Kwa hiyo kimsingi mkuu unakubaliana na mimi kuwasio lazima mawaziri wa rais wachaguliwe na rais, inawezekana na rais akachaguliwa na mawaziri wake wakapigwa chini bila yakuiba kura, hiyo ndio iliyokuwa hoja yangu ya msingi, je tunakuabaliana kwenye hilo?
Sidhani kama hiyo ndiyo ilikuwa hoja yako ya msingi katika mfano wa clinton maana hiyo ilitokea katika chaguzi mbili tofauti,
uchaguzi wa kenya umeonyesha kuwa serikali ya kibaki imekataliwa kila sehemu isipokuwa centra ambako pia kuna uvumi kuna utata. the guy aligundua kuwa hawezi kuiba kura zote za urais na za ubunge kama wanavyofanya ccm kwa sababu kura za wabunge ni personal kwa wabunge kuliko za urais.
kuna uwezekano huo kuwa rais akachaguliwa ila wabunge wakapigwa chini lakini hilo halikuwa katika kesi hii kulingana na taarifa za television nyingi za kenya ukiacha kbc.