Field Marshall ES
JF-Expert Member
- Apr 27, 2006
- 12,624
- 1,233
WAPINZANI WADAIWA KUFADHILIWA NA "MTU ANAYETAKA URAIS 2010"
BY: Reuben Kagaruki
Source: Majira, ISSN 0856-5086, # 50009 VOL. 11/3019
Vyama vya upinzani vinne vilivyoanzisha umoja hapa nchini, TLP, NCCR-Mageuzi, Chadema, na CUF, vinadaiwa kufadhiliwa na mfanyabiashara mmmoja maarufu hapa chini, mwenye malengo ya kugombea urais mwaka 2010, ili viongozi hao wazunguke nchi nzima kama wanavyofanya sasa katika kumuwekea mambo sawa kisiasa. Habari hizi zimetolkewa na vyonbo mbali mbali vya habari hapa nchini, hivi karibuni.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa TLP, Mrema, alikana tuhuma hizo na kusema kuwa wao wanafanya kazi ya kuwaamusha wananchi wapate hasira takatifu na waonfdokane na ondondocha unaowafanya wanyamaze kimyaa, huku nchi ikitafunwa na kikundi cha wachache. Alisema kuwa mbali na kutumia helikopta, ikiwezekana watatembea kwa miguu au mikokoteni kueneza hasira hizo kwa wananchi, wakigomee kikundi cha wachache wanaowaibia na kuendeleza ufisadi.
Mrema, alipobanwa zaidi amtaje mfadhili huyo, alisema ni mapema mno kusema kuwa kuna mtu au mfadhili, sisi hatuna hela za bangi, rushwa, wala madawa ya kulevya, kama kuna mtu mwema ajitokeze na atusaidie. Alipoulizwa kwamba wamepata wapi hela za ghafla za kuweza kukodi helikopta, alisema "...Nimegundua gaharama za kuendesha shangingi ni kubwa mno kuliko helikopta, kwa mfano tulipokwenda Songea na Rukwa, tulitumia hela ndogo sana kuliko tungetumia gari..."