Ili waweze kuondoa CCM Madarakani.
Quote:-
"Na Kibaki akishinda, ni wazi kwamba ataiba kura."
Very Tanzanian thinking, wakishinda upinzani then what mkuu? Watakuwa wameshinda kwa halali?
You are right Mtanzania,Ni jambo la ajabu sana Kwa wananchi eti kutokuwa na imani na mawaziri (zaidi ya nusu)pamoja na wabunge wao na kuwanyima kura, kisha kuwa na Imani na Rais na kummiminia kura za kutosha.Mkuu ES,
Hapa kuna tofauti, rais ambaye karibu baraza lake lote la mawaziri limeangushwa, amepoteza majority ya wabunge, hawezi kushinda kihalali hata siku moja.
Kama rais anapendwa hukisaidia pia chama chake kupata kura japo za kuridhisha.
Hili balaa la kuiba kura afrika ni zaidi ya ufisadi, inatakiwa tulikomeshe kwanza. Mtu anayeiba kura atashindwa kuiba pesa ili kuwazawadia hao marafiki wanaomwibia kura?
Zitto amesema anaweza asigombee ili apate muda wa kujiendeleza kitaaluma, hizi ndio siasa zinazohitajika, sasa wengine jitokezeni mpokee kijiti cha zitto tuendeleze riadha ya siasa, ili tusijenge tabaka la wakoloni weusi wanaosubiri kipigo kama samwel doe.
Kuna wazee wenye busara kama dr.malecela na Edwin Mtei waliosema sasa tupumzike. Heshima zao ndani na nje ya nchi zimenawiri zaidi.
Mkuu Mtanzania,
Heshima mbele, Bill Clinton alishinda urais, lakini wananchi wakasema Republican ndio wanaofaa kushika Congress na wakawachagua, kwa hiyo mawaziri wote wa Kibaki, wanaweza kushindwa lakini Kibaki, akashinda kama rais aliyekuwa amezungukwa na wahuni, sisemi ndivyo ilivyo lakini ninakuwa na open mind maana siasa hazina guarantees,
Kuhusu uchaguzi mzima wa Kenya, no question kuhusu uelewa mkubwa wa siasa wa wa-Kenya, kuliko sisi wa-Tanzania, lakini pia the fact kwamba ukabila ndio dhana kubwa ya siasa zao inakuwa ngumu sana kuelewa siasa za Kenya, kwa sababu sio siri kwamba the political na bureaucratic system ya Kenya, ni dominated na the Kikuyus, which makes ushindi wa Odinga, kuwa na matatizo makubwa kwenye kutawala,
Odinga, is he a true opposition kama Chadema? I am not sure, Moi alipaswa kuwa adui na Kibaki, lakini leo tunaambiwa ndiye aliyei-fund kampeni ya Kibaki, I mean this is too much of a confusion kwa wananchi wanaotaka mabadiliko ya kweli, lakini haiondoi ukweli kwamba the Kenyans wako advanced kwa uelewo wa siasa kuliko sisi, tatizo lao kubwa linalotufanya tuwe na nafuu kuliko wao at the end of the day, ni siasa zao za kikabila, ambazo kwa kweli sisi Tanzania hatuwezi kujifunza anything from it, maana kwenye hiyo system unachohitaji ni kuwa Mluo, au Mkikuyu, basi kampoeni itajifanya yenyewe, sasa sisi wabongo tutajifunza nini?
Ni Kibaki huyu tulimwona shujaa kwa kumgaragaza Uhuru Kenyatta, akafanyiwa tafrija hadi ikulu ya marekani! leo hii damu ya wakenya inamwagika kuliko hata ya kumtoa mwingereza. Hata kama atashinda gharama yake sivyo ilivyostahili. Ilikuwa shughuli kumtoa mrema nccr pale Tanga, angekuwa ikulu ingekuwaje?
Jamani tusimwondoe Dr.Kaunda na kumweka chiluba tukaona tumewini. Wanaoishi ulaya kwa posho za UNHCR acha wakae huko, wakizeeka waje tu. Tunao political newcomers kama Laurence Masha, Dr.David Mathayo, Zitto, Freeman Mbowe wanagombea na kushinda.