Wapinzani waibua mapya

Maseke ya Meme

JF-Expert Member
Jul 11, 2007
693
905
2007-10-17 15:35:49
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Lile soo la Ufisadi sasa limechukua sura mpya baada ya wapinzani kuibua ishu nyingine inayohusiana na tuhuma hizo.

Hata hivyo, safari hii wapinzani wameelekeza kombora lao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambako wamedai kuwa chombo hicho, kinatumia mapesa mengi ya kodi kwa ajili ya kuwalipa wabunge na hivyo kuwa sehemu ya hujuma za raslimali chache zilizopo.

Tuhuma hizo mpya za ufisadi dhidi ya Bunge zimetolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye aliwania urais kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi.

Akichangia mada kwenye mjadala wa kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere uliorushwa jana na kituo cha runinga cha Channel Ten, Dk. Mvungi akasema chombo hicho cha kutunga sheria kinatumia mapesa mengi yasiyolingana na hali ya uchumi wa nchi.

Akasema Dk. Mvungi kuwa kitendo cha Bunge kupitisha sheria ya kumpa kila mbunge kiinua mgongo cha Shilingi Milioni 60 baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitano bungeni hakitofautiani na ufisadi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya vigogo.

`Hili sasa limekuwa ni dola la ufisadi, kiinua mgongo cha Shilingi Milioni 60 kwa mbunge kila baada ya miaka mitano, hakiendani na hali halisi ya maisha ya Mtanzania,` akasema Dk. Mvungi.

Amesema katika hali halisi fedha, hizo hutolewa wakati wabunge hao wakienda kwenye uchaguzi ili ziwasaidie kuwanunua wapigakura na hatimaye washinde uchaguzi na kurejea tena bungeni kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Akasema Dk. Mvungi kuwa hatua hiyo hulenga kuwadhoofisha wapinzani wa wabunge hao ndani na nje ya vyama vyao ambao huwa hawana fedha za kupambana nao.

Hivi karibuni, umoja wa vyama vine vya upinzani nchini umekuwa ukishikia bango tuhuma kadhaa za ufisadi na kufikia kuwataja baadhi ya vigogo wanaodai kuwa ni vinara wa ufisadi.

Vyama hivyo vinne ni NCCR-Mageuzi, TLP, CHADEMA na Chama cha Wananchi, CUF.

SOURCE: Alasiri
 
I support Mvungi for unveiling this; although it is a well known thing. No wonder every one runs into politic. It will take almost 3 years or so for a professor at Muhimbili to earn 60 million. It will take us many years to undo the damages that have been exaccerbated by this bollock!

It is a crunch time now that we wananchi tuwape masharti wabunge wetu kuwa tunapowachagua moja ya kero yetu sisi wananchi ni hili swala la kiinua mgongo cha wabunge. Kwa kiasi hizi millioni 60 zinachangia kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika chaguzi.

Lingine, hawa wabunge wapunguze muda wa kukaa huko dodoma. Wanatumia pesa nyingi za walalahoi ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye huduma ya maji, mashuleni pamoja na barabara.

Waheshimiwa wabunge, mkiweza kutimiza hayo hapo juu niliyopendekeza wananchi tunaweza kurudisha matumaini kwenu. Mkiendelea kupuuza, dawa yenu inachemka. Muda wa kuinywa umekaribia.
 
Tshs 60 million after just 5 yrs !!
This is robbery!! Hakuna uwezekano wa kuwafungulia mashtaka na kuzuia hayo malipo ya 60 mil on the basis that hailingani na kazi waliofanya and therefore illegal?
 
nyie mnaongea nini? hiyo mbona ndogo sana ukilinganisha na marupurupu mengine waliyojiwekea kuanzia mafuta,Land Cruiser,posho ya vikao etc...ngoja tawaletea list kamili ili mtie akili mjue hawa wabunge is nothing but mafia tuu.
 
Hmmm! Bunge la mafisadi! Wahadhiri wetu hawalipwi vizuri kama wabunge, Madaktari wetu hawalipwi vizuri wabunge lakini wabunge ambao wanashindwa kutetea maslahi ya Watanzania wamejipangia mishahara na marupurupu manono! Na katika mwaka mzima muda wanaokaa bungeni haufiki hata siku 90! Na miezi mingine wanaishia kufanya biashara zao binafsi ala Nimrod Mkono style. Kweli hawa nao ni mafisadi!
 
Tuhuma hizo mpya za ufisadi dhidi ya Bunge zimetolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye aliwania urais kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi.
Wapinzani waibua mapya
usanii wa magazeti......
 
nyie mnaongea nini? hiyo mbona ndogo sana ukilinganisha na marupurupu mengine waliyojiwekea kuanzia mafuta,Land Cruiser,posho ya vikao etc...ngoja tawaletea list kamili ili mtie akili mjue hawa wabunge is nothing but mafia tuu.

!Lete hiyo list kamili tuanze kuitawanya kwa wapiga kura. !!
 
Milion 60!!

