BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,180
Wapinzani wapinga TAKUKURU kuchunguza mkataba wa Buzwagi
na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima
HATUA ya serikali kutangaza kuwa inachunguza tuhuma za ufisadi na utiaji saini mkataba wa madini wa Buzwagi, imetafsiriwa na wanasiasa wa kambi ya upinzani kuwa ni kulamba matapishi yake yenyewe.
Kwa mujibu wa tamko lililotolewa jana na ushirikiano wa vyama vinne vya upinzani, serikali haiwezi kujichunguza yenyewe baada ya wabunge wa CCM kukataa kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kuchunguza shaka iliyoonyeshwa na kambi ya upinzani katika mkataba wa Buzwagi.
Tamko hilo ambalo lilisomwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania (TLP), Augustine Mrema, kwa niaba ya viongozi walio katika ushirikiano huo, linaitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza tuhuma hizo kabla ya Novemba mwaka huu.
Kwamba iwapo serikali haitatekeleza hilo katika muda huo, kambi ya upinzani itatangaza mgogoro wa kitaifa utakaohusisha maandamano ya nchi nzima.
Kauli hii ya wapinzani inatokana na tamko la serikali lililotolewa wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoindamana serikali na kauli za kutaka ijisafishe kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje.
Membe alieleza kuwa serikali imekwishaiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuchunguza tuhuma hizo za ufisadi na kuwataka mabalozi kutoingilia masuala ya ndani ya nchi kwa vile wanakiuka mkataba wa Vienna.
Tamko la kambi ya upinzani linaeleza kuwa vyama vya siasa vya upinzani havina imani na uchunguzi unaofanywa na serikali kwa vile ni jambo gumu kwa serikali kujichunguza yenyewe.
Sisi vyama vya upinzani, tunamtaka Rais Jakaya Kikwete kuitisha kongamano la kitaifa litakalohusisha vyama vya siasa, taasisi za dini, wasomi, wanasheria na iunde tume huru ya kuchunguza tuhuma zote ambazo serikali imeshindwa kuzijibu, alisema Mrema wakati akisoma tamko hilo.
Alisema kambi ya upinzani iko tayari kufika mbele ya tume hiyo kutoa ushahidi dhidi ya madai ya ufisadi iliyoyatoa na kuongeza kuwa wanasiasa wa upinzani wako radhi kutoa ushirikiano kwa tume huru itakayoundwa na iwapo ushahidi huo huutakamilika, wahusika wako tayari kuwajibika.
Tunasisitiza kutokana na kiburi na kutojali kwa serikali kuhusu tuhuma zinazoikabili, iwapo itapuuza kauli hii ijiandae kukabiliana na mgogoro wa kitaifa utakaohusisha maandamano na migomo nchi nzima hadi hapo ufumbuzi na ukweli juu ya tuhuma za ufisadi utakapopatikana.
Tuhuma za ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na mikataba mibovu ya madini, haziwezi kuchunguzwa na serikali au vyombo vyake kwa sababu fedha nyingi za BoT zilipitia kwenye makampuni hewa, ili kugharamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa wagombea wa ngazi zote wa CCCM, alisema Mrema.
Wakati huo huo, vyama hivyo vimewaandikia barua mabalozi wote wa nje wanaoziwakilisha nchi zao vikiwaunga mkono kwa kufuatilia matumuzi ya fedha za misaada zinazotolewa na serikali zao.
Hatua hiyo inatokana na onyo la Waziri Membe kwa mabalozi hao alilolitoa mwishoni kwa wiki iliyopita akiwataka wasiingilie mambo ya ndani ya nchi.
Katika barua yao hiyo, vyama hivyo vimeeleza kusikitishwa na kusononeshwa na vitisho vilivyotolewa na Waziri Membe kwa mabalozi hao ambao wameonywa kuacha kuzungumza wazi wazi kuhusu tuhuma za ufisadi na kashfa nyingine zinazoiandama serikali.
Barua hiyo inaeleza kuwa nchi za Ulaya na Marekani ambazo balozi zao zimekemewa na Waziri Membe zinatoa zaidi ya asilimia 40 ya fedha za maendeleo ya bajeti ya Tanzania kwa kila mwaka, na pia kulipa madeni pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa Serikali ya Tanzania.