Wapinzani wanaitaka Demokrasia wakati wao wenyewe wanashindwa Kui-practice

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Mimi sio mwanasiasa ni mchakata Viazi tu kuwa chipsi hapa kitaani kwetu,
Lakini licha ya kutokuwa mwanasiasa haifanyi Nisiifatilie siasa kwa sababu ata hicho ninachokifanya kipo ndani ya hesabu ya wanasiasa,("Mmiliki wa kiwanda kidogo cha uchakataji kwa mujibu wa takwimu za Viwanda")


Nirudi kwenye mada "Wapinzani wanaitaka Demokrasia wakati wao wanashindwa Kui practice"

Kwanza Niseme wazi Sijaisoma Katiba ya Chama kikuu cha Upinzani (CHADEMA), lakini ata kama sijaisoma Sitaki kuamini kwamba KATIBA yao haina Ukomo wa Uongozi kwa ngazi ya Mwenyekiti kwa maana ya mihula ya Kiungozi,
Kama kweli haina basi ni kosa kwenye Katiba yao waandishi walikuwa wanajitazama Wao zaidi kuliko wengine,

Upinzani unatakiwa ujue kwamba ata Jumuiya ndogo ndogo za kanisa(Roman Catholic ) Zina Ukomo Wa Uongozi,
Mwenyekiti wa jumuiya yeyote hapaswi kuongoza zaidi ya mihula mitatu, na kila muhula wa uongozi ni miaka 3,hii ina maana uongozi wake utadumu kwa miaka 9 pekee na haiwezi kuzidi hapo ata kama anapendwa na wanajumuiya wenzake.

Kama tu kanisa linapractice Demokrasia kwa kiwango kikubwa hivyo kwa nini Vyama vya Upinzani vinashindwa Kuipractice,
Wanaililia Demokrasia wakati wanashindwa kuifanya wao kwa Vitendo,

Kwa Umri wangu mdogo kuanzia pale nimepata ufahamu wa kutambua mambo baadhi huwa nasikiaga tu,
Lipumba ni mwenyekiti, Dovutwa ni mwenyekiti, Mbowe ni mwenyekiti, Mrema Ni mwenyekiti na N.k

Mpaka sasa sijasikia mwenyekiti mstaafu wa Chama flani cha upinzani akaribishwa Ofisini na mwenyekiti wa sasa kujadili mambo kuhusu kukijenga chama chao,
Sijawahi na sijui lini nitasikia kutoka kwa Vyama vya Upinzani,.

Uongozi ni kubadilishana Vijiti, leo weka wazo lako, kesho toka na mwenzio aweke wazo lake,
Wewe waweza ulikosea mahala lakini anapokuja mwingine anaweza kurekebisha pale ili mambo yaweze kwenda,

Hauwezi kuwa kiongozi Daima, hauwezi kujiona wewe tu pekee ndio unafaa kuongoza hakuna wengine,
Ukishakuwa na mawazo ya Aina hiyo huo ni Ubinafsi na Kamwe hatuwezi kusonga Mbele.



Cc Zero IQ
 
Kwakweli upinzan nchi hii sijui wana kwama wapi tu yaan

Nashindwa kuwaelewa
Inaonesha wenyeviti ni wakubwa kushinda vyama vyao

Maana hata wafuas wanadai akitoka huyu mwenyeketi akija mwingine atanunuliwa na CCM

Sijui wao ni Malaya wakununuliwa kwa soda na kiepe
 
Kwakweli upinzan nchi hii sijui wana kwama wapi tu yaan

Nashindwa kuwaelewa
Inaonesha wenyeviti ni wakubwa kushinda vyama vyao

Maana hata wafuas wanadai akitoka huyu mwenyeketi akija mwingine atanunuliwa na CCM

Sijui wao ni Malaya wakununuliwa kwa soda na kiepe
Hiyo inashangaza kwa kweli,
 
Kwakweli upinzan nchi hii sijui wana kwama wapi tu yaan

Nashindwa kuwaelewa
Inaonesha wenyeviti ni wakubwa kushinda vyama vyao

Maana hata wafuas wanadai akitoka huyu mwenyeketi akija mwingine atanunuliwa na CCM

Sijui wao ni Malaya wakununuliwa kwa soda na kiepe
Nadhani mnashindwa kuelewa Jambo mapambano yoyote yanahitaji uvumiliv na consistency wapinzani bado wako kwenye mapambano Sasa unataka waweke watu wengine ili kilasiku wawe wapya kwenye mapambano wakisha ingia madarakani katiba inasema wazi urais Ni awamu mbili haiweze kutokea Hilo unaloliwaza Sasa mbowe wapi amezuiwa kugombea uenyekiti? Ccm haijawahi kuwa bench inawezekana nao wangekuwa Kama hivyo kwenye kupambana kuingia madarakani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom