Wapinzani tunaanza kusherehekea ushindi 2020

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Jamani wapinzani tumekwisha shinda uchaguzi huu

mbinu zetu za ushindi ni

1. Kwanza kila chama cha upinzani mkakati wetu wa kwanza ni kuwaeleza wapiga kura umuhimu wa kwenda kupiga kura kuwa sio tu kumchagua raisi bali ni pamoja na kuvipatia nguvu vyama vya siasa ili vijiendeshe. Tumepanga kuwaeleza wapiga kura kuwa ukiona vyama havina ofisi, havina watumishi n.k katika maeneo yao ni kwa sababu vyama hivi havipati ruzuku.

kuna fungu la fedha linatengwa na serikali la kuendesha vyama vya siasa na asilimia ya kura za uraisi kinazopata chama ndiyo mgao wa fedha chama hicho kinapokea katika fungu la ruzuku linalotolewa na serikali.

Ni lazima wananchi tuwaeleze umuhimu wa kuwa na vyama vingi, tuwakumbushe maisha ya miaka ya 80 na 90 ya mwanzo.

mimi ingawa nilikuwa bado niko shule lakini nakumbuka kule kwetu kilo moja ya kahawa ilikuwa sh 25 lakini mfumo wa vyama vingi ulivyoingia tu kilo ikapanda na kufikia sh 300. wapo wasiofanya tafiti wanaoweza kuhoji kama vyama vingi vilipokuja vilinunua kahawa?

hawa tutawakumbusha maisha ya zamani ya biashara isiyo na ushindani, pale bukoba mjini kulikuwa na duka moja tu ambalo watu walikuwa na uhakika wa kupata bidhaa. Enzi hizo alikuwa akiona wateja mmekuwa wengi anafunga duka anasusa kuwa siuzi na mnakaa nje kusubiri afungue. na mlisubiri kwa kuwa hamkuwa na mahali pengine pa kwenda. Huu unaitwa ushindani, jambo lolote linapokuwa halina ushindani watu mtafanyiwa vyovyote vile.

Hivyo lazima tuwaeleze wananchi athari za kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja ni kurudi kwenye maisha ya akitokea mtu akaturudisha kwenye mambo ya hovyo hatutakuwa na namna.

Hivyo ni lazima tuwaeleze watanzania, kila mwenye kupenda demokrasia ya vyama vingi iwepo, ajitokeze kupiga kura yake pia kuvigawia vyama vidogo ruzuku ili vijiendeshe.

ni lazima tuwaeleze matokeo ya kuvipa vyama hivi ruzuku ni nini? ili viwe na ofisi na vyenyewe vijiendeshe. vijiari watumishi hivyo tunatengeneza ajira pia kupitia kura zetu. vyama hivi havisimamishi wagombea wenye sifa ni kwa sababu vinaonekana ni masikini lakini tukiviwezesha maana yake tunavipa uwezo wa kusimamisha wagombea na watoto wetu hawa na sisi wenyewe ndiyo tutapata fursa za kugombea huko.

2. Mbinu yetu ya pili ya ushindi ni sote tumekubaliana kuhamasisha mafuriko ya wapiga kura katika uchaguzi huu. mafuriko haya tutayapata iwapo hatutakaa mbele ya wapiga kura kuwakatisha tamaa kuwaeleza hata mkitupigia hatuwezi kushinda kwa sababu sijui ya tume au nini......... Hatuendi kwa wananchi kulalamika bali tunaenda kwa wananchi kuwapa matumaini na kuwaeleza wao ndio waamuzi, ndio wenye nguvu na nguvu hizo ni kura yao.

ni lazima tuwaeleze wanayotegemea kusikia na sio kuwataka kuwaeleza tuliyonayo sisi. kwanza ni lazima tuwaahidi watanzania wote kuwa lengo letu wapinzani ni mambo yote mazuri ambayo yamefanywa na awamu zilizopita zote tutayaenzi na yale ambayo hayajakamilika tutayakamilisha. Tusirogwe kutafuta kuwaambia wananchi kuwa nyeusi ni nyeupe na nyeupe ni nyeusi tukitegemea watuelewe na kutukubalia. Msimamo wetu ni jambo lolote ambalo ni zuri kwa watanzania sisi tutaliendeleza.

lakini cha ziada sisi tunachotegemea kufanya ni kurekebisha makosa yote yalifanywa na awamu zilizopita na hapa tusijaribu kujitazama sisi wanasiasa huo ni ubinafsi, hapa lazima tutazame wananchi, mishahara, masoko ya mazao mbalimbali, ukuzaji wa taaluma mbalimbali, uendelezaji wa michezo, kufungua masoko ya wasaniii kama waigizaji, muziki, kuwezesha wataalamu wa ndani n.k

kwa tathmini fupi mimi niliyoifanya kwenye chaguzi zilizopita ni kwamba wafuasi wetu wengi huwa hawapigi kura na sababu kubwa ni vyama vyetu vya upinzani kufanya kampeni zinazoonyesha wapinzani hawawezi kushinda na kuchukulia watu wengi kuona kupiga kura hakuna maana. Ni lazima tukomeshe tabia hii. Tutalalamika lakini sio kwa wapiga kura.

Ni lazima kila mmoja wetu ampe sababu kila mtanzania ya kujitokeza kupiga kura na kumuaminisha kura yake ina thamani sana na ina nguvu ya kuleta mabadiliko na mabadiriko tunayoyapeleka kwa wananchi ni kubadirisha maisha yao sio mababdiriko ya kujitazama wanasiasa.

WAPINZANI TUMEKWISHA SHINDA LAKINI BADO TUNATAKIWA KUFANYA KAZI KUBWA KUSHEREKEA USHINDI HUU
 
Back
Top Bottom