Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,361
- 38,604
Kila siku tunawasikia viongozi toka vyama vingine vya siasa wakidai kutokuwepo kwa Tume "Huru" ya uchaguzi ndiyo sababu kuu ya kushindwa kuitoa CCM madarakani. Lakini sijawahi kusikia maelezo ya kina kuelezea tume huru ya Uchaguzi ni nini hasa. Hivi ili Tume ya Uchaguzi Tanzania iwe "huru" inatakiwa iweje?