Wapinzani Wanafadhiliwa Na "mtu Anayetaka Urais 2010"

Apr 27, 2006
26,588
10,374
WAPINZANI WADAIWA KUFADHILIWA NA "MTU ANAYETAKA URAIS 2010"

BY: Reuben Kagaruki
Source: Majira, ISSN 0856-5086, # 50009 VOL. 11/3019



Vyama vya upinzani vinne vilivyoanzisha umoja hapa nchini, TLP, NCCR-Mageuzi, Chadema, na CUF, vinadaiwa kufadhiliwa na mfanyabiashara mmmoja maarufu hapa chini, mwenye malengo ya kugombea urais mwaka 2010, ili viongozi hao wazunguke nchi nzima kama wanavyofanya sasa katika kumuwekea mambo sawa kisiasa. Habari hizi zimetolkewa na vyonbo mbali mbali vya habari hapa nchini, hivi karibuni.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa TLP, Mrema, alikana tuhuma hizo na kusema kuwa wao wanafanya kazi ya kuwaamusha wananchi wapate hasira takatifu na waonfdokane na ondondocha unaowafanya wanyamaze kimyaa, huku nchi ikitafunwa na kikundi cha wachache. Alisema kuwa mbali na kutumia helikopta, ikiwezekana watatembea kwa miguu au mikokoteni kueneza hasira hizo kwa wananchi, wakigomee kikundi cha wachache wanaowaibia na kuendeleza ufisadi.

Mrema, alipobanwa zaidi amtaje mfadhili huyo, alisema ni mapema mno kusema kuwa kuna mtu au mfadhili, sisi hatuna hela za bangi, rushwa, wala madawa ya kulevya, kama kuna mtu mwema ajitokeze na atusaidie. Alipoulizwa kwamba wamepata wapi hela za ghafla za kuweza kukodi helikopta, alisema "...Nimegundua gaharama za kuendesha shangingi ni kubwa mno kuliko helikopta, kwa mfano tulipokwenda Songea na Rukwa, tulitumia hela ndogo sana kuliko tungetumia gari..."
 
nadhani kuna post yangu moja jana nilisema wapinzani wanafanya hivi kwa kuweka mbele zaidi interest zao binafsi ! na hapo hapo wanatumia chance nzuri waliyonayo kuwafunga macho watanzania walio wengi, mfanyabiashara na siasa wapi na wapi ? huyo anataka kuendeleza ze biznesi yake ikulu ! sasa angalia kabila lake hapo na angalia chama flani flani ndio utajua !

sina maana ya kuleta ukabila *
 
CCM wanakula na Mengi huku nyuma wanamzunguka kwa maneno ya pembeni.

Akiwapa wao pesa sawa lakini akitoa upinzani matatizo.

Nimesikia toka 1990 kwamba Mengi anataka kugombea urais na sasa miaka 17 hajawahi hata kuchukua forms.

Hata kama anataka kuwa rais, atakuwa rais wa maana zaidi kuliko hao akina JK na Mkapa. Jamaa angalau ameshasaidia kuwatengenezea Watanzania ajira kibao.

Sasa huyu mbunge wa Chalinze/Bagamoyo ambako maendeleo ya watu wa kawaida yako chini sana, kama ana uwezo, alipokuwa mbunge si angenyanyua kidogo maendeleo ya jimbo lake?

Vile vile Njomba kule Mtwara, mambo ni mabaya mno.

Watu ambao wameshindwa kuleta maendeleo kama Wabunge naona kwa kweli hawafai kabisa.

Waache kumwandama Mengi ambaye mimi namwita ni shujaa wa Watanzania.
 
Huyu mengi Ipp media mzozo ataweza kututawala?

Hivi pale Ikulu kuna nini? huyu nae....(kama ni yeye)

Mmetawaliwa na JK, Mengi atashindwa kweli?

Sidhani kama Mengi anataka kuwa rais. Ni CCM wanamtumia tu ili kujibu mapigo ya wapinzani.
 
kama tumetawaliwa na watu wenye I.Q ndogo hivyo na tukatawalika nadhani kama mengi, mtu mwenye I.Q kubwa atagombea atakuwa amefanya jambo la maana sana tangia nchi hii ipate uhuru.
 
I don't care nani anafadhili nini, ninacho jali upinzani wanafanya wanachotakiwa check and balance. I'm sure now JK na cabinet yake wanakuna vichwa sasa. More to come.
 
We need that Cat who can catch the rats/mice; whether black or white; overall CCM are worst than dogs and pigs! At that time CCM will join the opposition to oversee as to what opposition is doing now! Tanzania ni nchi ya wote ambao ni Watanzania! Siyo nchi ya CCM peke yake!
 
CCM wanakula na Mengi huku nyuma wanamzunguka kwa maneno ya pembeni.

Akiwapa wao pesa sawa lakini akitoa upinzani matatizo.

Nimesikia toka 1990 kwamba Mengi anataka kugombea urais na sasa miaka 17 hajawahi hata kuchukua forms.

Hata kama anataka kuwa rais, atakuwa rais wa maana zaidi kuliko hao akina JK na Mkapa. Jamaa angalau ameshasaidia kuwatengenezea Watanzania ajira kibao.

