mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Kuwa na madhumuni ya kuiondoa CCM madarakani ni njozi hafifu isiyo na faida kwa taifa.
Siasa za kujibanza kwenye matatizo na mapungufu ya Serikali au taifa hazina faida kwa Tanzania.
Hii imenipelekea kujifunza tofauti kubwa Kati ya watu weusi wawili maarufu duniani. Wote walikuwa wanapigania kitu kimoja(uhuru wa mtu mweusi) lkn kwa njia tofauti.
1:Malcom X aliamini katika kupigania haki kwa kuwekeza kwenye matatizo yaliyokuwa yanawasibu watu weusi. Muda mwingi alitumia kupinga uonevu, kuhamasisha vurugu pale mtu mweusi anapoonewa, kuhamasisha watu wasiamini haki za mahakama maana ziliwabeba wazungu. Njia hii ilikuwa sahihi lkn hakuwahi kuleta matunda. Watafiti wa mambo ya kisaikolojia waliosema njia hii inatumia sehemu ya chini kabisa ya uwezo wa ubongo wa mwanadamu.
2:Martin Luther King Jr, aliwekeza kwenye Kile wanachotakiwa kukipata watu weusi sio matatizo yanayowasibu. Aliwekeza kwenye njozi za kile kinachotakiwa kuwa bila kujali kitatokea lini. Watafiti wa mambo ya kisaikolojia wanasema alichokifanya Luther ni zoezi la kiubunifu lililojumuisha sehemu zote za Uwezo wa ubongo wa Mwanadamu. Tatizo linaondolewa kwa kuhubiri njozi unavyodhani ni suluhisho la kudumu la tatizo sio kueleza tatizo.
Japo wote wawili waliuwawa lakni ni njozi ya Luther inadumu hadi kesho huku harakati za Malcom X zikibaki kukumbukwa kama harakati tu ambazo matunda yake hayapimiki.
Wapinzani jifunzeni kwa Luther, matatizo hayaondolewi kwa kumsakama anayesadikika kuwa Chanzo cha tatizo, Kulaani Vitendo na mipango unavyodhani sio sahihi na ni kazi nyepesi sana Bali ni kuhubiri Bila kukoma wala kutoka kwenye mstari mna njozi gani na Tanzania ili watanzania wajue hawa watu tangu wamekuwepo wanataka nini.
Kuhubiri matatizo, hakutaisaidia Tanzania lkn Kuhubiri njozi hata Leo vyama vyenu vikifa vizazi vijavyo vitakuwa vinasimamia njozi hizo. Kelele za wapinzani masikioni mwa mtanzania ni matatizo yanayomsibu sio njozi yao kwa mtanzania masikini.