Wapinzani wapinga TAKUKURU kuchunguza mkataba wa Buzwagi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Wapinzani wapinga TAKUKURU kuchunguza mkataba wa Buzwagi

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima

HATUA ya serikali kutangaza kuwa inachunguza tuhuma za ufisadi na utiaji saini mkataba wa madini wa Buzwagi, imetafsiriwa na wanasiasa wa kambi ya upinzani kuwa ni kulamba matapishi yake yenyewe.
Kwa mujibu wa tamko lililotolewa jana na ushirikiano wa vyama vinne vya upinzani, serikali haiwezi kujichunguza yenyewe baada ya wabunge wa CCM kukataa kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kuchunguza shaka iliyoonyeshwa na kambi ya upinzani katika mkataba wa Buzwagi.

Tamko hilo ambalo lilisomwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania (TLP), Augustine Mrema, kwa niaba ya viongozi walio katika ushirikiano huo, linaitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza tuhuma hizo kabla ya Novemba mwaka huu.

Kwamba iwapo serikali haitatekeleza hilo katika muda huo, kambi ya upinzani itatangaza mgogoro wa kitaifa utakaohusisha maandamano ya nchi nzima.

Kauli hii ya wapinzani inatokana na tamko la serikali lililotolewa wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoindamana serikali na kauli za kutaka ijisafishe kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje.

Membe alieleza kuwa serikali imekwishaiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuchunguza tuhuma hizo za ufisadi na kuwataka mabalozi kutoingilia masuala ya ndani ya nchi kwa vile wanakiuka mkataba wa Vienna.

Tamko la kambi ya upinzani linaeleza kuwa vyama vya siasa vya upinzani havina imani na uchunguzi unaofanywa na serikali kwa vile ni jambo gumu kwa serikali kujichunguza yenyewe.

“Sisi vyama vya upinzani, tunamtaka Rais Jakaya Kikwete kuitisha kongamano la kitaifa litakalohusisha vyama vya siasa, taasisi za dini, wasomi, wanasheria na iunde tume huru ya kuchunguza tuhuma zote ambazo serikali imeshindwa kuzijibu,” alisema Mrema wakati akisoma tamko hilo.

Alisema kambi ya upinzani iko tayari kufika mbele ya tume hiyo kutoa ushahidi dhidi ya madai ya ufisadi iliyoyatoa na kuongeza kuwa wanasiasa wa upinzani wako radhi kutoa ushirikiano kwa tume huru itakayoundwa na iwapo ushahidi huo huutakamilika, wahusika wako tayari kuwajibika.

“…Tunasisitiza kutokana na kiburi na kutojali kwa serikali kuhusu tuhuma zinazoikabili, iwapo itapuuza kauli hii ijiandae kukabiliana na mgogoro wa kitaifa utakaohusisha maandamano na migomo nchi nzima hadi hapo ufumbuzi na ukweli juu ya tuhuma za ufisadi utakapopatikana.

“Tuhuma za ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na mikataba mibovu ya madini, haziwezi kuchunguzwa na serikali au vyombo vyake kwa sababu fedha nyingi za BoT zilipitia kwenye makampuni hewa, ili kugharamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa wagombea wa ngazi zote wa CCCM,” alisema Mrema.

Wakati huo huo, vyama hivyo vimewaandikia barua mabalozi wote wa nje wanaoziwakilisha nchi zao vikiwaunga mkono kwa kufuatilia matumuzi ya fedha za misaada zinazotolewa na serikali zao.

Hatua hiyo inatokana na onyo la Waziri Membe kwa mabalozi hao alilolitoa mwishoni kwa wiki iliyopita akiwataka wasiingilie mambo ya ndani ya nchi.

Katika barua yao hiyo, vyama hivyo vimeeleza kusikitishwa na kusononeshwa na vitisho vilivyotolewa na Waziri Membe kwa mabalozi hao ambao wameonywa kuacha kuzungumza wazi wazi kuhusu tuhuma za ufisadi na kashfa nyingine zinazoiandama serikali.

Barua hiyo inaeleza kuwa nchi za Ulaya na Marekani ambazo balozi zao zimekemewa na Waziri Membe zinatoa zaidi ya asilimia 40 ya fedha za maendeleo ya bajeti ya Tanzania kwa kila mwaka, na pia kulipa madeni pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa Serikali ya Tanzania.
 
Kwa maoni yangu kama mkataba wa Buzwagi inabidi uchunguzwe basi iundwe kamati huru ya wabunge watano toka CCM watano toka upinzani na wanasheria watano. Pia uchunguzi huo uhusishe mikataba ya uchimbaji wa madini ya mwanzo kabisa ambayo hadi hii leo bado imefanywa siri. Vinginevyo ili kupunguza gharama kwa walipa kodi mkataba wa Buzwagi na mingine ya uchimbaji ifutwe na kuandikwa upya ili iwe na maslahi kwa Tanzania na Watanzania. Haiwezekani Barrick waendelee kung'ang'ania mikataba yenye manufaa kwa shareholders wao wakati huo huo inatishia uhai wa uongozi wa nchi uliopo madarakani.
 
Hili ndilo suala ambalo tulikuwa tunategemea lifanyike, na ndiyo ilikuwa imani kubwa kwa wananchi wa Tanzania. Halafu na JK alipoingia madarakani alituhakikishia hili. Lakini gafla nashangaa mawaziri wake kuwa wanatembea nchi nzima kupinga mikataba kuangaliwa upya/kufanyiwa marekebisho. Je wanapingana na kauli ya boss wao?

Lakini vile vile nikikumbuka kauli ya JK mwenyewe kwamba anashangaa kwa nini tunakuwa masikini pia nasikia kizunguzungu, inakuwaje mtu aliyepata 80% ya kura zote naye alalamikie kitu anachoweza kukiona hata kutokana na suala la BUzwagi tu?