Sasa huyu mbunge wa Chalinze/Bagamoyo ambako maendeleo ya watu wa kawaida yako chini sana, kama ana uwezo, alipokuwa mbunge si angenyanyua kidogo maendeleo ya jimbo lake?

Vile vile Njomba kule Mtwara, mambo ni mabaya mno.

Watu ambao wameshindwa kuleta maendeleo kama Wabunge naona kwa kweli hawafai kabisa.

Waache kumwandama Mengi ambaye mimi namwita ni shujaa wa Watanzania.

Mtanzania
Inaonekana wewe hujui ajira ambazo muungwana ametengeneza kama alivyoahidi, we njo dar utaziona, mojawapo ambayo ndo maarufu sana ni ile ya kuokota chupa za maji ya kunywa. Utawakuta vijana, wazee wanapita kila sehemu ya jiji kuokota chupa na bei ni sh 150 kwa kilo huko wanapoziuza. Inaitwa ajira ya JK
 
Mtanzania
Inaonekana wewe hujui ajira ambazo muungwana ametengeneza kama alivyoahidi, we njo dar utaziona, mojawapo ambayo ndo maarufu sana ni ile ya kuokota chupa za maji ya kunywa. Utawakuta vijana, wazee wanapita kila sehemu ya jiji kuokota chupa na bei ni sh 150 kwa kilo huko wanapoziuza. Inaitwa ajira ya JK

Hiyo sio ajira Judy,ni utani wa rejareja,hapo kilichotakiwa kufanyika ni kuelimisha jamii ya kitanzania kujali mazingira yao,kutochafua mazingira.Unajua usafi ni utamaduni katika jamii,nakupa mfano,Japan mtoto ataanza kufundishwa somo la usafi wa mazingira toka akiwa mdogo,ndio maana hata mtoto wa miaka 3,ukimpa pipi,baada ya kuimenya hiyo karatasi haitupi hovyo hadi atafute dust bin,na kama halipo jirani,ataiweka mfukoni,hadi atapolipata ndio atupe.Huwezi kusema kuokota chupa za maji ni ajira,hiyo si ajira bali ni mchezo wa kuigiza.Ajira ni viwanda,biashara,ufundi,kilimo,ufuagaji,na sio kuokota chupa.
 
Kama lengo la Mengi ni kugombea urais mie simshauri kufanya hivyo,nadhani anaweza kutoa mchango mkubwa sana katika jamii yetu bila hata ya kuwa rais,awe kama akina Bill Gates.Ikulu ni mzigo,si mahali pa kukimbilia,kama alivyosema Mwl Nyerere,mtu mwenye akili timamu hakimbilii ikulu,namuona Mengi kama mtu mwenye akili timamu,sidhani kama atapenda kwenda ikulu,pale hapafai,ni mahali pa majungu.Kama ni mali unayo bwana Mengi,kama ni umaarufu unao,huna haja ya kwenda kutafuta lawama pale ikulu.
 
Mtanzania
Inaonekana wewe hujui ajira ambazo muungwana ametengeneza kama alivyoahidi, we njo dar utaziona, mojawapo ambayo ndo maarufu sana ni ile ya kuokota chupa za maji ya kunywa. Utawakuta vijana, wazee wanapita kila sehemu ya jiji kuokota chupa na bei ni sh 150 kwa kilo huko wanapoziuza. Inaitwa ajira ya JK

Looh! Judy kama hizo ndio ajira alizoahidi JK basi tuna kazi kubwa.

Zaidi ya watanzania 30M wako mikoani, je na huko kawapelekea nini? Je hao wa Dar wangapi wanafaidika na kuokota hizo chupa? Na kwa kipato gani?
 
Bro J4 na Mtanzania,
Huo ndo utani wenyewe haswaa, kwa vile so far hakuna ajira yoyote tuionayo kwa macho sie wabongo na hata plans zenyewe za kutengeneza ajira so far hazipo, tutamfikiriaje muungwana? Its a shame yani we acha tu.
 
Tuache kutenda hii dhambi ya kumsingizia mzee wa watu jamani,

Ila nililojifunza hapa ni kuwa ccm wanamwogopa Mengi kwa sababu ama ni msafi kuliko hao wafanyabiashara wengine, ama yeye anaweza kuwa smart zaidi yao.

Kama wanaweza kuwa na pesa za mafisadi wote hao halafu leo wanamwogopa mfanyibiashara mmoja huu ni ujumbe kuwa kumbe ccm haina mtandao kama wanavyodai wao ila ni genge la wahujumu uchumi ambao kila kukicha wanamtaka kila mtu awe miongoni mwao iloi waweze kumshirikisha kwenye uchafu wao na ashindwe kusema wazi juu ya uchafu wao.

Mwacheni Mengi, Acheni wapinzani kwani huwa wanajitesa sana mpaka kupata fedha kwa ajili ya ziara hizo wanazofanya.

