Lizarazu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 6,334
- 7,868
Assalumu alaykum ndugu zangu waislamu na kwa wakristu wenzangu tumsifu yesu kristu.
Ni jambo linalofahamika kwa kila mtanzania kwamba ile miaka mitano mizito chini ya serikali dhalimu ya CCM inayoongozwa na Rais Magufuli atimae sasa inaelekea kufika tamati.
Ni takribani miezi kumi na wiki tatu zimebaki kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ambapo Watanzania watapata nafasi adhimu ya kuchagua viongozi wa kisiasa watakaowaongoza kwa miaka mingine mitano ambao ni madiwani, wabunge na Rais.
Kama inavyofahamika tu kwenye uchaguzi huo mchuano ni kati ya CCM na vyama vya upinzani hasa vile vyenye nguvu, wakati CCM ikitaka kuendelea kutawala na kurudisha viti vyote ilivyopoteza kwenye chaguzi za huko nyuma na tayari kuna dalili zote, lengo kuu la upinzani pia ni kuing'oa CCM kwenye kila nafasi iliyoshikiri kuanzia ngazi ya urais.
CCM kikiwa kama chama dola kina faida kubwa dhidi ya vyama pinzani kuelekea uchaguzi huo, maana chenyewe ndio kinachounda serikali ambayo ndio ina ratibu zoezi zima la uchaguzi na hivyo kutoa mwanya wa wao kujiandalia mazingira ya ushindi kwa urahisi sana.
Kwa kuangalia duru ya kisiasa iliyopo hapa nchini kwetu hasa kwa awamu hii ya tano ni ngumu kusema kwamba CCM imepoteza imani kwa wananchi na pia vile vile ni ngumu kusema wananchi bado wana imani na CCM.
Ninachomaanisha hapa hasa ni kwamba wanaopenda kuendelea kuongozwa na CCM wapo na pia vile vile waliochoshwa na CCM wapo tena wengi tu.
Mimi ni mmoja wa waliochoshwa na utawala huu wa CCM na sitamani kabisa kuona ukiendelea kwani hata hii miaka mitano tu yenyewe nimeiona ni kama miaka nane.
Nakubali yapo mambo yenye tija kitaifa yaliyofanywa na awamu hii tuliyonayo lakini hayajanishawishi hata kidogo kuona kwamba inastahili kuendelea kuniongoza, kwani mimi hayo ninayachukulia kama ni misplacement of priorities (kukosewa kwa vipaumbele).
Sasa basi, matazamio yangu ni kuona upinzani ukiiondosha serikali ya CCM mnamo mwezi October mwaka huu na kutengeneza serikali yenye sura mpya kabisa tangu kuzaliwa kwa taifa hili.
Lakini katika kuwaza hayo kuna maswali kadhaa ninajiuliza:
- Kwa hii miaka minne na nusu upinzani wetu umejiandaa vipi hili kuhakikisha kwamba hilo linawezekana?
- Je, viongozi wa upinzani wamejipanga vilivyo kukabiliana na zile dosari/figisu figisu zilizokuwa zinatunyima nafasi ya kushika dola kwenye chaguzi za nyuma endapo kama zitatokea tena mwaka huu? Au Kuna chochote tulichojifunza kwenye chaguzi zilizopita?
- Je, wapinzani tuko tayari kuingia kwenye uchaguzi chini ya muongozo wa katiba ile ile ambayo ndio kikwazo kikuu miaka yote?
- Je, wapinzani tuko tayari kuingia kwenye uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi halafu tutegemee matokeo tofauti na tuliozoea kuyaona?
- Je, Kuna uwezekano tukaona yale yaliotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana yakitokea na kwenye uchaguzi mkuu?
- Je, silaha pekee ya upinzani waliyonayo sasa ni kutegemea foreign interference (ufuatiliaji wa kigeni) kwenye uchaguzi mkuu hili kuhakikisha zoezi linaenda kidemokrasia?
- Je, kuna haja ya kutegemea ushindi kweli hasa kwenye kiti cha urais au ndio tujiandae kisaikolojia?
