Wapinzani wafanyiwa figisu Kata ya Mbagala Kuu: CCM yapita bila kupingwa

Ninachofurahia ni kwamba NEC ndo inatumika kusambaza chuki kwa haraka. Watu wa korogwe tayari kisha mbagala then sehemu nyingine kisha HAKI itadaiwa kinguvu ni suala la muda tu. Uzuri NEC hawana kinga na pia ndugu zao tupo nao mitaani zikianza vurugu sababu ya wao haitapendeza

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila atendaye kosa atalipwa , Mshahara wa dhambi ni mauti .
 
Huwa wanapewa tarehe ya kuchukua na kurudisha fomu, kuambiwa mwisho wa kurudisha ni saa ngapi na fomu wazirudishe wapi. Mengine yote ni mizengwe.
Nasikia kwa Waitara mkwara ulikuwa ndani ya CCM, waliotia nia kufumba na kufumbua muda wa kuchukua fomu na kurudisha umekata (mchakato ndani ya chama). Hivyo alipitwa bila kupingwa.

Korogwe vijijini wapinzani wa vyama kadha "hawakujua" wapi pa kurudisha fomu na nani wa kumpa hadi walipo ambiwa ni saa ya kufunga ofisi waondoke.

Niliwsikia CUF wakisema badala ya ma-agent wao, lilipigwa zengwe magent wa chama chetu kitukufu ndiyo walipewa utambuzi kuwakilisha CUF. Hivyo waliosaini fomu za matokeo ni CCM wakiwakilisha "CUF" .
Tanzania yangu ndiyo hii.
Nashukuru saana kwa uelimishaji mzuri, hii ni hatari, nashindwa kuamini maneno ya viongozi uongo wanavyougeuza kuwa UKWELI.
Yaani mpaka Leo tunamuhitaji BABA WA TAIFA atupe muongozo au tumelaanika.

Mzee Mwinyi
Mzee Mkapa
Mzee Kikwete

Vaeni vazi la Mwl muwe NEUTRAL
 
Ninachofurahia ni kwamba NEC ndo inatumika kusambaza chuki kwa haraka. Watu wa korogwe tayari kisha mbagala then sehemu nyingine kisha HAKI itadaiwa kinguvu ni suala la muda tu. Uzuri NEC hawana kinga na pia ndugu zao tupo nao mitaani zikianza vurugu sababu ya wao haitapendeza

Sent using Jamii Forums mobile app

Tz tumekalia bomu matakoni. iko siku litaturipukia. uvumilivu una mwisho.
 
Haingii akilini kuwa wanaokosea muda na kujaza form ni Upinzani peke take!
Kuna namna happy. Inatakuwa independent electrol commission. Tume huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom