Wapinzani walidhani ripoti ya CAG itawapaisha lakini wameambulia patupu. Sasa wanatakiwa wasiwe wanakurupuka

Huwa mnazungumzia watanzania gani? Marehemu Shujaa alisema kuwa wabunge wengi hawakuchaguliwa na wananchi, na Lusinde karudia kuwa wapo Bungeni kwa UBAVU wa Shujaa!

Wekeni free and fair election muone rangi halisi ya watanzania kuhusu CCM na Shujaa.

Kuhusu ripoti ya CAG ni sindano kwenye kalio la CCM, inachoma mno msijitikise itakatikia ndani.

Kichere kaongezewa ulinzi kwa kuwa mnataka kumdhuru.
Asante sana mkuu kwa kumaliza kazi ya kuwafunga midomo hao ma sukuma gang
 
Afu Nyie CCM legacy ya mtu huwa haihubiriwi kama neno la Mungu kila jpili..acheni hii kitu
 
Mtoa hoja una matatizo ya uchoyo wa ukweli,mbaguzi mkubwa,na unafiki mkubwa,wapinzani wote ni watanzania na ni haki yao kuongea na hii nchi sio ya ccm ni nchi ya sisi wote pamoja na utofauti wetu wa kiitikadi(ni haki iliyomo kwenye KATIBA)acha kujifanya una hati miliki ya nchi hii na uoga wa ccm upo wapi?kama wanajiamini tell them to level the playing field halafu wananchi waamue nani anasitahili kuongoza nchi yetu.
Hao ndiyo wenye kundi linalo pigana kuhakikisha wanapandikiza watu wao kwenye utawala wa mama Samia ili kuendeleza ukatili wao.
 
Mantiki ya kisiasa ya wapinzani wa kisiasa hapa Bongo hasa ACT wazalendo na Chadema kuwa ikitokea kuna suala fulani ndio iwe upenyo wa kupata kick za kisiasa sasa hivi halina nafasi tena. Maana watanzania wanafanya mambo yao kwa kutumia busara.

Huwezi ukawq upo Dubai umejifungia na kudhani ukijiliza kuwa kuna ufisadi au ulilipishawa kodi bil mbil ndio sababu ya kupata kick ya kisiasa.

Huwezi kukakamaa kwenye makamera ukikomaa kulazimisha hoja za ukaguzi wa CAG kuwa tayari ni undhirifu wa tril 3.6 huku ukidhani watanzania ni wajinga huku unapayuka mpaka shati linalowana kwa jasho la ukwapa kwa kudanganya watu kuwa mafuriko ya Morogoro na Rufiji yalisababishwa na ubovu wa bwawa la stieglers.

Huu sio wakati wa kuwapanda vichwa watanzania.
walimchukua lowasa pia wakaambulia patupu
 
Rais wa moyo wangu na mioyo ya watenda haki Mh. mama Samia kuna mahali amekosea au amekoseshwa na sasa naona kama kuna watu wanataka kumpanda kichwani kwa mgongo wa rais aliyetangulia mbele za haki . Wanasahau kuwa Dola iko chini ya amri ya mama Samia ambaye ni Mkuu wa Nchi.

Mh .Rais wa awamu ya sita ni mama Samia .
Kosa kubwa alilofanya ni kukubali kupangiwa baada ya kuapa. Alipaswa avunje baraza la mawaziri haraka sana. Ili waovu wajitenge na wema wawe huru. Huwezi kuchanganya giza na nuru.
Kuna watu bado wanaota kuwa Rais wa awamu ya tano bado ana mamlaka huku duniani.
Wanaota ndoto mbaya sana na huenda wakashikwa na wenda wazimu wasiposhikwa na kuambiwa kuwa wanaweweseka na jinamizi la matendo yao maovu waliyokuwa wanayafanya na waliyokuwa wamekusudia kuyafanya.

Kuna Genge ovu sana limethibitika wazi kuwa hawakua wanaipenda na kuitii serikali na katiba bali walikua kwa malengo na fadhila za mtu na sio taifa.

Mama Samia afanye hima apangue safu ya Awamu ya tano na atakayeleta chokochoko kuvuruga usalama wa nchi asisite kuwapa maagizo vyombo husika vifanye kazi yake.
Hapa hakuna cha uhuru unaoweza kuvuruga amani ya nchi. Nadhani hatua dhidi ya wachochezi zichukuliwe mapema sana na ikiwezekana hatua kali kama za wasaliti wakati wa vita.

Genge hilo lisiachwe likaeneza sumu nchi nzima italigharimu taifa letu na kumchafulia mama yetu Samia mtu mwema na mwadilifu ambaye hana ubaguzi wala ukabila wala hajajilimbikizia mali wala hajapora mali za umma.

