Wapinzani 'wasusia' Bunge

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Wabunge wa upinzani wametoka bungeni wakipinga kile wanachokiita kusuasua kwa mazungumzo ya muafaka kuhusu Zanzibar. Wabunge hao wametoka muda mfupi baada ya kikao cha bunge kuanza na asubuhi kabla ya Bunge Kiongozi wa kambi hiyo alikwenda nyumbani kwa Spika Samwel Sitta kumueleza nia yao hiyo.

Je, hii ni njia muafaka kushinikiza mwafaka wa Zanzibar?
 
Kutoka ndani ya Bunge sioni kama ni suluhu ila inaweza kuwa ni njia ya kuonyesha kutoridhishwa kwao na maamuzi ya CCM. Baada ya kutoka what next?
 
Shida ni uchache wa wabunge wa upinzani bungeni, mawazo yao ni sahihi kama kutoka kwao kungeleta upungufu wa wabunge unasababisha kutopitisha mswada au maamuzi
 
Wabunge wa upinzani wametoka bungeni wakipinga kile wanachokiita kusuasua kwa mazungumzo ya muafaka kuhusu Zanzibar.

Very good move, now this is what I am alyways talking about kwamba for God's sake do something badala ya kukaaa kulia lia tu kwa sababu this sends a strong message kwa the powers kwamba kuna problem na deal with it, and do it now! Sasa wasuke au wanyoe!

Bravo Wabunge wa Upinzani on this, I mean at least do something!
 
Chochote kinachoweza kuonyesha kwamba kilichotendeka huko Butiama kuhusu mwafaka kinakera na kitendeka. Pamoja na uchache wao, message sent na leo CCM hawawezi kuchoma nyama pale mnadani bila kulizungumzia hili. Vilevile hata wale wananchi ambao walikuwa hawajaelewa kinachoendelea wataamka na kujiuliza kunani! For this, I support the wapinzani's move.
 
.

Pili vipi kwanini wabunge wote ambao wanachukizwa na Ufisadi wa EPA na porojo zinazooendelea nao wasitoke Bungeni jamani???????

...I would hope that so,they just dont care and think that thing is aint for them,simply a part of ufisadi system...phucc that!
 
kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi.

ukisusa wenzio twala

Heshima mbele mkuu
hata kitu ni kwa ajiri ya masirahi ya Taifa ila kwa sababu kinausu CCM unakuwa mkali kama nini. lakini hamna tabu maana unatekeleza ibara ya .....
Pole sana maana Watanzania wameamua.
 
Internatinal community hapa naona wameanza kulichukulia serious jambo hili na haswa baada ya wabunge wa upinzani jana kutoka bungeni.

JK hana habari na hili kwani haoni kama nyumbani kwake kuna matatizo ,ila yeye anafikiri kumtoa kanal Barca kuna tofauti gani na kumtoa Karume pale?

Naunga mkono wapinzani kwa hatua yao hii na iwe endelevu ili kuhakikisha kuwa jamii na wananchi wanaanza kujiuliza na kupaza sauti zao juu kwani wa huku bara walikuwa wanaona kama hili ni jambo ambalo linawahusu wazanzibar peke yao na sio nchi nzima kwa ujumla wake.
 
Nilisikiliza ile habari ya bbc jana kuhusu sakata hili kidogo nivunje I-phone yangu. Yaani kuna mbunge alikuwa analeta sijui mambo ya ibara gani na miongozo ya spika hadi nikashangaa.

Tatizo ni kuwa ccm hawaonekani kuwa na mpango wa kuleta suluhu Zanzibar na wao kila kitu ni siasa tu.
 
Wabunge wa upinzani wametoka bungeni wakipinga kile wanachokiita kusuasua kwa mazungumzo ya muafaka kuhusu Zanzibar. Wabunge hao wametoka muda mfupi baada ya kikao cha bunge kuanza na asubuhi kabla ya Bunge Kiongozi wa kambi hiyo alikwenda nyumbani kwa Spika Samwel Sitta kumueleza nia yao hiyo.

Je, hii ni njia muafaka kushinikiza mwafaka wa Zanzibar?
Wapinzani kususia ni ujinga
 
Back
Top Bottom