Wapinzani tutulie tutawaliwe, tulikubali kushindwa.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kuna kitu hua najiuliza sana mpaka kichwa kinaniuma pengine hata kidonge kimoja cha panadol hakiwezi kusaidia kitu.

Hivi tulikua wapi wakati CCM wanajaza wabunge mpaka kuwafanya kua na idadi kubwa bungeni na kuamua lolote lile kwa wingi wao?Kwani miaka yote si ndio hua ni wengi zaidi kuliko upinzani?Inapofikia mahali tunaanza kulia baada ya matokeo tunataka kitu gani hasa kama tulikua na uwezo wa kuzuia ushindi huo?

Kama tulijua kabisa kua katiba yetu hii ya sasa na tume ya uchaguzi haviwezi kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki kabla ya 2015 tulikua tumelala wapi? Tulishindwaje kutoka barabarani kukataa kuingia kwenye uchaguzi tukiwa na katiba ya zamani tena ya enzi za chama kimoja? Mzee Lubuva la timu yake tulishindwaje kuwakataa kabla ya uchaguzi?

Kwa uelewa wangu ni kwamba kama tungekubali kuingia barabarani kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi pasingeshindikana jambo, Sidhani kama kungekua na askari ambaye angetoka barabarani kumtandika risasi mwandamanaji anayeidai katiba kihalali kesi yake maana inaweza kua mbaya sana kwa mujibu wa sharia.Tulikua na kila sababu ya kususia uchaguzi mkuu bila ya kua na tume huru ya uchaguzi, tena alishaliahidi hilo Rais Mustaafu mh JK na tungeamua asingelikataa hilo.Sasa tunalialia nini?

Kwa maoni yangu, hatuna haja ya kendelea kuipinga serikali iliyoko madarakani kwa sababu sisi ndio tuliowaruhusu kushika dola! Waliishiwa pumzi, shabaha yao ilibaki moja tu ya kuingia ikulu kwa namna yeyote kwa sababu walijua kua katiba yetu ni mbovu itawapa mamlaka ya kuamua lolote watakalo ili wakajipange upya kabla ya chaguzi zingine! Kwa wingi wetu na uungwaji mkono tuliokua na uwezo tulikua na uwezo mkubwa wa kuwazuia kukamata dola isivyokua halali hata kama zingetumika nguvu zozote ovu.

Tunajua kupige kelele lakini yanapoanza mapambano tunarudi nyuma, kama tuna uwezo huo ni kwanini turidhikie kuendeshwa nje na matakwa ya katiba?Sikubaliani na ukiukwaji wa katiba lakini tujue kama adui tulimruhusu sisi na anatumia mapengo na udhaifu wa katiba kjiamulia watakalo juu yetu.

Wananchi wananung'unika kila mahali, wanaona kama tumewasaliti, maisha magumu kila mahali hakuna unafuu wowote chini ya CCM! Hawaipendi CCM sasa wafanyaje maana tumekosa mbinu ya kisayansi ya kuizuia CCM kuendelea kushikilia dola.

Tusibaki kupiga kelele mithili ya yule ndege ambaye ukiingia msituni anapiga kelele utafikiri yeye ndiye mmiliki wa msitu lakini ukimrushia mshale ukamkosa msitu unakua kimya utadhani hakuna kiumbe anayeishi humo.Kwanini tusubiri hadi 2020 tuje kuanza kulialia tena.Wakati ndio huu tusipoteze muda kama ilivyokua 2015.Somo tosha tunalo wala hatuhitaji darasa tena.

Ikumbukwe kua duniani kote hakuna mtawala ambaye anaweza kutumia nguvu ya vyombo vya dola kupiga na kuumiza raia wake wanaosimami haki kuidai katiba au tume huru ya uchaguzi kwa njia halali, basi ikitokea hivyo ujue mtawala huyu atajiuhukumu mwenyewe kwa mkono yake au uzao wake.Huwezi kuidai katiba mahakamani huku ukijua majaji wote ni wateule wa watawala, hata wakikutendea haki huwezi kuwaamini.

Tuwasaidie wananchi hawa kuondokana na mdudu chuki,visasi,ubaguzi,dharau na maneno yenye vuashiria vya kuligawa taifa. Ni wajibu wetu kuwaelimisha kua nia yetu ni nini kwa ustadi wa hali ya juu! Watawala hawana jipya mbele ya wananchi zaidi ya kutumia nguvu nyingi kuwafanya wawaamini.

Kama ni ujasiri wa kuidai tume Huru ya uchaguzi na katiba mpya uanze sasa, Mzee JK alipata misukumo ya kulikamilisha jambo hilo lakini kubweteka kwetu kulimfanya zaidi kuomba hilo lisifanikiwe ilimradi tu uchaguzi upite ili chama chake kikajipange upya na ndio maana tunaona yanayotokea hivi sasa! CCM ilikua ipotee kabisa 2015 lakini sisi kuwachekea ndio kumezaa yote haya.