Chukua hatua Rais. Futa hao wasidizi wako wote uchague timu itakayokutii na kuilinda katiba na sheria za nchi. Waliopo walizoea kutishwa na kuendeshwa kwa mjeledi kama punda hawajui ustarabu na utu. Wataeneza propaganda zao mana wengi ni zao la urafiki,udini,ukanda na ukabila ,watajipenyeza huko huko kukuvurugia ndoto zako. Kifo cha mtu mmoja hakiwezi kuwa ndio mwisho wa utawala wa sheria na mamlaka ya urais Tanzania .
Mh. Rais usiwe na huruma na mtu anayekuonyesha dharau yoyote. Fyekelea mbali . Hakuna mtu mkubwa kuliko nchi hii. Ni zamu ya kumtii na kumwimbia nyimbo za xa hamasa na maendeleo mama Samia . Asiyetaka asipewe nafasi ya kueneza fitina mapema hivi.

Vyombo vya dola navyo sasa vimsaidie Rais kwa kuwakamata na hata kuwa tupa ndani na kuwafilisi wale walionufaika na awamu ya tano kifisadi halafu wanatoa maneno ya kichochezi na kumdharau Rais wetu mpendwa.

Wasaliti sio wapinzani bali ni Wale walioko ndani ya serikali na chama tawala wanaoleta chokochoko .

Hata wao wakati wanamtukuza yule aliyepita hawakuruhusu watu wamkejeli hasa ndani ya chama na serikali.
Kumheshimu Rais wa nchi ni muhimu sana na wakati mwingine ni lazima.
 
Akili za MATAGA bana shida sana badala kusikiti ripoti ya CAG no kama watch dog penye uthaifu mjishihishe unaanza kuifikiria CDM hopeless kabisa inawezekana huyu no msomi
Ndiyo wasomi wanao furahia mawazo ya kina kibajaj na msukuma kuwa std 7 wana uwezo kuwashinda wenye phd
 
Tulikubaliana upinzani umekufa. Kwa kudhirisha hili bunge ni 98% sisiemu, serikali za mitaa ni 100% sisiemu.

Hao wapinzani mnaowazungumzia na kuwaambatanisha na taarifa ya mkaguzi ni wapi?

Tutambue jambo moja upinzani ni upingwaji wa uonevu na kila aina ya ubaya atendewayo mtu. Upinzani ni zao la kutotendewa haki za wazi wazi au za vificho ila matokeo huonekana. Upinzani sio chama au taasisi au mtu. Hawa hua ni kielelezo tu cha kuongoza upinzani wa watu. Wapo wapinzani wengi waliuawa na watawala wakiamini ndio chanzo cha wao kupingwa ila baada ya muda upinzani hurudi pale pale na yamkini mara nyingi huweza kurudi kwa kasi.

KUUMALIZA UPINZANI.

TENDA HAKI.
Salaam zimewafikia mataga
 
Ndiyo wasomi wanao furahia mawazo ya kina kibajaj na msukuma kuwa std 7 wana uwezo kuwashinda wenye phd
Acha ubwege wako, jikite kwenye mada acha kutafurta msaada kwenye tuta.
 
Ripoti ya CAG kama haijawapaisha wapinzani basi imewapiga kabari na pingu za miguu maccm! Ndio maana unasikia maCAG wote wawili Assad na Kicheere wanatishiwa maisha! Ina maana mpaka sasa hivi timu ya CAG/ Wapinzani 3 Maccm na serikali yao wana -ve0!!!
Of course wewe ni mataga huwezi kuiona hiyo hesabu ndefu na darasa lako la kayumba!
Alafu mataga wengi wao ni raia wa nchi jirani
 
Tulikubaliana upinzani umekufa. Kwa kudhirisha hili bunge ni 98% sisiemu, serikali za mitaa ni 100% sisiemu.

Hao wapinzani mnaowazungumzia na kuwaambatanisha na taarifa ya mkaguzi ni wapi?

Tutambue jambo moja upinzani ni upingwaji wa uonevu na kila aina ya ubaya atendewayo mtu. Upinzani ni zao la kutotendewa haki za wazi wazi au za vificho ila matokeo huonekana. Upinzani sio chama au taasisi au mtu. Hawa hua ni kielelezo tu cha kuongoza upinzani wa watu. Wapo wapinzani wengi waliuawa na watawala wakiamini ndio chanzo cha wao kupingwa ila baada ya muda upinzani hurudi pale pale na yamkini mara nyingi huweza kurudi kwa kasi.

KUUMALIZA UPINZANI.

TENDA HAKI.
Upinzani kufa ni kukosa uhai, ila vyama vya upinzani vipo,tumia akili kupambanua mambo.
 
Repoti ya CAG ni nzuri mnoo kwa upinzani ndio maana CCM wanashikana uchawi huko bungeni.

Na naomba CCM waendelee hivi hivi kulumbana ili ikifika 2025 wasiwe na mawazo mamoja ya kutuibia kura. Uchaguzi wa 2020 ilikuwa ni mtu mmoja ali archestrate mpango mzima wa wizi. Safari hii labda wawatumie ma LY waje mbele kuiba kura lakini tutawatoa nduki.
 
Back
Top Bottom