Wapinzani wamekuwa wapiga ramli kwa kutoa matamko yasiyokuwa na msaada kwa wananchi

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
10,490
13,551
Utasikia matamko ambayo hayasaidii kutatua kero
  1. Wanashutumu serikali ambayo inatatua kero za wananchi
  2. Wanashutumu bunge linalofuata sheria
  3. Wapinzani hawaendi majimboni kwao, wapo tu dar kuhangaika na kesi
  4. Wanaishi dodoma lakini hawaingii bungeni
  5. Hawajui mpaka sasa wakienda majimboni watawaeleza nini wananchi
Kwa ufupi wapinzani hawajitambui!
 
Be the first to reply

Unataka wafanye kipi maana lengo limetimia kwa kubadili gia angani.Tulihubiri uovu na madhara ya ufisadi JPM kateka mada na anatekeleza.Muda wa kuzungusha mikono kauzuwia,tutawaambia wapiga kura wetu tumezuwiwa kuzungusha mikono na Tulia anatunyanyasa bungeni.
 
Kama wewe unadhani ndio raia pekee wa nchi hii basi wahamishe hao wapinzani uwapeleke pale unapohisi wanastahili kupaza sauti.


Funga domo hilo.
 
Utasikia matamko ambayo hayasaidii kutatua kero
  1. Wanashutumu serikali ambayo inatatua kero za wananchi
6. Wanalalamika kupanda kwa kodi na bei ya bidhaa muhimu wakati wananchi wenyewe hawalalamiki kwa kuwa serikali inatatua kero zao
 
Ngoja 2020 watatutambua manaake haiwezekani tuwatume wakatuwakilishe then waishie kuwa Watoro kwenye majukum yao ya Msingi ya kutuwakilisha....Ngoja waendekeze siasa zao zenye mlengo wa kutafuta Public Sympathy, they should know we are no longer interested with Cheap politics.....Wakatimize ahadi zao Majimboni
 
Ngoja 2020 watatutambua manaake haiwezekani tuwatume wakatuwakilishe then waishie kuwa Watoro kwenye majukum yao ya Msingi ya kutuwakilisha....Ngoja waendekeze siasa zao zenye mlengo wa kutafuta Public Sympathy, they should know we are no longer interested with Cheap politics.....Wakatimize ahadi zao Majimboni
2020 ni mbali, subiri kidogo tu uchaguzi wa serikali za mitaa ndiyo ulevi utawatoka
 
Chadema kimbilio la mafisadi na majizi.

Watu wanaotoa lugha chafu mtandaoni kimbilio lao ni chadema kwenda kuchangiwa pesa .!!!!
 
Ndugu mtoa mada, ningekuwa nakufahamu ningekupa zawadi japo kidogo. Watu hawa wanaojiita wapinzani ki ukweli kabisa wameishiwa sera na hawana jipya.

Mheshimiwa rais Magufuli amewamaliza ndiyo maana hawana cha kuongea zaidi ya kuongea utumbo utumbo tu kila siku ili waonekane kwenye vyombo vya habari.

Watanzania wamemkubali rais Magufuli na wanaendelea na shughuli zao za kila siku bila matatizo yoyote, lakini wao (wapinzani) wanajaribu kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali iliyopo madarakani kwa kumwita rais Magufuli ni dictator ingawa hata sifa za u dictator hawazijui, zaidi sana wananchi wameshawapuuza kwa kiwango cha hali ya juu.

Wapinzani wakitaka kuonekana mimi nawashauri waende mitaani kutafuta shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI, NAOMBA UWAPUUZILIE MBALI WOTE WENYE MAWAZO YA KIPUUZI JUU YAKO. SISI WATANZANIA TUNAONA NA TUNATHAMINI KAZI NZURI UNAZOZIFANYA. MUNGU AKUBARIKI SANA. AMINA.
 
Ameshindwa uji na chai ataweza tanzania
Ni vichaa wa ccm ndo wanashangilia
Tatizo ni mental emmition disorder ma autistic mko wengi sana
 
Utasikia matamko ambayo hayasaidii kutatua kero
  1. Wanashutumu serikali ambayo inatatua kero za wananchi
  2. Wanashutumu bunge linalofuata sheria
  3. Wapinzani hawaendi majimboni kwao, wapo tu dar kuhangaika na kesi
  4. Wanaishi dodoma lakini hawaingii bungeni
  5. Hawajui mpaka sasa wakienda majimboni watawaeleza nini wananchi
Kwa ufupi wapinzani hawajitambui!
Ni kweli kabisa Mkuu. Hata hawajielewi waligombea ubunge kwa ajili gani!
 
Ameshindwa uji na chai ataweza tanzania
Ni vichaa wa ccm ndo wanashangilia
Tatizo ni mental emmition disorder ma autistic mko wengi sana

Uji na Chai wanalilia watoto wa mama au wanaokula kwa baba.Ukiwa mtu mzima uji na chai si habari kubwa.Kuna wanaofungua kinywa kwa kupata dona na mboga zake. Uji ni ziada.Jenga hoja zaidi ya ongezeko la bei ya sukari la muda wa miezi 2.Ikifika Septemba 2016 ukakuta bei ya sukari imeshuka utasemaje?

Je bei ya mchele,mahindi,sabuni mahali ulipo ikoje? Michango ya shule kwa huduma za mitihani,ulinzi ikoje?Huduma za afya kijijini ulikotoka au walipo ndugu zako ikoje? Kama huduma hizi zinaendelea kuwa dhaifu JPM kalikoroga,ukiona zinaendelea kuimarika na raia wanaridhika kuzungusha mikono si hoja tena.

Wapo wanaolalamika mafisadi papa hawakamatwi wanaonewa wanyonge.Swali langu kwao ni hili mnasemaje kwa waendesha boda boda na hawana liseni,matokeo ya ajali nyingi za boda boda zina faida au madhara? je ni busara kuacha watoto wetu na wadogo zetu wacheze pool asubuhi? wakusanyane vujiweni na kusubiri neema ya mafanikio kwa kusimuliana matokeo ya ligi za ulaya,visa vya Diomond na Wema kuanzia asubuhi hadi jioni.

Wasipokuwa na cha kufanya tuilalamike serikali kwa kutowapa ajira? Natamani kuijua nchi moja Ulaya ambayo mzazi alilala usingizi tu na serikali ikawaandalia watoto wote wa nchi hiyo kupata fursa sawa za kufanikiwa.

Nikiangalia na kupitia mijadala yetu huwa ninajiuliza hawa tunaosema wamebebwa iwe wapo CCM au CHADEMA na CUF kuna familia ambayo baba,mama,watoto wote na wajukuu wana vyeo bila vyeo bila kujali uwezo na juhudi za kila mmoja wao?

Ninasikiliza Marekani ambako baadhi yetu hudhani ni kielelezo cha demokrasia inakuwaje akina Bush wawili waongoze nchi? na bado Bush watatu kagombea.Bill Clinton kawa rais wa Marekani sasa mkewe anagombea na aweza kuwa rais wao ingekuwa hayo yametokea Tanzania tungesemaje?
 
Back
Top Bottom