Wapinzani wamerudi nyuma miaka 20

kandamatope

JF-Expert Member
May 19, 2018
589
627
Mwaka 1992 Tanzania inarudisha mfumo wa vyama vingi
NCCR MAGEUZI ilikuwa na manguli wa siasa

Mpaka tunaingia katika chaguzi wa vyama vingi 1995 NCCR ilikuwa na watu wenye uwezo wa kuongoza dola na Taifa kwa ujumla

Baada ya hapo NCCR ikafa
Ikafuhatia CUF 2000 - 2005 Ilikuwa na watu wenye uwezo na ushawishi wa kushika dola
CUF nayo ikaja kufa
Ikafuhatia Chadema 2010 - 2015
Watu walikuwepo wenye uwezo wa kushawishi na kushika dola

Baada ya hapo Chadema nayo ndembe ndembe
2020 CCM haina mpinzani kabisa
Labda kwa upande wa visiwani angalau kidogo ACT wazalendo
Wakipewa dola kule Zanzibar watu wenye uwezo na ushawishi wa kushika dola na kuongoza serikali wanao na nchi itatulia bila wasi wasi wowote

Upande wa bara 2020 hakuna chama chenye wanasiasa bora na manguli wa kushika dola na kuiongoza
Ukweli ndio huo na ni lazima usemwe.

Siwaoni manguli wa siasa Chadema, wala CUF, wala NCCR mageuzi hata ACT upande wa Tanzania Bara hakuna ushawishi wowote wa kisiasa zaid ya harakati kama zile za kumpokea LISU kwa maandamano na kisha giza likizama na story imekufa

Unafanya harakati za kwenda kuaga mwili wa mzee mkapa kwa mbwembwe unazuiliwa kuingia uwanja wa Taifa kwa kutokufuhata protokali na story imekwisha
Hoja yangu 2020 wapinzani wametepeta mapema asubuhi tu...
Mwenye kubisha na abishe tu
 
Nyomi iliyo mpokea Lisu ni ishara kwamba watanzania wamemstukia mpenda kiki. Anajenga matuta barabarani halafu anayaita flyover.

Mpenda kiki ananunua magofu ya ndege (Terrible tins) kwa keshi halafu popo ndiyo wanafaidi. Watanzania wamemchoka kweli kweli. Lisu ndiyo habari ya kisiasa kwa Sasa.
 
Acha kutafta reply na views kwa kuandika vtu vya .......kama wamerudi nyuma mlifunga bunge live la nini why mlizuia mikutano yao ya ndani na nje why mliwatishia
 
Kwanza umesikia speech ya leo ya Kikwete kwenye mazishi ya Mkapa? Alafu mwambieni mpenda sifa wenu ajiandae kukabidhi ikulu hapo October 2020
 
Mtasema JK kajiunga Chadema. Maana nyie anayewapa ukweli anaitwa mwanasiasa wa hovyo toka Chadema
mbowejames_4-___CDOmiTsJuS0___-.jpg
 
Ni kweli, na wanaccm ni watoa rushwa kuanzia mwenyekiti wao ndio maana anapata kura 100% kama anaongoza makondoo. Hapo ndio ujue rushwa inapofusha.

Mwenyekiti wenu juzi kapata 99% huko hai, katoa sh ngapi na wale waliopiga kura 99% ni makondoo au ngurue wa moshi?
Na kuna mshabiki wenu alisema ilitakiwa ifike mia, kwa hiyo kwenu inapendeza ila kwa wengine sio poa.
Unaonyesha wazi uwezo wako wa ufaham ni mdogo sana.
 
Tofauti na NCCR&CUF,kifo cha CDM kitapelekea kudhoofu kwa upinzani wote kwa ujumla wake kutokana na siasa zao (CDM) za kijuha (za kupambana hadi na wapinzani wenzao)

Hili ombwe linainufaisha CCM zaidi kuliko CDM.
 
Lazima warudi kama kila kesi wanashtakiwa wao,mikutano wanakatazwa wao,kina Lisu wanapigwa risasi mchana kweupe,wabunge na madiwani wanaunga mkono kwa lazima
 
Nchi ndo imerudi miaka 200 nyuma.Sasa hivi siasa imekua ya upande mmoja tena ni kusifu na kuabudu.Hakuna tena hoja motomoto za kisiasa kama miaka ya hapo katikati,nasio kwamba hoja hakuna bali kuna watu wameamua tuishi hivi kibubu bubu.ukitaka kuongea upige magoti nakusujudu ukitoa hoja umesimama wanakwambia unatumika na mabeberu.
 
Back
Top Bottom