- Je, kuna mgombea sahihi aliyeandaliwa vilivyo kuchuana na Rsis Magufuli kwenye kiti cha urais?
Karibuni kwa michango wana jamvi.
Asanteni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Maoni ya wadau:

Kuna theories 2 hapa za kuangalia
1. Tuchukulie kwamba hakuna Figisu zozote je Upinzani umejipanga na una sifa ya kushinda.
2. Je kwa figisu zilizopo kama zipo Upinzani una nafasi na umejiandaa kushinda?
Bahati mbaya umejikita kwenye Dhana no.2 ukiacha theory no.1.
Mimi naanza na no.1.
Kwamba, assume uwanja sawa wa ushindani viashiria vikoje?
1. Idadi ya wanachama ni muhimu kupima uelekeo kwa sababu 85 ya wanachama hukipigia chama chao pasi kuangalia sababu zingine yaani chama kwanza.
Mpaka leo CCM wanadai wana wanachama 15 milion by Polepole wakati CHADEMA wanadai wana 6 milion by Mbowe.
Sasa hapo jiulize nani ana fursa ya kushinda.
2. Potential Candidates, je vyama vina wagombea bora wenye uwezo wa kushindana na wenye ushawishi na fursa kubwa ya kushinda?
Hebu angalia hili kwanza; ni majimbo/kata ngapi ambazo CCM hupita bila kupingwa kwa sababu hakuna mgombea wa upinzani aliyejitokeza (sio wale waliofanyiwa figisu au kununuliwa) kwa mfano serikali za mitaa kabla ya figisu, 15% ya nafasi gombewa wapinzani hawakusimamisha wagombea (rejea salam za mwaka mpya za Kamanda Lissu).
Hapa pia kuna suala la ubora wa wagombea, katika chaguzi kadhaa tumeshuhudia Wapinzani wakija na wagombea dhaifu wasiokubalika katika jamii na mara nyingi wamekuwa wakisubiri kufaidika na minyukano ndani ya CCM (kusalitiana) pamoja na wale walioachwa na CCM ndio wawateuwe kugombea upinzani mfano mzuri ni Lowasa kwenye Urais na watu kama Cecil Mwambe (Ndanda) au
Kalanga wa Monduli.
Takriban asilimia 40 ya walioshinda Ubunge upinzani wamepatikana kwa mfumo huu.
2. Maeneo yenye Ushawishi (Political Strong Holds). Pemba ni ya CUF (samahani nasikia siku hizi ni ACT), Arusha, Kilimanjaro, Mara, Dar, Kigoma Mjini ni maeneo ambayo kwa 100% upinzani unatazamiwa kushinda majority (haya ni maeneo ambayo hata figisu figisu haziwezi kubadili matokeo).
Upinzani una maeneo mangapi kama haya kujihakikishia ushindi?
Pia tuangalie Rekodi nzuri ya utendaji kwa wapinzani walioko madarakani, this is a starting/running capital.
Hivi tukiacha ushabiki na upenzi wa vyama tunaweza kusema kwa dhati kwamba diwani au mbunge wangu toka upinzani amejipambanua kwa utendaji bora, kujitoa na kujituma ipasavyo?
Au tutakuwa na hoja kwamba tulitengwa au mbunge hakusanyi kodi?
Tunaweza kutembea kifua mbele na kujidai kwamba kata, majimbo na halmashauri zinazoongozwa na wapinzani ni mfano wa kuigwa na ndio BORA kuliko CCM. Au tunakuja na visingizio kibao.
Kubwa zaidi Vyama vyetu vimejipangaje na vimesimamiaje ubora/utendaji wa wagombea iliosimamisha au kuwadhamini?
Je tunaweza kusema kwa dhati kwamba kwa kazi nzuri iliyofanywa na diwani au mbunge huyu wa Upinzani mtu yoyote anaweza kuiona na kumchagua tena bila kujali uchama?
Kwa kuchelea kuchosha msomaji niishie hapa nikiwa nimeangalia dhana moja ya kwanza kabla ya kuangalia figisu zilizopo ambayo ni dhana ya pili.
TUJIPIME