Wapinzani wakubali Lowassa kushushwa

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,307
6,514
Wanasiasa wa vyama vya upinzani nchini wamekubaliana na matokeo ya utafiti unaoonyesha Rais John Magufuli ameongezeka umaarufu hadi kufikia asilimia 74.5, huku mpinzani wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Edward Lowassa akishuka hadi asilimia 20.1.

Dk Magufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, akipata asilimia 58.47, ukiwa ni ushindi mdogo kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akizichukua tangu alipoapishwa Novemba 5 mwaka jana. Utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Ms Infotrak Research and Consult na Ms Midas Touche East Afrika na kuwahoji watu 1,200 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika kanda sita na mikoa 15 unaonyesha Rais Magufuli ameongezeka umaarufu kwa zaidi ya asilimia 20, huku Lowassa akishuka kwa asilimia 20.

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alisema ikiwa utaitishwa Uchaguzi Mkuu leo, Rais Magufuli ataongoza na kumuacha mbali Lowasa. Zitto alisema harakati zake za utumbuaji ‘majipu’ na kupambana na ufisadi, vimemfanya ajulikane zaidi na hivyo kuongezeka kwa umaarufu. “Jambo hili si jipya kwa sababu yeye (Magufuli) yupo madarakani, lakini Lowassa hayupo madarakani na alizuiwa hata kufanya mikutano,” alisema. Hata hivyo, aliponda ‘aina ya utumbuaji majipu’ kwa madai kuwa hawezi kuongoza nchi ikiwa Serikali haitaboresha mfumo wake wa utawala. “Lazima aboreshe mfumo kwani licha ya hayo kufanyika, hata tukiangalia gharama za maisha bado zipo juu, bei ya vyakula kama sukari na mchele havijabadilika tangu alipoingia madarakani licha ya kufanya mambo kadhaa,” alisema.Hata hivyo, alipongeza Wizara ya Elimu kwa kutekeleza sera ya elimu bure, huku akisema wizara nyingine nyingi, kama ya maji bado hazijafanya kitu.

Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba naye aliukubali utafiti huo, akisema kuongezeka umaarufu kwa Magufuli kunatokana na hatua nzito alizochukua katika kipindi kifupi alichokaa madarakani. Profesa Lipumba alisema vitu vilivyompaisha zaidi ni hotuba aliyoitoa bungeni mjini Dodoma, ubanaji wa matumizi ya Serikali ikiwamo kuzuia ziara holela za nje, kuwabana mafisadi na ukusanyaji wa mapato. Hata hivyo, alisema Serikali haiwezi kuendeshwa kama zimamoto na kusisitiza kuundwa kwa mfumo ambao utakuwa msingi wa utendaji kazi zake. “Pamoja na yote nimeona baadhi ya mawaziri na watendaji wakifanya kazi kwa kufuata matukio na matumizi ya vyombo vya habari. Nchi haitaweza kuendeshwa kwa mtindo huu,” alisema.

Kuhusu safari za nje kwa kibali cha Ikulu, Profesa Lipumba aliunga mkono ubanwaji wa matumizi, lakini akapinga Ikulu kuwa watoaji wa vibali vya safari hizo. “Inawezekana kukawa na safari ya kuangalia matumizi mabovu yanayohusu Ikulu yenyewe, itawezaje kutoa kibali hapo? Kuwe na mfumo utakaodhibiti suala hilo,” alisema.

Kwa upande wake, aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC, Hamad Rashid alisema utafiti huo ni sahihi kwa kuwa kuonyesha anataka uwajibikaji kwenye Serikali yake, kumemuongezea umaarufu. “Alipotoa hotuba yake bungeni tukasema kama atatekeleza haya nchi itakwenda vizuri, lakini ndani ya siku chache ametekeleza kwa vitendo. Ikiwa uchaguzi mkuu utafanyika leo, Magufuli ataibuka na ushindi kwa zaidi ya asilimia 80,” alisema.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa alipinga utafiti huo akidai ikiwa kutafanyika Uchaguzi Mkuu, mchuano baina ya Lowassa na Rais Magufuli utaendelea kuwa mkali. Alisema yapo mambo ya msingi ambayo amefanya vizuri ikiwamo suala la uwajibikaji kwa watumishi wa umma na baadhi ambayo hajafanya. “Ni vizuri afuate sheria za utumishi wa umma ili watu wasifanye kazi kwa hofu, kusiwe na vitisho ili waweze kutimiza wajibu wao. Wafundishwe kuwajibika kwa uadilifu. Vitisho na kuogofya siyo sahihi,” alisema. Alimtaka Rais kutokaa kimya kuhusu suala la Zanzibar kwa madai kuwa, linachafua sura ya nchi ikiwa halitachukuliwa hatua.

CHANZO:MWANANCHI
 
Ukweli ndio huo
Hakuna namna wamebaki kujificha kwenye ID feki Jf
Lakini mioyoni mwao Wanamkubari
 
They have compared onions and rice, which are not comparable. Wanamchokoza tu Lowasa wa watu ambaye katulia tuli. Hawa watafiti wanataka tu cheap popularity. Why do such a research? Is lowassa a president? Of which country? Unalinganisha raisi na mtu ambaye ni mwananchi wa kawaida!!!! E. L. sasa hivi ni mwananchi tu, si haki kumlinganisha na mtu yeyote aliyeko serikalini.

...waache wapuuzi hawana kazi za kufanya huko maofisini.Nawashangaa eti unamlinganisha mtu anaeongoza serikali na mwananchi wa kawaida?! nadhani Lowassa bado anawatetemesha sana huko ugambani.!!
 
Utafiti huu ni sawa na Ronaldo yuko benchi la akiba halafu umtaje mchezaji aliyeko uwanjani kuwa katika mechi hiyo kacheza vizuri kuliko Ronaldo ambaye yuko benchi
 
wangelinganisha Kikwete na magufuli katika kipindi kimoja, kmulinganisha Lowasa ambaye sio rais ni upungufu wa uweledi.

halafu kmuhoji Lipumba sio sahihi, mbona hawakumhoji mbowe?
 
Acheni masihara bana, kwani lini takwimu zilimuinua Lowasa na kumshusha magufuli? Mbona tangu kipindi cha kampeni takwimu zilisema Magufuli yuko juuu teeeehee e kweli mnafiki hafichiki. Kumbe Lowasa alikuwa juu mkashindwa kusema kwa unafiki wenu. Haya Tumewasikia.
 
Hivi unaanzaje kulinganisha Lowassa na magufuli katika kipindi hiki?ni watu wawili tofauti mmoja ni raisi wa nchi mwingine ni mwananchi wa kawaida siyo hata kiongozi
 
Tanzania tafiti bado sana , labda hii elimu bure itawasaidia kujifunza kwa wenzao wa nje. Tafiti inafanywa kwa ajili kufurahisha wakubwa, hapa si bure watu wanatafuta kupanda vyeo kwa tafiti za kijinga kama hii. Rai: Huyu aliyeongoza tafiti hii anapaswa kutafutiwa mwalimu wa kumfundisha kwenye darasa la pekeake.
 
Back
Top Bottom