Historia inaonesha kua hakuna mpinzani wa kweli ambaye amefanikiwa kwa kuogopa jela/mahabusu,virungu vya wanausalama au kufunguliwa rundo la kesi mahakamani na wengine hukimbia nchi zao. Ukiona mtu anapiga kelele kama yule ndege akirushiwa mshale mmoja kakimbia ujue kua huyo si mpinzani, ni kati ya wale wachezao na akili za wananchi wakiwa hawana dhamira ya kweli.

Nasema hivi tuwaachelia tu CCM waendelee kututawala kwa sababu tumekosa mbinu za kushindana nao, tuwaachie tu kwasababu wao wana dola! maana hili ndio neno kuu linalotutia woga kufanya mambo ya msingi bila kuogopa mkono wa mtu ilimradi ni utaratibu wa halali kisheria.
 
Ku

Kwa akili yako kuna Kiongozi huko upinzani anayetosha kupewa Nchi kweli?
 
Viongozi wetu wa upinzani wanaogopa sana kupigwa virungu kwenye maandamano na kwa woga huo tutatawaliwa na ccm milele. Ccm haita badilisha tume ya uchaguzi wala katiba kwa maneno.
Zanzibar SUK ilipatikana baada ya maandamano ya 2001.
Tukifanya maandamano ya mara kwa mara tutapata katiba mpya na tume huru. Lazima tulipie gharama za mabadiliko.
 
Watanzania wanaham na mabadiliko ya chamaa, tatizo upinzani wanajichanganya dakika za mwishoniii. Mfano mwaka juzi ilikuwa ni halali ccm waondoke madarakani kabisaaa, lakini hawa wapinzani walichowafanyia watanzania ilikuwa ni aibu kubwaa. kile kitendo cha kusubiri waliokatwa ccm halafu ndo wawe wagombea na huku watu hao waliku wa na tuhuma na kashifa mbalimbali, kilitukasirisha wanainchiii.
Kwahiyo mleta maada ni kwamba tatizo sio katiba wala tume, tatizo upinzani wetu tanzani hauna mwelekeo sahihi ndio maana wanainchi wanaamua ni bora ccm ibakie madarakani milelee.
Na siku kukitokea upinzani wenyeweredi ushindi wao utakuwa wakihistoriaa
Kwa sasa hamna chama kinachofaa kama ccm
 
Nami nafikiri hili ndio tatizo kubwa mkuu, maamuzi hayatoki nyoyoni.
 
Viongozi wetu wa upinzani wanaogopa sana kupigwa virungu kwenye maandamano na kwa woga huo tutatawaliwa na ccm milele. Ccm haita badilisha tume ya uchaguzi wala katiba kwa maneno.
Zanzibar SUK ilipatikana baada ya maandamano ya 2001.
Tukifanya maandamano ya mara kwa mara tutapata katiba mpya na tume huru. Lazima tulipie gharama za mabadiliko.
Unachosema ni sahihi mkuu, hilo liko wazi na ndio maana nikasema kua hatuhitaji darasa kulipihania hilo maana kumbukumbu tunazo.CCM hawawezi kuachia madarakani kwa kuwachekelea,tazama ya Zenji 2015. Bulembo alisema watatoa kila kitu lakini sio Ikule, sasa upinzani wa nini? Si ufutwe tu ndugu yangu?
 
Wanatosha sana, tunao watu wenye shule zao na wengine walikua hata mawaziri kwa serikali zilizopita na waliongoza vyema tu.
 
Issue siyo Uongozi hapa ni Tume.ya Uchaguzi na uandikishwaji upya wa Daftari. bila hayo mawili tusitegemee kupata wabunge na madiwani wengi.

CCM wanatumia polisi ,jeshi,tume na mahakama kukiuka haki za RAIA.Na Sasa po busy kuweka MTU wao TLS hawaamini katika ushindani.Hawaamini katika utawala wa sheria.Muda wote akili ya CCM ni RAIA tu wenye maovu.

Tumeona wakikwapua raslimali za Taifa lakini wanajitetea ati hawafukui makaburi Sasa ona kwa walio support Wapinzani wanachofanywa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Watanzania wanaham na mabadiliko ya chamaa, tatizo upinzani wanajichanganya dakika za mwishoniii. Mfano mwaka juzi ilikuwa ni halali ccm waondoke madarakani kabisaaa, lakini hawa wapinzani walichowafanyia watanzania ilikuwa ni aibu kubwaa. kile kitendo cha kusubiri waliokatwa ccm halafu ndo wawe wagombea na huku watu hao waliku wa na tuhuma na kashifa mbalimbali, kilitukasirisha wanainchiii.
Kwahiyo mleta maada ni kwamba tatizo sio katiba wala tume, tatizo upinzani wetu tanzani hauna mwelekeo sahihi ndio maana wanainchi wanaamua ni bora ccm ibakie madarakani milelee.
Na siku kukitokea upinzani wenyeweredi ushindi wao utakuwa wakihistoriaa
Kwa sasa hamna chama kinachofaa kama ccm
Walisema JK anataka kurefusha muda madarakani kwa kigezo cha katiba. Wapinzani hawaeleweki, macho yao yanaona mambo yaliyo karibu sana.

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Sasa hivi ni issue ya madawa ya kulevya kwanza!! Unataka tume huru ya nini?? Inayoruhusu kiongozi kuuza dawa za kulevy?
 
Back
Top Bottom