Wapinzani waja na ufisadi mwingine

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Wapinzani waja na ufisadi mwingine

na Ratifa Baranyikwa, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SERIKALI imetakiwa kutoa ufafanuzi wa juu ya ubinafsishaji wenye utata wa Kiwanda cha Karatasi cha Mgololo, kinachodaiwa kuuzwa kifisadi kwa Kampuni ya Rai Group Ltd, ya nchini Kenya.

Hayo yalibainishwa jana bungeni na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Lucy Owenya, wakati akisoma hotuba yake ya kujibu ile ya bajeti ya wizara hiyo iliyosomwa na Waziri wake, Mary Nagu.

Katika hotuba hiyo, Owenya alisema, kambi ya upinzani, inakusudia kuwasilisha hoja binafsi bungeni iwapo serikali itashindwa kutoa taarifa kamili juu ya kiwanda hicho sambamba na kueleza mchakato wa ubinafsishaji wake kwa kampuni hiyo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku tano tu zimepita, tangu Waziri Nagu, alipotoa ufafanuzi juu ya ubinafsishaji wa kiwanda wakati akijibu swali la Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, (CHADEMA).

Katika majibu yake hayo ya wiki iliyopita, Nagu alisema kuwa, kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa kufuata taratibu zote.

Katika hotuba yake ya jana, Owenya alisema serikali haikuwa makini katika ubinafsishaji huo, kwani kumbukumbu zinaonyesha kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa Kampuni ya Rai Group, lakini utafiti wa kambi ya upinzani umebaini kuwa hakimilikiwi na kampuni hiyo kama ilivyo kwenye makubaliano ya uuzwaji.

Alisema utafiti huo umebaini kuwa kiwanda hicho kimeuzwa kwa Kampuni ya Angel Hurst Industries ya nchini Uingereza, inayodaiwa kumiliki hisa asilimia 99.9.

"Kampuni ya Angel Hurst Industries inaonekana kwenye Certificate of Incentives No. 00021049 iliyotolewa na Kituo cha Uwekezaji (TIC) Aprili 19, 2004 kwa Mufindi Paper Mills Ltd, ambayo ndiyo kampuni iliyosajiliwa baada ya kununua Kampuni ya Southern Paper Mills (SPM) ambayo ilikuwa na asilimia 100, mali ya serikali na hivyo kusimamiwa na NDC," alisema.


Katika ufafanuzi alioutoa Waziri Nagu mwishoni mwa wiki, bungeni alisema Kampuni ya Angel Hurst Industries, inamilikiwa kwa asilimia 100 na Rai Group, na hivyo kutokuwa na tatizo lolote kwani kampuni zote mbili ni wamoja.

Kambi ya upinzani inaielezea kauli hiyo ya Nagu kuwa iliyozidisha utata kuliko majibu na kusisitiza kuwa inahitaji taarifa kamili.

Aidha, akielezea mchakato mzima wa ubinafsishaji wa kiwanda hicho, Owenya alisema kwa mujibu wa kifungu cha mkataba wa mauziano, kinatamka bei ya mauziano ya kiwanda kuwa ni dola za Marekani milioni 26 lakini cha kushangaza ni kwamba, mkataba huo unaeleza serikali italipwa dola milioni moja tu za Marekani siku ya kuwekeana saini na dola 3,000,000 zitawekwa kwenye Escrow Account ambazo mwekezaji atazichukua atakapokuwa ametimiza masharti, ikiwemo kukarabati kiwanda chake.

"Maana yake ni hela zake na si malipo ya ununuzi wa kiwanda, mambo haya yanahitaji ufafanuzi na kauli ya waziri haikutoa ufafanuzi kabisa wa hali hii tata. Fedha nyingine dola za Marekani milioni 22 atazitumia mwekezaji kwa kufanyia kiwanda ukarabati, nazo zinabaki kwake kama lengo lilikuwa kuhakikisha kiwanda kinaendelea, kwanini serikali haikusema hivyo wazi katika mkataba,?"

"Ni nini tafsiri ya purchase price, Mheshimiwa Spika, hivi anadanganywa nani? Kwa dola milioni moja kwa nini isielezwe hivyo waziwazi? Kama tatizo ni kukosekana kwa mnunuzi kama serikali inavyotaka kueleza, kwanini hakikuuzwa kwa sh moja, yaani ‘Nominal Value'?"

Kwa mujibu wa maelezo ya kambi ya upinzani, Kampuni ya Rai Group inadaiwa kumilikiwa na Wakenya wawili waliotajwa kwa majina ya Jaswant Singh na Sarbjit Singh kila mmoja akiwa na hisa 0.006.