Mimi nafikiri kwa busara alivyorudi arudishe wale wanaohutubia kwenye stendi eti uzuri wa bajeti. Huwezi kuhutubia uzuri wa bajeti, Uzuri wake unatakiwa kuonekana mitaani. Wananchi ndio wanafaa kuwaelezea mawaziri uzuri wa bajeti. Utaelezeaje uzuri wa bajeti kwa watu ambao hawawezi kupata mlo kwa siku?
 
Hili swali nilishauliza ni wapi ambapo Zitto alidai kuwa kuna rushwa kwenye mkataba wa Buzwagi?
 
Mzee Mwanakijiji hawa jamaa wanatafuta njia ya kutokea ndio sababu wanatapatapa namna hii. Zito alitoa hoja ya msingi ambayo Bunge lilikuwa linatakiwa kuunda kamati kulishughulikia lakini hivi sasa ni mazingaombwe tu.

Serikali hivi sasa imeshindwa kufanya kazi zake kwa ufasaha takriban wiki tatu tangu rais alipoenda nje lakini rais anarudi anasuasua tu na hawa viongozi wanakula pesa ya walipa kodi bila kufanya kazi. Kazi iliyopo ni ya kuzomewa tu. WHAT A JOKE!
 
Hili ndilo suala ambalo tulikuwa tunategemea lifanyike, na ndiyo ilikuwa imani kubwa kwa wananchi wa Tanzania. Halafu na JK alipoingia madarakani alituhakikishia hili. Lakini gafla nashangaa mawaziri wake kuwa wanatembea nchi nzima kupinga mikataba kuangaliwa upya/kufanyiwa marekebisho. Je wanapingana na kauli ya boss wao?

Lakini vile vile nikikumbuka kauli ya JK mwenyewe kwamba anashangaa kwa nini tunakuwa masikini pia nasikia kizunguzungu, inakuwaje mtu aliyepata 80% ya kura zote naye alalamikie kitu anachoweza kukiona hata kutokana na suala la BUzwagi tu?

Mimi nafikiri kwa busara alivyorudi arudishe wale wanaohutubia kwenye stendi eti uzuri wa bajeti. Huwezi kuhutubia uzuri wa bajeti, Uzuri wake unatakiwa kuonekana mitaani. Wananchi ndio wanafaa kuwaelezea mawaziri uzuri wa bajeti. Utaelezeaje uzuri wa bajeti kwa watu ambao hawawezi kupata mlo kwa siku?

Hili la kusema hajui kwanini Tanzania ni maskini mimi limeniacha mdomo wazi. Itakuwaje Rais wa nchi usijue nini kinachoisibu nchi yako mpaka inakuwa maskini. Kwa maana nyingine huwezi kutataua matatizi ya nchi yako kama hujui tatizo liko wapi.

Miaka ile ya nyuma uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania ulikuwa ni kilimo cha mazao ya biashara ikiwemo Pamba, Kahawa, Katani n.k. ambapo baadhi ya uzalishaji wa mazao hayo ulikuwa unaathirika kwa hali ya hewa na mengineyo ikiwemo bei katika soko la dunia matokeo yake iliathiri mapato ya fedha za kigeni. Uzalishaji wa mazao hayo haukuwa mkubwa sana ili kulikwamua taifa katika hali ya umaskini na hili pia lilichangiwa na wananchi kuanza 'kukopwa' mazao yao na vyama vya ushirika ambako kuliwavunja nguvu wakulima wengi.

Wengi tulitegemea kuja kwa 'wachukuaji' or wawekezaji katika nyanja mbali mbali za uchumi wa Tanzania na hasa uchimbaji wa madini kungeongeza kwa kiasi kikubwa ajira, mishahara mizuri na hatimaye mapato ya kodi na hivyo kuinua pato la Taifa na kuikwamua Tanzania katika kundi la nchi maskini duniani, lakini miakataba hiyo ilisainiwa bila kujali maslahi ya nchi kama tulivyoona katika mkataba ulioboreshwa wa Buzwagi ambao hauna maslahi yoyote kwa Tanzania.

Kama Tanzania ingeambualia 40% Kwa bei ya October 4, 2007 $728.40*2,640,000 (ounces zinazosemekana ziko pale Buzwagi)=$1,922,976,000 ya mgodi wa Buzwagi pekee yake ambao unakadiriwa kuwa na uhai wa miaka 10 basi kwa mwaka Tanzania ingepata kwa mwaka $48,074,400 na katika miaka 10 $480,744,000 hii ingesaidia sana kuinua kiwango cha maisha cha Watanzania wengi kama pesa hii itaelekezwa katika kuahkikisha hilo, lakini tutakichokipata toka Buzwagi ni kidogo mno. Sasa tukiweka mapato ya migodi yote kwa mwaka, Tanzania inaweza kabisa kuwa na bajeti ambayo haina utegemezi kwa wafadhili. Lakini hili kama siri kali itakuwa tayari kupunguza matumizi ya anasa na yasiyokuwa ya lazima kama mashangingi, kutibiwa nje kwa vingunge (anayestahili kutibiwa nje awe Rais na Waziri Mkuu tu labda na wake zao).

Lakini viongozi wetu tunawajua walivyo mahiri katika ufujaji wa pesa, kwa hiyo pamoja na rasilimali zetu zote tutabaki kuwa nchi maskini wakati utajiri wetu unawanufaisha wageni.
 
Hii hesabu mbna inakaribia na ambayo TRA wametoa mkuu BAK, ingawa andiko ni la miaka 10 iliyopita?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom