vyama zaidi ya 20 lakini vinavyoshiriki na angalau kushinda ubunge na udiwani ni vitano.

Chadema ambacho ndiye kinara wa upinzania Tanzania, wamekuwa wakitumia mtindo wa operesheni lukuki kama M4C,Sangara,Ukuta,Kata funua na kuishia kuchukua wagombea kutoka CCM.

CUF nguvu kubwa ipo Zanzibar huku tegemeo likiwa ni Sefu, NCCR-Mageuzi chenye mbunge mmoja ni chama chenye homa za vipindi mara kipotee mara kiibuke.

ACT-Wazalendo kimeanza miaka michache iliyopita kina mbunge mmoja,madiwani kadhaa na kinaongoza halmashauri moja huko mkoani Kigoma.
Bado hujapona na ule ulemavu wako wa akili,go to get further Brain Treatments out Tz. maana ndiyo wanakuharibu zaidi daily unazidi kufyatuka.
 
Tegemeo na kiburi kikubwa cha ccm ni tume ya uchaguzi tu kwa sasa. na ww mleta mada unalijua hilo ndiyo maana umeandika haya uliyo yaandika.

vyama vya upinzani kwa sasa hv siyo tanzania tu vina nguvu kubwa mno. hii ni kutokana na changamoto za ongezeko la watu ambapo hakuna serikali ambayo inaweza kukamilisha matamanio ya watu inao waongoza.

sasa kwa afrika hata upinzani ufanye maajabu gani bado watawala wataamua yao kama tulivyoona gambia, uganda na sehemu nyinginezo
Tume huru inapatikanaje?
 
Wamewafunga watu kamba za miguu na mikono kisha wanawalaumu hawawezi kuogolea,wekeni tume huru basi nyie magamba.

Rafiki unapiga madongo vioo vya nyumba ya mboga mboga vitakwisha
 
baada ya kusoma kichwa cha habari na mleta ni wewe nimeghairi kusoma habari yote kwani km kawaida yako itakuwa imejaa fitina, majungu na dhihaka,

badilika 2017 uishi maisha tofauti na hayo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom