Maseke ya Meme
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 833
- 1,215
2007-10-17 15:35:49
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Lile soo la Ufisadi sasa limechukua sura mpya baada ya wapinzani kuibua ishu nyingine inayohusiana na tuhuma hizo.
Hata hivyo, safari hii wapinzani wameelekeza kombora lao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambako wamedai kuwa chombo hicho, kinatumia mapesa mengi ya kodi kwa ajili ya kuwalipa wabunge na hivyo kuwa sehemu ya hujuma za raslimali chache zilizopo.
Tuhuma hizo mpya za ufisadi dhidi ya Bunge zimetolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye aliwania urais kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi.
Akichangia mada kwenye mjadala wa kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere uliorushwa jana na kituo cha runinga cha Channel Ten, Dk. Mvungi akasema chombo hicho cha kutunga sheria kinatumia mapesa mengi yasiyolingana na hali ya uchumi wa nchi.
Akasema Dk. Mvungi kuwa kitendo cha Bunge kupitisha sheria ya kumpa kila mbunge kiinua mgongo cha Shilingi Milioni 60 baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitano bungeni hakitofautiani na ufisadi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya vigogo.
`Hili sasa limekuwa ni dola la ufisadi, kiinua mgongo cha Shilingi Milioni 60 kwa mbunge kila baada ya miaka mitano, hakiendani na hali halisi ya maisha ya Mtanzania,` akasema Dk. Mvungi.
Amesema katika hali halisi fedha, hizo hutolewa wakati wabunge hao wakienda kwenye uchaguzi ili ziwasaidie kuwanunua wapigakura na hatimaye washinde uchaguzi na kurejea tena bungeni kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Akasema Dk. Mvungi kuwa hatua hiyo hulenga kuwadhoofisha wapinzani wa wabunge hao ndani na nje ya vyama vyao ambao huwa hawana fedha za kupambana nao.
Hivi karibuni, umoja wa vyama vine vya upinzani nchini umekuwa ukishikia bango tuhuma kadhaa za ufisadi na kufikia kuwataja baadhi ya vigogo wanaodai kuwa ni vinara wa ufisadi.
Vyama hivyo vinne ni NCCR-Mageuzi, TLP, CHADEMA na Chama cha Wananchi, CUF.
SOURCE: Alasiri