Hiyo ni hela nyingi saana.Sidhani kama kuna mhadhiri anaepata hela kama hiyo hata baaada ya miaka kumi.Mshahara wa profesa wa muhimbili hauzidi milion moja na nusu at most kabla ya makato,akitoa matumizi ya mwezi anabaki na hela kidogo saana na ndio maana aidha huenda kwenye hospitali binafsi kuongeza kipato kdogo au hujihusisha na biashara au wachache huenda kwenye siasa.Wazoefu mtatuambia,nafikiri ni wafanyakazi wachache hata kama ni waandamizi serikalini wanaopata kiinua mgongo kiasi hicho baada ya kistaafu miaka 30 su zaidi ya kulitumikia taifa kwa moyo mkunjufu.
 
milioni 60 wakati hawafanyi hata kimoja huko bungeni! tunapelekeshwa tu na wamawiri wachache huko bungeni, kisha wabunge wanalipwa mamilioni hayo.

ndio maana unakuta mtu hataki kuachia ubunge, japo kuwa anajiona hasa kuwa hawasaidii kwa lolote waliompigia kura
 
Milioni 60???
Kweli hizi ni hela nyingi sana.. Kumbuka hapa kila mwezi wanapata milioni 3 achilia mbali ile lakimoja na ishirini ya vikao kwahiyo kwa hesabu ya haraka haraka kwa myaka nitano mbunge anapata yafuatayo

1. milion 3 x myezi 12 mara miaka 5 sawa na mil.mil 180
2. Posho ya vikao kwa mwaka laki 120 x 90 x miaka 5 sawa na mil 54
3.Kinua mgongo mil 60
4. mkopo wa shangingi si chini ya mil 40

Kwa haraka haraka myaka 5 kila mbunge anakomba si chini ya milioni 334.

Mnaionaje hiyo biashara?? ndo maana hata akinunua ubunge kwa milioni 100 si hoja!!
 
Kwa ujumla pesa zote wanazopewa wabunge ni rushwa ili kuwafanya wasiisimamie kidedea SIRIKALI pale inapokuwa inaboronga. Hii inawafanya wabunge wa CCM wanaojifanya wajuaje wafikiri mara mbilimbili kisha waamue either wawatumikie wananchi wakose pesa au aseme hoja imepita na aendelee kula hizo pesa. Si mnakumbuka Mkapa alikuwa anawaita na kuwaambia kuwa yeye ndo anayepitisha majina yao, hivyo wasilete mdomo mrefu vingevyo unga utamwagika. Sasa Dr. kakimbia Muhimbili kuja kuchuma mahela ya bure leo umwambie badaada ya miaka mitano arudi tena wodini eti kwa ajili kuisimikia SIRIKALI!! Nani atakuelewa hapo.Hizo pesa zinawafunika kabisa Ubongo,Shahada,PhD,Masters yaani wanakuwa Misukule tu.
 
Sijasikia hata wabunge wa upinzani wakilalamika. Wote mambo yao ni yale yale, kwenye mashangingi wamo, kiinua mgongo wamo, posho kubwa wamo, wanatofautiana tu pale ambapo wao wanazidiwa kete kama kwenye madini.
 
Hi ndio fad ya Bunge kufanya kazi kwa ilikadi...sasa hao Wabunge ambao leo wanapata shida uya kuzomewa na mwingine nasikia kachomewa nyumba sijui wapi kule...ndio sababu wanapata KIUNUA MGONGO HASWA.. na hiyo nayyo sio Hongo kwa wahwshimiwa je PCB wanaweza kuanza uchunguzi.......
 
mimi sioni haja ya kubishana tuliingize hili moja kwa moja katika vikao vya watanzania kupitia nwanaharakati za binadamu kila mtu anashida humu Tanzania bora huyo mvungi kuna mama zetu wanauza pombe wapate kula nani hajui hili tuachie kikwete atumalize hivihivi tu? wabunge wa upinzani wao ni size yetu tutawailiza msimamo wao wako pamoja ama wanakataa hiyo pesa? wakijibu wanaikataa tunaanza nao, kama hawako tayari kukataa malipo hayo tunaanza kwa maandamano nchi nzima mimi siogopi kuomba kibali kama mnaweza kuniunga mkono? tupeane habari ya kufanya kikao chetu kupinga hilo sio la siasa, nataka majibu yenu na ushirikiano sio utani.
 
Sijasikia hata wabunge wa upinzani wakilalamika. Wote mambo yao ni yale yale, kwenye mashangingi wamo, kiinua mgongo wamo, posho kubwa wamo, wanatofautiana tu pale ambapo wao wanazidiwa kete kama kwenye madini.

Hapo, hapo hapo sasa! Siasa za Bongo magumashi matupu....
 
Sijasikia hata wabunge wa upinzani wakilalamika. Wote mambo yao ni yale yale, kwenye mashangingi wamo, kiinua mgongo wamo, posho kubwa wamo, wanatofautiana tu pale ambapo wao wanazidiwa kete kama kwenye madini.

haki ya nani bana huu ni ukweli mtupu na sasa acha nicheke ! hahaaaa, itakuwa vizuri kama JK atabadirisha mawaziri 3 na kuwapa nafasi hizo wapinzani halafu tuone itakuwaje ! sijui watazidiana hata huko ?
 
Sijasikia hata wabunge wa upinzani wakilalamika. Wote mambo yao ni yale yale, kwenye mashangingi wamo, kiinua mgongo wamo, posho kubwa wamo, wanatofautiana tu pale ambapo wao wanazidiwa kete kama kwenye madini.

Mkuu Mtanzania,

Heshima mbele, this is strong and bold, keep it up and I am down!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom