Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,261
- 105,421
Nimetoka kusoma thread ya Regia Mtema anasema "amerudi" kutoka Kilombero, apparently Kilombero si base yake ni sehemu ya kwenda wakati wa uchaguzi, na uchaguzi ukiisha ni muda wa "kurudi mjini" kutoka Kilombero.
Najua nimekuwa critical kwa wapinzani huko nyuma, particularly Regia. Lakini nafikiri ni muhimu watu wawe critical ili wapinzani wajue wanakosea wapi na wajirekebishe vipi.
Moja ya vitu vilivyotajwa katika uchaguzi huu uliopita ni kwamba wapinzani wamekuwa na "vyama vya uchaguzi" vinavyopata muamko wakati wa karibu na uchaguzi, na uchaguzi ukiisha vinafifia uhai.
Ningependa kuona wapinzani, hususan CHADEMA na CUF vyama vilivyoonyesha muamko wa kisiasa na kiasi kikubwa cha uhamasishaji wa wananchi, vianze kufanya kampeni za chinichini za 2015 kuanzia sasa. Mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine.
Vyama vianze kuwajua watu wenye potential ya kusimamishwa kushindania ubunge mapema, vianze kuwaweka katika nafasi za majimboni huko watakapoweza kushirikiana na wananchi moja kwa moja na kujulikana, pamoja na kuimarisha vyama hivi. Ni muhimu kuanza hizi shughuli mapema na kutongojea mpaka mwaka wa uchaguzi ambapo mambo mengi yanakuwa yanatokea pamoja.
Nisingependa kuona uchaguzi wa 2015 unafika halafu wanaupinzani hawajajifunza makosa ya 2010, wanaanza kuokoteza wagombea wa ajabu ajabu dakika za mwisho, na hawana mkakati madhubuti wa kuchukua majimbo haya.
Nawakilisha hili na ningependa kusikia strategist wa upinzani wanasema nini.