Ingekuwa ni kweli watu kama wakina Akwilombe na wenzake wangeshasema huko ccm kuwa ni nani anawapa pesa wapinzani ila kwa vile wanajua kuwa wapinzani wanachangishana basi wamekuwa hawana la kusema ama kuwalaumu watu uongo.
 
JK yuko karibu sana kuweka historia ya kuwa "President who promised alot, and ended up in travelling alot and delivered nothing"
Anaysema Judy ndio kweli. Sasa hivi kama ukitaka kupata ajira ya maana uwe mtu wa fitna kama Salva Rweyamamu, kupikia majungu wengine, ajira nyingi anazotoa ni hizo za watu kuokota viatu vilivyokwisha na chupa, lakini kweli aliyoahidi hakuna hata moja lililotekelezwa mpaka sasa, hakuna hata dalili.
 
Mimi nafikiri the question at hand ni kwamba how far mwananchi as mwananchi wa Tanzania can do, katika kuchangia kulisaidia taifa lake, katika nchi kama yetu Tanzania, where all the power is centered kwenye executive branch,

Wananchi tulitakiwa ku-fall kwenye Parliament branch, lakini reality ni kuwa hicho chombo kimegeuka kuwa toothless au rubberstamp ya executive branch, na kutunyang'anya wananchi the power ya kui-check executive branch, huku Judicial Branch yetu imegeuzwa kuwa Banana Republic, Sasa in the wake of all this, ikiwa ni pamoja na a compromise meadia, je wananchi tutawakilishwaje kwenye kuhakikisha kuwa serikali yetu ni fanctionable as it shopuld kulingana na katiba yetu?

Serikali yetu isilalamike wanapotokea wananchi waliochoshwa wenye uwezo wa kipesa wanapoamua kuwasaidia wake wenye nia ya kuirekebisha, ili itimize yale yaliyomo kwenye katiba yetu, unless wakidai kutaka kuiondoa madarakani serikali yetu na CCM, kinyume cha sheria, then tutaelewa wakilalamika, otherwise wasitafute njia za mkato za kujibu tuhuma nzito against baadhi ya viongozi wao, katika zile tuhuma hakuna siasa, kuna legal evidence zinazotakiwa kujibiwa mahakamani, sio majukwaaani. FULL STOP.

Katika nchi yoyote inayofuata The Rule of Law, kama yetu serikali au CCM, walipaswa ku-comeout na kusema kuwa kuna mfadhili anayewasaidia wapinzani kwa manufaaa yake ili aje agombee urais mwaka 2010, kwa kufanya hivyo mfadhili huyo na vyama hivyo vya upinzani, wanavunja sheria zetu one, two, three, and four, kwa hiyo ikibidi tutawafikisha mahakamani, anything less ni dalili tu za kutka kuigeuza ishu ya mafisadi kuwa ya kisiasa, badala ya kuwa kama ilivyo, yaani ya kisheria, lakini wananchi sasa sio wajinga tena, pia tunasikia kuwa baadhi ya viongozi wetu wa juu ambao hawaridhiki na uhuni unaofanywa na baadhi ya viongozi wenzao, tunasikia ndio waliohusika na kuvuja kwa mkataba wa Buzwagi, na aal the other infos za BOT, nasikia pia urafiki wa karibu wa Karamagi na Muungwana, ndio hasa chanzo cha yanayojiri maana kuna baadhi ya mawaziri sasa hivi wana-toast glasi zao,

Wananchi we real do not care how the changes will come about, hata kama it takes wivu wa viongozi against viongozi, tunachotaka ni serikali inayowajali wananchi na kuheshimu sheria zetu, the rest ya matatizo ya viongozi kwa viongozi wa CCM it is none of our bussines, lakini it becomes our bussiness kama yanasaidia kuvujisha mikataba mibovu ambayo ni hasara kwa taifa letu,

Kama kuna mfadhili, aendeleee tu unless kuna mahali kwa ufadhili wake, anavunja sheria zetu, serikali inpaswa ku-worry about viongozi waliotuhumiwa na sio habari za kampeni za urais wa 2010!
 
kusema kukweli hata kamamtu kama mengi anawafadhili upinzani kwa ajili ya kumuwekea sawa mambo kwa ajili ya kugombea uraisi mwaka 2010 ni afadhali ya yeye ambaye anaonyesha moyo wa kuwasaidia watanzania wengi katika upandfe wa viwanda kwani amewapatia ajira watanzania wengi sana kwenye makampuni yake.
 
Nina kaswali kadogo: Hivi ni dhambi gani au ni kosa gani kikatiba au ni tatizo gani kwa mtu binafsi kuamua kutoa pesa na kuusaidia upinzani?
Hivi CCM wanaposaidiwa na akina Azam,Mengi,Mohamed Interprise na hao magabachori wengine kibao mbona hawasemi???
Kwanini issue halali zinapokuja upinzani inakuwa taabu???
Au CCM wanahaki zaidi kuliko vyama vingine??Kama ndio kwa kifungu kipi cha sheria.
Denmark walikuwa tayari kutoa pesa kusaidia uwezo wa vyama vya upinzani,hawa wakuu wa CCM wakakataa, sasa wanataka nini!!!
 
Back
Top Bottom