Kambi ya upinzani imesisitiza kuwa inataka kujua hao wawekezaji wenye hisa asilimia 0.006 kama ni kweli wawekezaji na wanaweza kukifufua kiwanda.


Owenya alisema kuwa serikali itamke ndani ya Bunge kama jambo hilo kisheria ni sahihi na hao wenye hisa zaidi ya asilimia 99 wanaonekana wapi katika mkataba na kama mkataba wa mauzo hauwataji kukitokea tatizo wao watawajibikaje na mkataba ambao si washiriki.

"Kwanini kuwa na mkataba kama kuna weza kuwa na watu waliojificha nyuma na mkataba kusainiwa na watu wasio na kitu? Je, Rai Group waliosajiriwa kwa mujibu wa sheria Tanzania ni wamiliki wa MPL Ltd kwa pamoja wakati wa kuuziana wanamiliki tu asilimia ya 0.01?" alihoji.

Aidha, kambi ya upinzani imelalamika kiwanda hicho kuuzwa kwa bei ya kutupa ukilinganisha na thamani halisi ya kiwanda.

Akinukuu hukumu iliyotolewa na mahakama ya kazi juu ya uchunguzi wa mgogoro wa kazi Na 80/2006 ya chama cha wafanyakazi TUICO na PSRC na wenzake, inadaiwa kuwa ilitamkwa " si rahisi kuamini kuwa mali zote za Southern Paper Mills Ltd (Kiwanda cha Mgololo) za thamani ya soko la mabilioni si chini ya bilioni 500 kwa makisio yangu na si ile ya bilioni 85 iliyotumika kuuzia tunaona hii ni "token/book price value" tu ambayo mathalani flat rate ya trailer Scania linalofanya kazi lilithaminiwa kwa sh 300,000 kwa kila trailler ambayo ni chini ya bei halisi hata ya tairi lake moja tu…"

Owenya alisema hali hiyo ni ya kutisha kama gari la tani 60 tena "heavy duty" liliuzwa kwa bei ya 600,000 bei inayofanana na bei ya tairi moja tu la gari hilo na kuongeza kuwa " hapa kunahitajika maelezo ya kutosha," alisema.

Alizitaja rasilimali za kiwanda hicho zilizouzwa kwa bei ya kutupa kuwa ni pamoja na nyumba, zikiwemo za daraja la kwanza, kijiji kizima cha wafanyakazi kama ilivyorekodiwa katika mashauriano ya kamati ya "FAST TRACK" ya Baraza la Mawaziri Agosti 4, 2003 .

Kambi ya upinzani pia imeitaka serikali kueleza juu ya eneo la hekta 28,000 ambazo hazikulipwa kitu kabisa na kutaka tathmini ifanyike upya kuangalia bei halisi ya maeneo yote hayo au mkataba uvujwe.

Aidha, NGO inayoitwa ICOMET inayodaiwa kupewa hekta 2,000, lakini ikapewa hatimiliki ya hekta zote 28,000 na kuhoji kuwa NGO hii ni ya nani.


Aidha, kambi ya upinzani imeitaka serikali kusimamia utaratibu unaoeleweka kuwalipa waliokuwa watumishi wa kiwanda hicho zaidi ya 760 ambao bado wanadai haki zao pamoja na hukumu iliyotolewa mahakamani, wakitakiwa kulipwa zaidi ya sh 2,647,255,816.

Wakati huo huo kambi ya upinzani pia imeitaka serikali kutoa ufafanuzi juu ya kuuzwa kwa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kinachodaiwa kuuzwa kwa bei ya kutupa ya sh bilioni 116 kwa mwekezaji anayejulikana kama ILLOVO.

Kambi ya upinzani imesema kuwa imeshtushwa na bei hiyo mara baada ya kubaini kuwa Kilombero ilikuwa na viwanda viwili, yaani K1 ambacho kina eneo la hekta 6,214.5 na K2 hetkat 3,153.
 
Hivi kwa nini mikataba yoote ya Bongo hukosi hizi last name Singh na kina Patel au the like? !!Mhmm!
 
Mambo Bado Ni Kiza Mgololo, Wafanyakazi 750, Hawajalipwa Mafao Yao Na Wenzao 58, Wamesha Fariki Dunia Kwa Ugumu Wa Maisha. Tena Kwa Wiki Takribani Mbili Mmiliki Amekizima Kiwanda Kwa Matatizo Yake Binafsi, Mishahara Hajatoa Na Hari Ni Ngumu Kwa Kweli
 
ni prf juma kapuya tu kwa sasa ndiye mwanaccm pekee anayefaa kuwa rais 2015
 
Back
Top Bottom