Wapinzani Wajipange - Mwanga Umezidi Giza

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,463
40,963
Siasa ni Sayansi yenye kanuni tofauti na Sayansi asilia (natural science).

Awamu hii, kwa kipimo chochote kile, demokrasia na haki za binadamu ikihusisha haki za kisiasa, uhuru wa kukusanyika, uhuru wa kushiriki shughuli za kisiasa, uhuru wa maoni na uhuru wa kupata habari; vyote kwa pamoja, kinyume na inavyoelekezwa na katiba, vimekanyagwa na kuchezewa kwa kiasi kikubwa.

Hayo hayakufanywa kwa bahati mbaya bali kwa malengo na dhamira maalum. Dhamira kubwa ilikuwa ni kuwajengea watu uoga na hofu. Hilo limefanyika kwa nguvu kubwa na kwa kudhamiria. Matokeo yake ni kama ifuatavyo:

1) Viongozi kadhaa wa kuchaguliwa kama wabunge na madiwani wameingiwa na hofu ya kukosa kuchaguliwa. Na baadhi yao kwa vile kwao uongozi haukuwa na lengo ya kuwatumikia wananchi bali kuweza kuendesha maisha yao, kutokuwa wabunge au madiwani ni kukosa ajira ya kuwapa kipato. Suluhisho la pekee kwao ikawa ni kusalimu amri, na kujiunga na watawala wa sasa alimradi kama watawahakikishia kipato, iwe ni kwa pesa taslimu au kwa kupitia vyeo na madaraka.

2) Baadhi ya viongozi wa vyama ambao nao walikuwa wakitegemea kuwa kupitia uongozi wa vyama, wangeweza kujipatia kipato, walipoona wanazidi kubanwa na uwezo wa kupambana hawana, wakaamua kunyosha mikono na kufuata maslahi ya maisha yao binafsi.

3) Baadhi ya wanasiasa waliokuwa wanaibukia, wakiwa na shughuli zao mbalimbali za kiuchumi, kwa vile waliwindwa na kudhoofishwa, waliamua kunyosha mikono, na kujitenga na siasa za upinzani.

4) Vyombo vya habari, navyo vilibanwa hasa, ili na vyenyewe na wanahabari wao, angalao waendelee kuishi na kufanya kazi, walinyosha mikono, na kuamua kuishabikia serikali na CCM.

Watawala walitaka haya yaliyotokea yatokee. Kwa sababu yakiwa dhahiri, kila mmoja atakuwa muoga wa kupingana na watawala, akijua kuwa ukipingana nao, yatakupata yaliyowapata wenzako ambao wamefilisiwa, wamefunguliwa mashtaka bambikizi, wamepotezwa, wameshambuliwa na wengine kuuawa. Hii ndiyo inaitwa state terrorism.

Lakini wakati yakipangwa haya, hakukuwa na utambuzi dhahiri, wa nini jamii yetu na ya kimataifa itafanya au kunena. Waliamini kwa vile vyombo vya habari vitakuwa vimeuawa, mengi ya maovu hayatasikika popote. Hali hiyo imekuwa tofauti. Na matokeo yake yamekuwa kinyume na ilivyotarajiwa:

1) Tanzania kwa mara ya kwanza inatazamwa kama nchi isiyoheshimu haki za watu wake

2) Tanzania inatazamwa kwa ukaribu katika masuala yote yanayohusu utawala wa sheria, demokrasia, haki za kiraia na uhuru wa vyombo vya habari

3) Tanzania kwa mara ya kwanza imepunguziwa misaada kutoka jumuia ya kimataifa

4) Kutokana na kupungua kwa misaada, serikali imeshindwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi wake, na kutoa ajira mpya, mambo ambayo yamewafanya wananchi kuiona serikali haiwathamini

5) Kutokana na kupungua kwa misaada, ili serikali kutimiza wajibu wake, imelazimika kuweka kodi ama zisizolipika au zile ambazo zinafifisha au kufukuza uwekezaji, na hivyo kushuhudia uwekezaji kidogo sana ukilinganisha na awamu ya nne. Hii imesababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira, na kupungua kwa kasi ya uwekezaji na ukuaji wa export in terms of volume and value (taarifa ya BOT inaonesha hivyo). Mathalani, kwenye sekta ya madini, Tanzania imekuwa ndiyo nchi inayoongoza kwa mazingira mabaya ya uwekezaji Duniani, ikifuatiwa na Venezuela.

Kwa upande mwingine, mbinyo wa jumuia ya kimataifa kuhusiana na demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari, umekuwa ukiitesa serikali. Hii ndioyo sababu inayoifanya serikali kurudia mara kwa mara kutamka kuwa uchaguzi mkuu utakuwa HURU, WAZI NA WA HAKI. Na Serikali, hata kwa kutumia Tume hii ya Uchaguzi isiyo huru, inaweza kuufanya mchakato mzima kuwa huru, wazi na wa haki. Serikali itafanya hivyo kwa imani na madhumuni yafuatayo:

1) Serikali inataka kuionesha jumuia ya kimataifa kuwa madai kuwa serikali/CCM inagandamiza demokrasia ni uwongo bali watu wanaipenda sana CCM na zaidi Rais ambaye yupo madarakani.

2) Vyama vya siasa vya upinzani, viongozi wao, na wananchi ambao ama wanaunga mkono upinzani au wangegombea kupitia upinzani, tayari wametishwa na matukio ya huko nyuma, wametishika kiasi cha kutokuwa tayari kujitokeza kutoa upinzani kwa serikali iliyopo, na hivyo hata kama uchaguzi ukiwa huru na wa wazi, hakuna watakaojitokeza kutoa ushindani.

NAFASI ILIYOPO KWA UPINZANI
1) Kwa kuwa serikali/CCM wameahidi kuwa uchaguzi utakuwa huru, hata kama watalazimika kucheza faulo kama ilivyozoeleka, kutakuwa na hofu kubwa, pengine kuzidi awamu zote kwa sababu ya ahadi waliyoitoa

2) Serikali/CCM watakuwa na hofu kubwa ya kutenda uovu ulio wazi na wa kupitiliza kwa sababu wanajua kuwa Dunia inawaangalia ili kuthibitisha madai yake kuwa Tanzania kuna ugandamizaji wa demokrasia na haki za watu

3) Serikali/CCM ingependa kuepeleka taswira mpya kwa jamii ya kimataifa ili kupata tena misaada kutoka mataifa ya nje kwaajili ya kutekeleza miradi iliyoanzishwa ambyo mpaka sasa imekuwa ikijengwa kwa mikopo bila ya ufadhili wa mataifa rafiki kama ilivyozoeleka.

Kuna mtego kwa wapinzani. Kama wapinzani hawatajiandaa, wakiamini kuwa CCM na serikali yake wataharibu uchaguzi, halafu serikali ikaufanya uchaguzi kuwa huru na wazi sana, Serikali/CCM itakuwa imefanikiwa kuifanya Jumuia ya Kimataifa kutokuwa na uhalali wa kuendelea kuilalamikia awamu ya 5 kuwa inagandamiza demokrasia.

Wapinzani, jiandaeni kwa nguvu na weledi kuliko miaka yote. Hii ni nafasi nzuri kuliko awamu zote zilizopita. Msipoitumia, hamtaipata tena.
 
Umenena vyema ila wale wa kile chama cha ujamaa watakuambia tuko kwenye rightrack
 
Never forget that
human beings, by and large, do not want to hear truth; rather, they try to make
true that which they love. Who needs truth if it's going to put you out of
business? We would much rather delude ourselves by simply ignoring the facts,
even if we only succeed in prolonging the inevitable. Unfortunately, by so doing,
we also guarantee disastrous long-term results.

Nimeinakili kutoka kwenye kitabu kinaitwa "Million Dollar Habits, naona mleta mada unjaribu kuwapa faraja wapinzani kwa kuwaambia kile "wanachopenda kuambiwa" hata kama ni uongo kwasababu watu hatupendi UKWELI!
 
Aisee nimeona deni la ATCL nikajua kabisa ili ltabebwa na sisi wafanyakazi kwenye kodi manaake misaada hakuna na miradi ndo hivo haijakamilika. Kuhusu siasa mi naona CCM inajitahidi sana kununua wanaCDM kuaminisha dunia kwamba inakubalika na ndo maana wanazuia mikutano ya CDM kwa sababu wanaogopa itaonesha otherwise. Mungu atusaidie maana naona giza kali sana hapo mbele!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hili bandiko lako ni zuri sana, ila limepelea ubora baada ya kukosa wito wa tume huru ya uchaguzi. Kumbuka wananchi wengi hawajajiandikisha kupiga kura maana hawana imani tena na tume ya uchaguzi iliyopo, kwani wanatii moja kwa moja maagizo ya rais aliyepo madarakani. Iwekwe nguvu ya kutosha ili ipatikane tume huru ya uchaguzi. Kuna uzi humu wa leo kuhusu tume huru vya uchaguzi iweje, hiyo ya wangalau mfano wa Ghana ni muhimu.
 
Wanamuita jasusi mbobevu, napenda agombee Urais kwa chama kingine tuone nguvu za ujasusi wake kama ataweza kuishinda TISS ya CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kushinda anaweza ishinda shida iko kwa huyo atakaye tangaza siku hiyo labda akahifiche sehemu ambayo haijulikani ndio atamke mshindi nani
 
Hao wapinzani sijui wanaongozwa na kiongozi gani kwa sasa. Nafasi nzuri ilikuwa wakati Kikwete anaondoka 2015 lakini kuna wapenda pesa wakaamua kubadilishia gia angani.

Mpinzani wa kweli huwezi kumjua kwa kumuona akiongea mbele ya vipaza sauti za vyombo vya habari huku mapovu yakimtoka, mpinzani wa kweli anaishi na upinzani wake ndani ya nafsi yake pasipo kujionyesha hadharani.

Mpinzani wa kweli anafanana na wale Yesu aliowasema ndani ya Biblia kwamba hawapigi makelele njiani wakiwa wamevaa mavazi marefu, alichonacho ndani ya nafsi ndio chenye umuhimu kuliko mbwembwe za kutaka kuonekana.
 
Never forget that
human beings, by and large, do not want to hear truth; rather, they try to make
true that which they love. Who needs truth if it's going to put you out of
business? We would much rather delude ourselves by simply ignoring the facts,
even if we only succeed in prolonging the inevitable. Unfortunately, by so doing,
we also guarantee disastrous long-term results.

Nimeinakili kutoka kwenye kitabu kinaitwa "Million Dollar Habits, naona mleta mada unjaribu kuwapa faraja wapinzani kwa kuwaambia kile "wanachopenda kuambiwa" hata kama ni uongo kwasababu watu hatupendi UKWELI!
Uwongo ni upi? Kuwa Serikali haiwezi kuendesha uchaguzi huru kama ilivyotamka?
 
Mkuu hili bandiko lako ni zuri sana, ila limepelea ubora baada ya kukosa wito wa tume huru ya uchaguzi. Kumbuka wananchi wengi hawajajiandikisha kupiga kura maana hawana imani tena na tume ya uchaguzi iliyopo, kwani wanatii moja kwa moja maagizo ya rais aliyepo madarakani. Iwekwe nguvu ya kutosha ili ipatikane tume huru ya uchaguzi. Kuna uzi humu wa leo kuhusu tume huru vya uchaguzi iweje, hiyo ya wangalau mfano wa Ghana ni muhimu.
Wananchi wengi kutojiandikisha, na vyama vya upinzani kutowataka mashabiki na wanachama wao kujiandikisha, ni baadhi ya makosa ya msingi ambayo yanaipa CCM nguvu ya kulifanya zoezi la uwazi wakijua kuwa hata kwa kuhesabu kura halali, bado watashinda.

Kujiandikisha hakuzui kudai Tume Huru.
 
Kimsingi watu hawawezi kuendelea kujiandikisha huku hawana uhakika wa usalama wa kura zao. Hata hivyo vyama vya upinzani wakiwataka wanachama na washabiki wao wajitokeza hawatajitokeza kwa wingi maana wanajua uchaguzi sio wa haki. Walipaswa kudai tume huru kwa nguvu zote, ili ikirudi awamu ya mwisho ya kujiandikisha watu wawe na imani kwa mbali. Hiyo tume huru ya uchaguzi ikidaiwa kwa nguvu za dhahiri itautia najisi huo uchaguzi, hata ukifanyika utakosa uhalali na kuzidisha msukumo wa ndani na nje.
 
Back
Top Bottom